Kuna jamaa yangu aliazima external akaja akaondoka nayo, nikamuomba anaiagizie akakubal, hakuagiza nikafanya hivyo mara 4 kwa nyakati tofauti hakuagiza pia, nikamuagizia jamaa yangu mwingine alikuwa anaenda aliko mkoani ampe akawa hapokei simu na sms hajibu hatimaye akamgei. Nimeampa sitokuja kuazimisha vitu vyangu tena, Mwingine nilimuazima screw drivers zangu akapoteza, akaomba alipe hajalipa hadi leo.
Jamaa mwingine aliomba nimnunulie HDD akawa na hela pungufu, nikamdanganya kuwa muuzaji tunafahamiana kasema tulipe ndani ya siku 4,lakini nilitoa hela yangu ya mfukoni ili nilipe nikitaka ye akija kuleta inakuwa tu yangu. Ni week ya pili hii hatutafutani.
Rafiki zetu wanachangia kwa kiasi kikubwa sana kurudisha mafanikio yetu nyuma