Watu Wazima Vikojozi !!

Watu Wazima Vikojozi !!

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
24.jpg
Kikojozi, au Nocturnal enuresis kwa Kiingereza
Kikojozi ni jina analopewa mtoto anayekojoa kitandani hasa wakati wa kulala.

Ni kawaida kwa watoto walio na miaka 6 kukojoa wakiwa usingizini.
..............
Lakini unajua kuwa watu wazima, akina baba na masharubu yao, au hata akina mama na vyeo vyao ni vikojozi?
Wataalam wanasema karibu watu wazima wote wamewahi kukoja vitandani wakiwa usingizini.
Utafiti unaonyesha kuwa wengi ya watu vikojozi ni wanaume. Wanaume wengi hujikojolea usiku

Kwa USA ni afadhali ukojoe kitandani lakini sio kukojoa nje,
mama mmoja huko Oklahoma , anajuta kwanini alimwambia mtoto wake wa miaka 3 kukojoa nje.
Mtoto huyo Dillan Warden alikuwa amebanwa sana na mkojo, hivyo mamake akamuonya asikojoe kwenye suruali yake. alipofika mahali kando palipojificha , Bi Ashley Warden akimvua mwanawe suruali ili ajisaidie.
Mara polisi wakafika pale, maskini mtoto huyo wa miaka 3 akakamatwa na kutozwa faini ya dola 2500/- kwa kukojoa hadharani.
..........
Lakini kwa nini mtu mzima na heshima zake au msichana mrembo awe na matatizo ya kukojoa kitandani?
Mtu kuwa na stress,au msongo kuna weza kumsababishia mtu matatizo ya ukojozi.
Mheshimiwa mmoja , mkuu fulani serikalini, Afrika mashariki ni kikojozi, lakini anamshukuru mkewe kwa kumvumilia.
Wewe unaweza kumvumilia mkeo au mumeo akiwa kikojozi??

Unajua kuwa Tanzania ina idadi kubwa zaidi ya watu wazima wanaokojoa vitandani kuliko Kenya na hata Uganda?
Tanzania ina watu wazima vikojozi, laki 8 ! Kenya inafuata karibu kabisa kwa kuwa na wanaume na wanawake laki 6.
Wanasayansi wanasema tatizo hilo la watu wazima kukojoa ni kubwa na linasumbua wengi lakini kwa sababu ni jambo la aibu wengi hawataki kulijadili.
Kuna mameneja wabunge na hata mawaziri ambao ni vikojozi
Takwimu zinasema kwamba katika kila watu wazima 100 wawili wao ni vikojozi.

Jee unajua kuwa nchini Uingereza kuna chama cha vikojozi? Watu wazima wanaokojoa wakiwa usingizini mjini
London wameanzisha chama kinachoitwa The Bladder And Bowel Foundation.

Source: BBC
 
Hiyo fine ya kukojoa njiani ingewekwa huku, tungeweza kulipa madeni yote. Kama umtu mzima na bado unajikojolea utakuwa mgonjwa na ni maradhi yanayotibika.

Boflo hizo takwimu za TZ vs KY umezipata wapi
 
Last edited by a moderator:
Looh!!
Me nilidhani ni ule mkojo utokao baada ya kufanya tendo la ndoa.
 
hiyo fine ya kukojoa njiani ingewekwa huku, tungeweza kulipa madeni yote. Kama umtu mzima na bado unajikojolea utakuwa mgonjwa na ni maradhi yanayotibika.

boflo hizo takwimu za tz vs ky umezipata wapi

Bbc .....
 
Nilidhani niko peke yangu, kumbe tu wengi hivi! Naona nasi inabidi tuanzishe umoja wetu ili tuwe tunachangiana kununua pampasi.
 
Bofloooooooooooo at work
Ahsante mkuu kwa kutuhabarisha jambo muhimu, huyu mkuu wa nchi ya Afrika Mashariki atakuwa ni JK
 
Hii sio shida kubwa, kama mtu ameshajua ana shiida ya kukojoa basi asinywe vitu vya majimaji kabla ya kulala akajisaidie before kulala na katikati ya usiku mtu amuamshe au atege alarm aamke kujisaidia, na mara nyingi unakuta mtu anazembewa toka utotoni hadi anakua inakua problem, though kuna baadhi ni matatizo ya vibofu n the like ambao wanahitaji utaalam wa kidaktari zaidi
 
Nilidhani niko peke yangu, kumbe tu wengi hivi! Naona nasi inabidi tuanzishe umoja wetu ili tuwe tunachangiana kununua pampasi.

naomba mimi na wewe tuanzishe vugu vugu hilo.... watu laki 8 vikojozi...!
Hilo litakuwa bonge la NGO, na wafadhili lazima wamwage mihela na misaada mingine ya kitabibu na hapo ndo tutasema umasikini kwaheri....LOL
 
naomba mimi na wewe tuanzishe vugu vugu hilo.... watu laki 8 vikojozi...!
Hilo litakuwa bonge la NGO, na wafadhili lazima wamwage mihela na misaada mingine ya kitabibu na hapo ndo tutasema umasikini kwaheri....LOL
Kwani na wewe kikojozi? Membership ni kwa vikojozi peke yake.
 
Back
Top Bottom