watu wahofiwa kufa kwenye ajali mtongani

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,495
3,458
kuna ajali imetokea mtoni mtongani pale kwenye mto mzinga darajani. roli lilokuwa limebeba korosho limepinduka. ni ajali mbaya sana ambayo umetokea kwenye mkusanyiko wa watu. Majirani wa pale baadala ya kuokoa watu wenyewe walikuwa wanagombania viroba vya korosho zilizobanguliwa huku wengine wakitafuna. Chanzo cha ajali hakijajulikana. Inaskitisha sana.
 
Pole yao hao waliokumbwa na accident eneo lile.The accident has befallen them at a very dangerous spot.
Yaani pale kwa waosha magari hapatabadilika ukipata accident au kuharibikiwa na gari majira ya usiku basi ujue hautoki na kitu wataiba kila kitu kinachochukulika kwa urahisi.
Jambo la kwanza kwenye accident zitokeazo eneo lile huwa ni kuwasachi majeruhi au waliokufa then baadae ndio watasaidiwa.
Lilishawahi kupinduka lori la bia pale watu walikunywa mpaka wakakaa na nyingine zikaenda kuuzwa kwa mabaa ya karibu.
Inasikitisha sana mtu anapopoteza hali ya ubinadamu kutokana kwa matumizi ya bangi na madawa ya kulevya na pia vijana wengi hawana ajira pale kwa hiyo wamejiajiri kwenye wizi.
 
Jamani Tusiwe Watu wakulalamika sana!! Pia Tuangalie Chanzo!! Ile barabara ni Very Poorly Constructed!! No design no any thing!! Hawa Wajapan Kweli waliamua Kutudharau!! Ila Mzee Magufuli alishasema watairudia Haraka Iwezekanavyo!! Ila Hadi sasa Naona Hii barabara inazidi Kusababisha Maafa!! Kwa nini Tusifanye Option B??...............
 
Pole kwa taifa zima kila kukicha nguvu kazi ya taifa inapotea inasikitisha sana.
 
Maeneo ya pale Mtongani kuna raia huwa ikitokea ajali kwao ni furaha, huwa wanaiba kila kinachowezekana kuibiwa hata kwa watu waliopoteza maisha. Hatari sana pale.
 
Pole zao wafiwa na hata MUNGU azilaze roho za marehemu mahala pema peponi!


Ameeeen!!
 
Mimi naelekeza lawama kwa tanroads na mamlaka zinazohusika na usalama barabarani; nchi nilizobahatika kutembelea ajali yoyote ikitokea uchunguzi wa kina hufanyika kujua nini kimesababisha na hadhari gani iwekwe kuzuia ajali nyingine isitokee kwa sababu ile ile. Hapo kwetu kila kukicha ni ajali. Zinatolewa sababu tu kuwa ni tairi, dereva, utelezi n.k. Lakini sijawahi kusikia uchunguzi umefanyika na kupelekea alieuza tairi amechunguzwa na kuchujuliwa hatua, au alama imewekwa kutahadharisha mahali penye utelezi n.k. Alama za barabarani kila kukicha zinapungua na hakuna hakuna mtu anaekumbuka kuweka zingine. Ugonjwa wetu mkubwa ni kila kitu kinaendeshwa kisiasa, hata katika mambo ya kitaalamu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom