barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Watu wasiojulikana wameiba na kutokomea na CCTV(camera) zilizowekwa kandokando ya mipaka ya vijiji na mbuga ya Hifadhi ya Ruaha(Ruaha National Park) katika Tarafa ya Pawaga na Idodi.
Kamera hizo ziliwekwa na mamlaka husika ili kuzuia vitendo vya ujangili vinavyofanywa na majangili wakubwa wanaofadhili wanakijiji wa vijiji vilivyochini ya MBOMIPA kuhujumu maliasili na wanyamapori katika hifadhi ya Ruaha.
Kuondolewa/kuibiwa kwa kamera hizi kunaongeza uwezekano wa kuendelea kwa ujangili na wizi wa mali katika mipaka na ndani ya mbuga ya Ruaha iliyoko kati ya mikoa ya Iringa na Mbeya.
Mamlaka husika zimeanza uchunguzi kubaini wote waliohusika na uwizi huo wa kamera maalumu za kufuatilia ujangili.
Siku kadhaa barafu wa JF nilileta uzi huu Mh. Kigwangalla, karibu Maliasili na Utalii. Anza na hawa majangili wa Ruaha National Park kumpa changamoto Waziri wa Maliasili Mh.Hamis Kigwangala kuanza na majangili wa Ruaha National Park,na siku kadhaa baadae,majangili hao wameshirikiana na wanakijiji wa vijiji vya MBOMIPA kwa kuwarubuni ili kuendeleza uwizi.
Hizi ni changamoto za sekta ya utalii na ujangili katika Wizara ya Mh.Kigwangala,tunamsihi tena na tena,hii ndio wizara ambayo wadau wana pesa kuliko waziri.Aingie kwa step...Kupotea kwa CCTV huko Ruaha National Park ni salamu kwa Mh.Kigwangala.