Serikali Imeifuta Hifadhi ya Taifa Kigosi Tabora Huku Ikipunguza Ukubwa wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,060
49,748
Serikali Imefuta Hifadhi ya Taifa ya Kigosi Mkoani Tabora Huku Ikipunguza karibia robo ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mkoani upande wa Mbeya.

--
Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani ameipongeza serikali kufuatia juhudi za kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na hivyo kufuta Hifadhi ya Taifa ya Kigosi ambayo ilizuia kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo ufugaji na kuwakosesha wananchi wa maeneo jirani kufanya shughuli endelevu za kiuchumi ndani ya hifadhi hiyo.

Cherehani ameiomba serikali kuwasajili wananchi ambao watafanya shughuli endelevu katika eneo hilo husasani wafugaji wa nyuki pamoja na wavuvi ili waweze kutambulika na kurahisisha usimamizi mzuri wa shughuli hizo.

Itakumbukwa hifadhi hiyo imesababisha kukosekana kwa fursa hizo kwa wananchi ambapo Serikali imeona ni vyema kufuta Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi ambao utasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Sheria ya misitu sura 323 ina ruhusu kufanyika kwa shughuli za kiuchumi ndani ya Hifadhi za Misitu kwa kuzingatia matakwa ya uhifadhi na utaratibu maalum.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Kufuta Hifadhi za Taifa wakati Kuna mapori kibao ambayo sio Hifadhi ni Sahihi?

--
Bunge la Tanzania leo limepitisha maazimio mawili ambayo moja ni, Azimio la Kuridhia Kufanyika Marekebisho ya Mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, pili ni, Azimio la Kuridhia Kufutwa kwa Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu Kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi.

Serikali imeona ni vema kufuta Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi ambao utasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ambapo pamoja na mambo mengine itatoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli za kiuchumi kwenye eneo hilo kwani sheria inaruhusu kufanyika shughuli hizo ndani ya hifadhi za misitu kwa kuzingatia matakwa ya uhifadhi na utaratibu maalum.

Aidha, uamuzi wa kurekebisha mipaka utakuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo kutoa eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 478 ambalo litamegwa kutoka kuwa sehemu ya hifadhi kwenda kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo na ufugaji katika vijiji 29.

Aidha, manufaa mengine ni kutunza vyanzo vya maji na kuboresha mifumo ya ikolojia katika Bonde la Usangu, kuimarisha uhifadhi wa maliasili, kuondoa migogoro ya mipaka, kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa na kuwezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli nyingine za kiuchumi.

Chanzo: TBC
 
Utasikia muwekezaji kutoka Roma nchi ya wakatoliki anauziwa aweekeze
 
Serikali hata kama inafuta au kupunguza, ihakikishe inayapima hayo maeneo na kuyawekea miundombinu, kama watu walijenga hovyo pavunjwe papangwe upya
 
Ingekuwa vyema kuleta na andiko la wizara au mamlaka linalotoa sababu ya kufanya hv. Yaweza kuwa kwa sababu muhim,hebu fuatilia sio kutia huruma na lawama hapa jf
Soma hapo Juu ,gazeti limenukuu sababu za kufuta kutoka Kwa Wizara.
 
Serikali Imefuta Hifadhi ya Taifa ya Kigosi Mkoani Tabora Huku Ikipunguza karibia robo ya eneo la Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Mkoani upande wa Mbeya.

--
Mbunge wa Ushetu, Emmanuel Cherehani ameipongeza serikali kufuatia juhudi za kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na hivyo kufuta Hifadhi ya Taifa ya Kigosi ambayo ilizuia kufanyika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo ufugaji na kuwakosesha wananchi wa maeneo jirani kufanya shughuli endelevu za kiuchumi ndani ya hifadhi hiyo.

Cherehani ameiomba serikali kuwasajili wananchi ambao watafanya shughuli endelevu katika eneo hilo husasani wafugaji wa nyuki pamoja na wavuvi ili waweze kutambulika na kurahisisha usimamizi mzuri wa shughuli hizo.

Itakumbukwa hifadhi hiyo imesababisha kukosekana kwa fursa hizo kwa wananchi ambapo Serikali imeona ni vyema kufuta Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi ambao utasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Sheria ya misitu sura 323 ina ruhusu kufanyika kwa shughuli za kiuchumi ndani ya Hifadhi za Misitu kwa kuzingatia matakwa ya uhifadhi na utaratibu maalum.

Chanzo: Mwananchi

My Take
Kufuta Hifadhi za Taifa wakati Kuna mapori kibao ambayo sio Hifadhi ni Sahihi?

--
Bunge la Tanzania leo limepitisha maazimio mawili ambayo moja ni, Azimio la Kuridhia Kufanyika Marekebisho ya Mipaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, pili ni, Azimio la Kuridhia Kufutwa kwa Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu Kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi.

Serikali imeona ni vema kufuta Hifadhi ya Taifa Kigosi ili kuruhusu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Msitu Kigosi ambao utasimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) ambapo pamoja na mambo mengine itatoa fursa kwa wananchi kufanya shughuli za kiuchumi kwenye eneo hilo kwani sheria inaruhusu kufanyika shughuli hizo ndani ya hifadhi za misitu kwa kuzingatia matakwa ya uhifadhi na utaratibu maalum.

Aidha, uamuzi wa kurekebisha mipaka utakuwa na manufaa mbalimbali ikiwemo kutoa eneo lenye ukubwa wa Kilomita za mraba 478 ambalo litamegwa kutoka kuwa sehemu ya hifadhi kwenda kwa wananchi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi kama vile kilimo na ufugaji katika vijiji 29.

Aidha, manufaa mengine ni kutunza vyanzo vya maji na kuboresha mifumo ya ikolojia katika Bonde la Usangu, kuimarisha uhifadhi wa maliasili, kuondoa migogoro ya mipaka, kuongeza mchango wa sekta ya utalii katika Pato la Taifa na kuwezesha upatikanaji wa maji kwa ajili ya shughuli nyingine za kiuchumi.

Chanzo: TBC
kigosi ipo tabora kweli mkuu
 
Soma hapo Juu ,gazeti limenukuu sababu za kufuta kutoka Kwa Wizara.
Kwa Mkoa wa Tabora hifadhi nyingi zimevamiwa na wafugaji, wakulima wameanzisha hadi shule na zahanati wanyama wamekimbia misitu imekatwa Sana.
Kinachoendelea ni wanasiasa kutumia wavamizi wa misitu kama mtaji wa kisiasa.
Fuatilia habari za Wilaya za Sikonge na Kaliua misitu ilivyovamiwa
 
Back
Top Bottom