Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Sasa hapa ni nani ana ignorance hata zikipigwa kura Kati yako wewe unayetetea taifa lisilo lako na mtoa mada anayetetea taifa lake?.
naanza kuwa na wasiwasi na wewe pengine ukiwa USA baby yako waliku Cameroon ndo maana ubongo wako umefyatuka.

Wasiwasi wako ndo maradhi yako.

I suggest you mind your own.
 
Mungu humpa MTU pesa hasa aanziapo 40 na kuendelea na ndio hudumu sana kwani uwezo kiakili unakuwa mkubwa kuliko Under 40,angalia waliochini ya Umri huo wenye pesa mwisho wao.....
Acha kujidanganya wewe komaa usikate tamaa
 
Kweli banaa wapo watu wengi sana ambao walivyokuwa vijana hawakuwa na muelekeo na baada ya miaka 40 na kuendelea wamekuwa matajiri wakubwa
unapofikisha miaka 40 hata uwezo wako wa kufikiri unakomaa zaidi na kuondokana na mawazo ya kitoto.

Madisko. Pamba na starehe. Hapa ndipo watu wanapo pevuka zaidi na kufikiria juu ya maisha.

Angalia vijana wengi sana wene umri chini ya miaka 40 ni wachache sana waliofanya mambo makubwa na yamaendeleo.

Nje na hapo ni kula bata kwa kwenda mbele mwisho wa siku unaishia kuokota makopo.
 
nafurai sana kwa mada nzuri sana yenye kuhamasisha watu waamke na kubadilisha fikra mgando na kuelekea kwenye safari ya mafanikio.

Niukweli usiopingika kwamba jamii kubwa hasa ya waafrika ni waathirika wakubwa wa fikra mgando na zimepelekea bara la africa kuonekana ni nchi maskini sana.

Embu tujiulize sisi waafica tunatofauti gani na wazungu nje ya rangi?

Wazungu ni kama sisi ila tofauti kati yao na sisi ni fikra au mawazo.

Waafrica wengi tunaangamia kwa kukosa maarifa, na wenzetu wazungu wamewekeza sana kwenye maarifa.

Na wanawafundisha watoto maarifa tangu wakiwa wadogo kabisa mashuleni na kujiamini.

Waafrica tumewekeza kinyume na wenzetu wazungu hatuwekezi katika Elimu, hatuwajengi watoto wetu katika kujiamini na kuaminiwa.

Tumewajenga watoto wetu katika hofu na kushindwa, hivyo mtoto ukua kutokana na malezi aliyojengewa tangu mtoto hivyo ulivyo ni matokeo ya mbegu uliyopandiwa tangu ukiwa mdogo.

Tazama watoto wa matajiri na watoto wa watu maskini uwapime kwa kufikiri kwao, utagundua watoto wa matajiri wana kitu zaidi ya watoto wa maskini.

Leo ukimwuliza mtanzania mapato na matumizi yako kwa mwezi kwa mwaka ni kiasi gani hajui.

Sasa kama hujui mapato na matumizi yako utawezaje kuwekeza?

Maana sisi wafanya biashara siri yetu kubwa na safari ya kuanza kuwekeza ilianzia hapo kwenye mapato na matumizi.

Watu wengi hawapendi kusoma vitabu. Na kuudhuria semina za ujasiria mali.

Matokeo yake ni kushinda kwenye smart phone, kuperuzi kwenye WhatsApp, Fb na kwingineko kazi kupiga domo na kutumiana picha za kijinga.

Wakati ungeitumia cm yako vizuri kutafuta maarifa ya kujifunza ili utoke hapo ulipo ungekuwa mbali sana.

Watu hawapendi kwenda kwenye maduka ya vitabu na kujinunulia vitabu vya elimu ya ujasiriamali na kujifunza.

Lakini kila ijumaa wananunua magazeti ya udaku na michezo maskini ya Mungu utamkuta kijana anajua habari za Manu kuliko hata wenye timu hiyo.

Utakuta kijana anajua habari za wema sepetu kuliko hata wema anavyojijua mwenyewe.

Wakati angetumia muda uo kutafuta maarifa angekuwa mbali sana.

Waafrica kuchangiana maharusi na ubarikio ni hodari sana lakini kuchangiana kwenye mambo muhimu ya maendeleo ni wavivu sana.

Nini hitimisho langu.
Ni kubadilika tunavyofikiri, kubadilika tunavyo tenda kujenga tabia ya kuwekeza kidogo ulicho nacho maana hakuna kikubwa kama hakikuanza kidogo, hakuna elf 1 kama hakuna mia 5

tuanze kujenga tabia ya kujisomea na kutumia smart phone zetu vizuri hakika utafanikiwa sana.
 
Dah....piga ua raha ya pesa ni matumizi...Ukiipata wakati hata mishkaki kwako huwezi kuitafuna ...utanunua iliyonona halafu utatafuniwa...[emoji13]
 
Upo sahihi kabisa,wengine pia wanadhani hata kupata degree baada ya 40 years haiwezekani...nimeanza masomo university at 43 yrs, currently mm MD (medical doctor) at 48 years...
 
Back
Top Bottom