Mimi naelekeza lawama kwa tanroads na mamlaka zinazohusika na usalama barabarani; nchi nilizobahatika kutembelea ajali yoyote ikitokea uchunguzi wa kina hufanyika kujua nini kimesababisha na hadhari gani iwekwe kuzuia ajali nyingine isitokee kwa sababu ile ile. Hapo kwetu kila kukicha ni ajali. Zinatolewa sababu tu kuwa ni tairi, dereva, utelezi n.k. Lakini sijawahi kusikia uchunguzi umefanyika na kupelekea alieuza tairi amechunguzwa na kuchujuliwa hatua, au alama imewekwa kutahadharisha mahali penye utelezi n.k. Alama za barabarani kila kukicha zinapungua na hakuna hakuna mtu anaekumbuka kuweka zingine. Ugonjwa wetu mkubwa ni kila kitu kinaendeshwa kisiasa, hata katika mambo ya kitaalamu.