Watu Wanafanya Ibada ya Sanamu Bila Kujua

John Achila Mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
111
Reaction score
214
Watu Wanafanya Ibada ya Sanamu Bila Kujua

Ibada ya sanamu ni nini
Mara nyingi watu wamedhani kwamba ibada ya sanamu ni kuweka kinyago hapo mbele yako na kuanza kukiabudu. Kwa upande mwingine, watu wanashangaa wenzao ambao wana vinyago majumbani, mahekaluni, kazini, nk, na wakiviabudu na kuviita miungu yao. Ibada ya sanamu ni ibada kamili.

Baadhi ya watu wanaweza kuona kuwa hao wamepotea. Je, wanajua Mungu anavyoingalia ibada ya sanamu? Umewahi kujiuliza ni watu wangapi wanaabudu sanamu na hawajijui, huku wananyooshea wenzao vidole?

Hebu tuone maana ya mungu ili ujue ni nani mungu katikati yako.

Mungu ni kile ambacho unakipa kipaumbele na nafasi ya kwanza maishani mwako. Kwa ajili ya “mungu”, utafanya mambo uyapendayo na usioyapenda ili kumpendeza huyo “mungu” wako. Ukiweza kufanya vyema mambo upendayo na usiyoyapenda kwa ajili ya huyo “mungu”, utaitwa “mcha mungu”. Zingatia kuwa neno “mungu” limeandikwa kwa herufi ndogo, ikimaanisha kuwa hapo ni “kitu chochote” na siyo Mungu katika Yesu Kristo.

Katika agano la kale, kuabudu sanamu ni kitendo chochote cha kwenda kuabudu au kusujudia, au kutumikia kitu kingine chochote, tofauti na Mungu mkuu mmoja aliye hai (Yehova).

Siku hizi, sanamu bado ni chombo chenye nguvu ambacho shetani anatumia kututenga na Mungu. Na sanamu hizi zinaweza kuja kwa namna nyingi tofauti. Sanamu hizo zinaweza kuja kama raha za maisha, fedha, elimu, kila kitu ambacho watu hukiona kuwa cha juu sana au kinachoweza kuvuta mawazo yetu mbali na Mungu.

AINA ZA IBADA YA SANAMU
Hebu tuangalie aina tatu za sanamu zinazoabudiwa na watu. Aina hizo ni sanamu zenye mfano wa mtu; sanamu-watu; na sanamu-vitu.

1. Sanamu zenye mfano wa mtu
Hivi ni vitu vyote visivyo na uhai vyenye mfano wa mtu, ambavyo vinatengenezwa na watu kwa lengo la kuabudiwa. Kulingana na Biblia, tabia ya hizi sanamu ni kwamba, zina midomo lakini hazisemi, zina macho lakini hazioni, zina masikio lakini hazisikii, zina pua lakini hazinusi, na wanaoziabudu wanafanana nazo kiroho.
Kitabu cha Zaburi 115 kinasema: 4 “Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. 5 Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, 6 Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, 7 Zina mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. 8 Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia”.

Hizi sanamu ndiyo zile zote zinazoabudiwa na wapagani, pamoja na baadhi ya madhehebu. Kwa mfano, utakuta sanamu imewekwa ndani ya nyumba ya ibada, na watu wanakwenda kuiangukia na kuisujudia, hata kuitolea sadaka na kuiomba, jambo ambalo ni machukizo makubwa kwa Mungu. Kulingana na kitabu cha Kutoka 20:3-5, ni dhambi kubwa kusujudia sanamu yo yote ile.

2. Sanamu-watu
Hii ni aina ya sanamu ambayo ni tofauti kidogo na ile ya kwanza. Ile ya kwanza ina midomo lakini haisemi, ina macho lakini haioni, ina masikio lakini haisikii. Hii ya pili nayo ni hivyo hivyo, ina macho lakini haioni, ina masikio lakini haisikii, ina macho lakini haioni. Tofauti tu ni kwamba ile ya kwanza (sanamu mfano wa mtu), haipumui, ila hii ya pili inapumua. Ile ya kwanza imetengenezwa kwa miti, udongo, chuma, fedha au dhahabu, lakini hii ya pili ni wanadamu wenyewe.

Tuangalie maandiko katika biblia yanasemaje kuhusu sanamu hii.

Ezekieli 12:1
: “Neno la Bwana likanijia tena, kusema, 2 Mwanadamu, wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, ila hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi”.
Hii maana yake ni kuwa, sanamu siyo tu mawe na udongo vinavyoweza kuwa sanamu, bali hata watu ni sanamu.
Kama hujamaanisha kumfuata Yesu, wewe ni sanamu
. Kwa sababu una macho lakini huoni mambo ya rohoni, una masikio lakini husikii sauti ya Mungu, una kinywa lakini hakineni mambo ya Mungu, Hivyo, wewe ni sanamu pamoja na viungo vyako vyote. Hebu tuangaze kuhusu viungo.

Kichwa chako ni sanamu/mungu wako, ndiyo maana unakitumikia kwa vitu vya kidunia, kama Malkia Yezebeli.
Masikio yako ni sanamu/mungu wako, ndiyo maana unayatumikia kwa kubadilisha vipuli kila siku.
Macho yako ni sanamu/mungu wako, ndiyo maana unayatumikia usiku na mchana, kupaka uwanja, na kubadilisha kope na kuchonga nyusi.
Mdomo wako ni sanamu/mungu wako, ndiyo maana unautumikia kwa rangi na kila aina ya lipstick
Mikono yako na miguu ni sanamu/mungu wako, ndiyo maana unaitumikia kwa bangili na kucha za bandia.
Tumbo lako ni mungu wako ndiyo maana unalitumikia kwa kulinywesha pombe na kuliburudisha kwa kila linachohitaji usiku na mchana.

Huna muda wa kufunga na kuomba, walau kwa wiki mara moja, kwako kufunga ni adhabu kubwa.

Wafilipi 3:19 inasema: “mwisho wao ni uharibifu, Mungu wao ni tumbo, utukufu wao u katika fedheha yao, waniao mambo ya duniani”.
Ikiwa hujamaanisha kumfuata Yesu, kila kiungo katika mwili wako ni sanamu (mungu). Ndiyo maana biblia inasema tuvifishe viungo vyetu vilivyo katika nchi, maana kwa hivyo huzaa dhambi, na ndiyo ibada ya sanamu.
Kitabu cha Wakolosai 3 kinasema: 5 “Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu; 6 kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya Mungu”.
Kwa hiyo, kiroho, watu wenyewe, tu sanamu.

3. Sanamu-vitu
Hizi ni sanamu zote zisizo na muonekano au maumbile ya mwanadamu, lakni zinaabudiwa.
Mfano wa sanamu hizi ni kama vile kazi, fedha, umaarufu, elimu, mali kama nyumba, magari, ardhi n.k. Mtu akiwa na hivi na hana Kristo katika kuendesha maisha yake, yeye ni mwabudu sanamu.

Tukumbuke kuwa tusipomuabudu Mungu wa kweli, basi tunaabudu sanamu, na tusipoabudu sanamu basi tunamuabudu Mungu wa kweli. Hakuna katikati. Ni aidha uwe wa shetani au wa Mungu.

Kwa mfano, kama kazi yako ina heshima kuliko Mungu kiasi kwamba unakosa hata siku moja ya wiki kumtolea Mungu wako, hiyo kazi ni sanamu/mungu kwako.
Kama elimu yako, au umaarufu wako au cheo chako kina nguvu kuliko Neno la Mungu, basi hicho ulichonacho tayari ni mungu wako.

Tumeona kuwa kuabudu sanamu ni kitendo chochote cha kuabudu au kusujudia, au kutumikia kitu kingine chochote, tofauti na Mungu Yehova mkuu mmoja aliye hai.

Siku hizi, sanamu bado ni chombo cho chote chenye nguvu ambacho shetani anatumia kututenga na Mungu. Sanamu hizo zinaweza kuja kama raha za maisha, fedha, elimu, kila kitu ambacho watu hukiona kuwa cha juu sana au kinachoweza kuvuta mawazo yetu mbali na Mungu.

Tukumbuke kuwa kulingana na biblia (Ufunuo 21:8), wote wanaoabudu sanamu, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti: “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Hivyo, tuchambue matendo yetu, ili tuweze kubaini pale tunapoabudu sanamu, na kuacha. Pia, tujielekeze kwa Mungu, ambaye kwake, ibada za sanamu ni machukizo makubwa.
 
Ni kweli. Kuna msalaba, picha za wazungu, na minara inayotupiwa mawe kama shetani au kubusu au kuzunguka jiwe na kuzuru makaburi sehemu fulani.
 
Tukumbuke kuwa kulingana na biblia (Ufunuo 21:8), wote wanaoabudu sanamu, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti: “Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili”.
Hivyo, tuchambue matendo yetu, ili tuweze kubaini pale tunapoabudu sanamu, na kuacha. Pia, tujielekeze kwa Mungu, ambaye kwake, ibada za sanamu ni machukizo makubwa.
Naona hata huu mwenge hapa Tanzania ni ibadan kubwa sana ya sanamu, hili dude linaabudiwa nchi nzima. Ni laana hii.
 
Hahah Kuna watu wanaweka mpaka stika ya mtumishi kwenye magari ili gari lilindwe.
Waliwacheka wanaoweka sanamu mbele na kuanza kasali Sasa na wao wanaweka stika kwenye magari na nyumba ili zilindwe.

Hii ni ibada ya sanamu 100%
Mnakula nyama iliyo chinjwa na waislamu huku mkijua ...mfano wasabato wanajidai kutokula nguruwe ila nyama za mabuchani zina chinjwa na waislamu sawasawa na ibada zao inaelekezwa kibla na kutamkiwa maneno ya miungu yao
 
Mnakula nyama iliyo chinjwa na waislamu huku mkijua ...mfano wasabato wanajidai kutokula nguruwe ila nyamq za mabuchani zina chinjwa na waislamu sawasawa na ibada zao inaelekezwa k8bla na kutamkiwa maneno ya miungu yao
Mungu wetu siyo Ayatolaha Khamenei kwamba kajifungia kwenye mahandaki haoni na hawezi kututetea.

Mungu wetu ni moto ulao, neno lake ni upanga ukatao kuwili.

Mamlaka tuliyonayo kupitia ushindi wa Damu ya Yesu ni zaidi ya kuchinja.

Maagano yote hayana nguvu kwetu kupitia Damu ya Yesu.
 
Unatumia injili gani....injili Inasema usile chakula au mnyama aliye fanyiwa ibada zisizo faa za miungu ...na kama ukila iwe ni kwa kuto kujua ...sasa ni nani asiye jua kuwa nchini machinjioni mifugo uchinjwa kwa ibada za Kiislamu?
 
Angalau wagalatia wameanza kujitambua kua wanafanya ibada za kisanamu
Wakijitambua sawa sawa wataacha kula hata nyama za mifugo iliyo chinjwa kiislamu pia ....na kuhusu ibada ya sanamu waislamu mnaifanya tena ni moja ya nguzo zenu...ibada ya jiwe jeusi ni ibada kamili ya shetani na sanamu tena mnapunguza nguo za kujisitili mfanyapo hiyo ibada ...kwanini ibada izingatie kuwa uchi uchi
 
Bora wanaofanya ibada ya sanamu kuliko wanaofanya ibada ya imagination ya kitu wasichokijua
 
Mnakula nyama iliyo chinjwa na waislamu huku mkijua ...mfano wasabato wanajidai kutokula nguruwe ila nyama za mabuchani zina chinjwa na waislamu sawasawa na ibada zao inaelekezwa kibla na kutamkiwa maneno ya miungu yao
Unamaanisha kuna viumbe hawali vitoweo vilivyoandaliwa na Makafiri ila wanakula samaki walioandaliwa na Makafiri mabuchani au siyo Mkuu?

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Mnakula nyama iliyo chinjwa na waislamu huku mkijua ...mfano wasabato wanajidai kutokula nguruwe ila nyama za mabuchani zina chinjwa na waislamu sawasawa na ibada zao inaelekezwa kibla na kutamkiwa maneno ya miungu yao
Kwani kuna shida gani kula nyama iliyochinjwa na muislamu?
 
Bora wanaofanya ibada ya sanamu kuliko wanaofanya ibada ya imagination ya kitu wasichokijua
Kuna viumbe hawali vitimoto ila kipindi cha mfungo wao biashara hudoda balaa kwa wauzaji, Binadamu tuna unafki sana.

Dini ya kweli ni Mtu mwenyewe ila si kukariri vifungu vya maandiko matakatifu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Back
Top Bottom