Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Watu waliofanikiwa baada ya umri wa miaka 45

Mafanikio yanapimwaje kwani?

Vigezi ni vipi na ni kwa mujibu wa nani na nini?
Mkuu, vigezo vya mafanikio ni ile hali ya kupata mahitaji muhimu ya kimaisha na Kwa wakati mwafaka.
1.Kuwa na nyumba bora pamoja chombo cha moto cha kutembelea.
2.Kuwa na uwezo wa kula chakula bora kila Siku na siyo bora chakula.
3.Kupata matibabu yenye kiwango kizuri pindi uuguapo.
4.Kuwa na uwezo wa kusomesha watoto wako ktk Shule Shule bora na siyo bora Shule.
5.Kuwa na uwezo wa kutatua shida ndogo ndogo Kwa wakati mwafaka.

Na mengine mengi yanayofanana na hayo ,mkuu hayo ndo mafanikio.
 
Ni kweli but Mara nyingi studies huwa zinaangalia percentage, yaani waliofanikiwa at 45 against wasiofanikiwa,so msibeze na you have to work hard kabla ya huo umri,kwanza hata kwa akili ya kawaida jinsi umri unavosonga ndo majority performance yetu inapungua na huo ndo ukweli
 
Una point

Ni afadhali ule msoto wa maisha ujanani lakini uje kula bata ukubwani na si kinyume chake.

Kweli Ndugu yangu halafu Mungu alivyo mkuu utashangaa anakuachaa unaishi maisha marefu hadi unakutana na wale uliokuwa ukiwaletea dharau.
 
Kwa nini ukate tamaa
Adamu mwenyewe licha ya kufukuzwa bustanini aliendelea na haso zake nje ya garden hadi kufa
Yesu mwenyewe licha ya kusulubishwa msalabani anaendelea hadi leo kuhakikisha anawaokoa wote kwa toba zao ingawa wameoza kwa dhambi wazitendazo
 
Mkuu, vigezo vya mafanikio ni ile hali ya kupata mahitaji muhimu ya kimaisha na Kwa wakati mwafaka.

Wakati muafaka ndo upi huo na ni muafaka kwa mujibu wa nani? Kuna muongozo maalumu unaoelezea na kuelekeza kuwa huu ndo wakati muafaka?

1.Kuwa na nyumba bora pamoja chombo cha moto cha kutembelea.

Nyumba bora ndo ikoje hiyo? Manake nyumba nyingi za Tanzania na ubora hakuna kitu kabisa.

2.Kuwa na uwezo wa kula chakula bora kila Siku na siyo bora chakula.

Chakula bora ndo kikoje hicho?

3.Kupata matibabu yenye kiwango kizuri pindi uuguapo.

Matibabu mazuri Tanzania? You can't be serious dude.

4.Kuwa na uwezo wa kusomesha watoto wako ktk Shule Shule bora na siyo bora Shule.

Mfano...?

5.Kuwa na uwezo wa kutatua shida ndogo ndogo Kwa wakati mwafaka.

Kama shida zipi kwa mfano?

Na mengine mengi yanayofanana na hayo ,mkuu hayo ndo mafanikio.

Mafanikio kwenye nchi yenye nominal GDP per capita ya $963?

Mafanikio kwenye nchi yenye HDI ya 0.521 ambayo ni karibu na ya mwisho mwisho huko?
 
Mimi nitaendelea kuutafuta u trillionaire hata nukiwa na 80 years. Japo pia jitahidi kuwa na mali angalao kwa 50 years uwe na vitu kadhaa ikiwamo nyumba japo.
 
Mkuu umesema neno zuri sana. Mtu hapaswi kukata tamaa.
Mfano mtu anaajiriwa serikalini miaka 30 anastafy na miaka 60.kama atajaliwa kuishi miaka 90 yaani mia mingine 30 je, haimpasi kutafuta zaidi na zaidi?
Mtu mmoja alistaafu mahali na miaka 60 akiwa na miaka 62 akajiunga na diploma ya ualimu sasa anazaidi ya miaka 70 anafundisha na anawatunza wajukuu na hajachoka.
Kwa hiyo mapambano ni wakati wote wa maisha ukiwa na afya.
 
Kuna Mzee mmoja mshauri wangu mkubwa wa kibiashara, alianza kampuni ya ujenzi ya umeme akiwa na miaka 48, na maisha ya kawaida sana. Sasa ni mtu mwenye zaidi ya Dola 500 millioni na Wafanyakazi karibu 200. Hakuwa na pesa alipoanza ila alikuwa na 1) Jina zuri, 2) Uzoefu wa kazi 3) Juhudi na maarifa 4) Heshima kwa kila mtu 5) Uaminifu 6) Uwezo wa kujifunza wengine na kusikiliza ushauri 7) Good communication.
 
Tatizo pesa ukizipata ukubwani sana huzifaidi yaani huli bata ipasavyo na tayari majukumu yanakuwa yashakuandama familia kubwa,ila bora uzidake ukubwani kuliko kufa maskini.
 
Mfano mwingine kwa hapa Tanzania baadhi ya wabunge wamekuwa na maisha mazuri baada ya kuingia kwenye siasa. Mfano sugu, nk
 
Back
Top Bottom