Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Tena miaka hiyo unakuwa na hekima pia
 
Binadam tunatakiwa tupate kiasi gani cha mali ndio turidhike na maisha? Manake naona hata wamiliki wa makampuni ya Google Inc, Facebook, Samsung, etc.. hawalali usiku na mchana wanasaka kuongeza mpunga wakati accounts zinasoma $ 50+ B... ?
 
nafurai sana kwa mada nzuri sana yenye kuhamasisha watu waamke na kubadilisha fikra mgando na kuelekea kwenye safari ya mafanikio.

Niukweli usiopingika kwamba jamii kubwa hasa ya waafrika ni waathirika wakubwa wa fikra mgando na zimepelekea bara la africa kuonekana ni nchi maskini sana.

Embu tujiulize sisi waafica tunatofauti gani na wazungu nje ya rangi?

Wazungu ni kama sisi ila tofauti kati yao na sisi ni fikra au mawazo.

Waafrica wengi tunaangamia kwa kukosa maarifa, na wenzetu wazungu wamewekeza sana kwenye maarifa.

Na wanawafundisha watoto maarifa tangu wakiwa wadogo kabisa mashuleni na kujiamini.

Waafrica tumewekeza kinyume na wenzetu wazungu hatuwekezi katika Elimu, hatuwajengi watoto wetu katika kujiamini na kuaminiwa.

Tumewajenga watoto wetu katika hofu na kushindwa, hivyo mtoto ukua kutokana na malezi aliyojengewa tangu mtoto hivyo ulivyo ni matokeo ya mbegu uliyopandiwa tangu ukiwa mdogo.

Tazama watoto wa matajiri na watoto wa watu maskini uwapime kwa kufikiri kwao, utagundua watoto wa matajiri wana kitu zaidi ya watoto wa maskini.

Leo ukimwuliza mtanzania mapato na matumizi yako kwa mwezi kwa mwaka ni kiasi gani hajui.

Sasa kama hujui mapato na matumizi yako utawezaje kuwekeza?

Maana sisi wafanya biashara siri yetu kubwa na safari ya kuanza kuwekeza ilianzia hapo kwenye mapato na matumizi.

Watu wengi hawapendi kusoma vitabu. Na kuudhuria semina za ujasiria mali.

Matokeo yake ni kushinda kwenye smart phone, kuperuzi kwenye WhatsApp, Fb na kwingineko kazi kupiga domo na kutumiana picha za kijinga.

Wakati ungeitumia cm yako vizuri kutafuta maarifa ya kujifunza ili utoke hapo ulipo ungekuwa mbali sana.

Watu hawapendi kwenda kwenye maduka ya vitabu na kujinunulia vitabu vya elimu ya ujasiriamali na kujifunza.

Lakini kila ijumaa wananunua magazeti ya udaku na michezo maskini ya Mungu utamkuta kijana anajua habari za Manu kuliko hata wenye timu hiyo.

Utakuta kijana anajua habari za wema sepetu kuliko hata wema anavyojijua mwenyewe.

Wakati angetumia muda uo kutafuta maarifa angekuwa mbali sana.

Waafrica kuchangiana maharusi na ubarikio ni hodari sana lakini kuchangiana kwenye mambo muhimu ya maendeleo ni wavivu sana.

Nini hitimisho langu.
Ni kubadilika tunavyofikiri, kubadilika tunavyo tenda kujenga tabia ya kuwekeza kidogo ulicho nacho maana hakuna kikubwa kama hakikuanza kidogo, hakuna elf 1 kama hakuna mia 5

tuanze kujenga tabia ya kujisomea na kutumia smart phone zetu vizuri hakika utafanikiwa sana.
Facts[emoji108]
 
Hivi katika hiyo mifano hakuna mmoja kutoka Tanzania tukamtumia? Maana vingi vinavyowezekana Amerika/Europe huwa Africa vinashindikana
 
Wakuu salamu.

Ipo imani mbaya sana miongoni mwetu vijana, imani iliyopofusha akili zetu na kutufanya tuamini ujinga usio na kichwa wala miguu, imani ya kivivu kabisa na imani yenye roho ya mauti ndani yake.

Ya kwamba, kijana ukifikisha umri wa miaka 40 na bado unateseka kimaisha, yaani huna pa kulala na kula yako ya taabu sana basi kamwe huwezi kufanikiwa tena kimaisha.

Wakuu, imani hii ni ya kijinga kuliko ujinga wenyewe.

Kwanza kabisa nataka kuwaweka wazi ya kwamba, mafanikio namba moja hapa duniani ni "Afya ", kuwa na afya ndo baraka za kwanza kabisa ambazo Mungu humjalia mwanadamu.

Huwezi kuwa na mabilioni ya pesa benk halafu upo hospitali miaka mitatu umelazwa unaumwa ugonjwa ambao hauna tiba halafu ukawa na amani na au ukaifurahia pesa yako.Kiuhalisia maskini atakuwa na amani na furaha kuliko wewe Tajiri.Sasa twende kwenye mada.

Swali nalowauliza na ningependa sana wanijibu wanaosema kwamba ukifikisha miaka 40 huwezi tena kufanikiwa, nataka wanijibu, Kwa hiyo ukifikisha miaka 40 hujafanikiwa utakaa na kusubiria ufe?

Utakata tamaa kiasi kwamba hautajishughulisha kwa lolote kisa tu umefikisha miaka 40? Bahati mbaya ni kwamba kuna watu wana imani kabisa juu ya msemo huu haramu kwamba, "life starts at 40".

Henry Ford, mwanzilishi wa magari ya Ford alianzisha kiwanda cha kutengeneza magari hayo akiwa na umri wa miaka 45,hakuwa na pesa taslimu, alikuwa na mawazo tu, kupitia mawazo yake gari la Ford likatengezwa hadi kuwa kiwanda kikubwa na magari hayo kusambaa kote duniani, leo hii familia ya Ford ni matajiri wakubwa, alianza mwaka 1908,miaka 14 kabla Nyerere hajazaliwa.

Jack Weil, alianzisha biashara ya mavazi ya Cowboy akiwa na miaka 45 na alikuwa na mtaji mdogo sana, leo hii Cowboy ni maarufu pote duniani, Jack Weil amekufa mwaka 2008 akiwa tajiri mkubwa na akiwa na umri wa miaka 107.

Harland Sanders, akiwa na umri wa miaka 62 alistaafu kazi akiwa na mafao kidogo Sana, alichanganyikiwa kabisa akataka kujiua, alikuwa na hali ngumu mno kimaisha. Baadaye alipata wazo la kukaanga kuku na kuwawekea viungo vya kuvutia, na kisha akawa anawaweka kwenye makopo, alianza kuwatembeza nyumba hadi nyumba, mtaji ukakua akafungua kampuni, inayoitwa "Kentucky fried chickens "ndani ya miaka 12 alikuwa tayari ana dola mil mbili.

Mzee huyu amekufa akiwa tajiri.
929e5a8e6f7abd950c6615338669f688.jpg

Mzee Sanders enzi za uhai wake.

Kama huyu mzee aliweza inakuwaje siye vijana tunashindwa? Tunaona aibu kufanya biashara flani eti tutachekwa, huyo anayekucheka hawezi kukupa hata sh 500 ya chai.

Mwaka 2009 nilikuwa na rafiki yangu mwenyeji wa shinyanga, huyu jamaa alikuwa na miaka 48, aliishi maisha magumu sana, nyumba yake Ilikuwa ni ya tope na nyasi, baadaye Siku moja aliniambia, "Masesa, mimi pamoja na kuwa umri umeenda lakini siwezi kukata tamaa, hapa nimepata mbuga ya kulima mpunga hela tano ".

Na kweli msimu ulipofika alilima Kwa kujituma hasa, alipovuna akasubiria msimu wa mazao kupanda bei, aliuza kisha akaanzisha biashara ya duka kubwa, kila baada ya miezi kadhaa akipata faida anaongeza duka jingine, kufikia miaka miwili baadaye alikuwa na maduka 15. Alijenga nyumba nzuri sana kahama, tayari alikuwa amepata mafanikio. Bahati mbaya aliuawa na majambazi."Pumzika Kwa amani rafiki yangu Maduhu Ngeleja ".

Hakuna umri maalumu wa mafanikio, kinachomzuia mtu kufanikiwa ni ugonjwa na kifo au ulemavu basi. Zaidi ya hapo hakuna. La kuzingatia hata Kama una shida kiasi gani, tambua kuwa, hakuna usiku usio na mchana.

Naandika waraka huu siyo kwamba tayari nimeshafanikiwa, la hasha, nipo napigana kiume kutafuta mafanikio.

Naandika ili tupeane moyo kwa wale wenzangu na mimi waliokata tamaa kabisa, mara nyingi tunajifunza kwa watu waliofanikiwa na siyo walioshindwa.
Ingefaa ukawa JF man of the year!
 
Kibongo bongo ukishafikisha umri kama huo ndo bas tena labda ukatajirike peponi
 
Kibongo bongo ukishafikisha umri kama huo ndo bas tena labda ukatajirike peponi
Wewe ndo wale wale wenye akili mgando, kuna watu huwa wanafanikiwa wakiwa na miaka 25 tu, na baadaye hufilisika kabisa, lakini baadaye hupigana hadi kufanikiwa tena wakiwa wazee.
Unachokiwaza ndo kinachokutokea, ukiwaza umaskini utapata umaskini ukiwaza utajiri utapata utajiri.
Umri hata hauhusiani na utafutaji mafanikio, inaonekana wewe ukiwa na pesa Kama kina mzee Bakheresa huwezi tena kujishughulisha, utakaa na kuanza kula tu.
Usiwaone hao majambazi ukadhani walizaliwa wakiwa majambazi, Hapana, hao wamekata tamaa Kama wewe ndo wakaona hakuna mafanikio zaidi ya kupora, hiyo ni hatari Sana.
Mtu anafikisha miaka 47 bado hana mbele wala nyuma, anatamani mwanamke mzuri hawezi Kumpata Hana pesa, anatamani mambo mengi mazuri, anaona Kwa umri huu siwezi tena kufanikiwa ni bora tu nikapore benk, ndo anakutana na mauti.
Jitathimini Sana fikra zako, fikra zako ndo hatima ya maisha yako.
 
Back
Top Bottom