Ajali mbaya eneo la Makongo: Watu 18 wahofiwa kupoteza maisha!

made

JF-Expert Member
Jun 29, 2010
890
581
Jamani nimeandika kwa haraka lakini kuna ajali mbaya sana hapa Makongo imeua watu kadhaa,imehusisha gari kama tano hivi,daladala mbili.

==============

WATU Sita wamekufa na wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa katika ajali iliyotokea barabara ya kuelekea Bagamoyo eneo la Makongo, jijini Dar es Salaam, baada ya gari la abiria ‘daladala' iliyokuwa inatokea Tegeta kuelekea Mwenge kuacha njia na kugongana na daladala nyingine iliyokuwa ikitokea Mwenge kuelea Kunduchi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni, Camillius Wambura, ameithibitishia FikraPevu kuwa tukio hilo limetokea Juni 21, 2014 saa Saba mchana na kuwa daladala iliyopata ajali inayofanya safari zake kati ya Tegeta Nyuki na Ubungo yenye namba T 441 CKT, imegongana na daladala nyingine inayofanya safari zake kati ya Makumbusho na Kunduchi yenye namba T 377 CKT mara baada ya kukosa mwelekeo.

Ajali-Makongo-1.jpg

10452334_757604927648421_7442749163729132767_n.jpg

attachment.php

Wambura, amesema ajali hiyo imehusisha magari matatu mara baada ya daladala hiyo kukosa mwelekeo, ambapo miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Lugalo na majeruhi wamelazwa hospitalini hapo wakiendelea na matibabu huku dereva wa daladala iliyosababisha ajali hiyo akiwa anatafutwa baada ya kukimbilia mafichoni baada ya kusababisha ajali hiyo.

Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Kamanda Awadhi Haji, amesema ajali hiyo imehusisha magari manne, moja likiwa ni la raia wa China, ambaye gari lake liliwakanyaga majeruhi na kuwaua sita kati yao.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Lugalo, ambapo maiti na majeruhi wamepelekwa Brigedia Jeneral, Josia Mekere, amethibitisha kupokea majeruhi 12, na maiti sita huku wengine hali zao zikiwa ni mbaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema ajali hiyo imetokea wakati dereva wa gari la abiria ‘daladala' lilokuwa likielekea Mwenge kutokea Tegeta, kuwa katika mwendo kasi na kushindwa kulimuda hali iliyopelekea gari hilo kuhama barabara na kuingia katika upande wa pili na kusababisha ajali hiyo.

- See more at: http://www.fikrapevu.com/watu-6-wam...ajali-ya-barabarani-dar/#sthash.cVZdckCA.dpuf
 
Watu 18 wamefia hapo na majeruhi zaid ya 20 wanahari mbaya,

Ajali hiyo imehusisha Dalala mbili ambazo ambayo ni mbaya sana saa hii 14:00 kamili
 
Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam imepata ajali mbaya leo mchana baada ya kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 18 katika eneo la Makongo Sekondari jijini Dar. Maiti bado zipo eneo la tukio, habari zaidi zitakujia hivi punde.!
 
Jamani nimeandika kwa haraka lakini kuna ajali mbaya sana hapa Makongo imeua watu kadhaa,imehusisha gari kama tano hivi,daladala mbili.
Umeandika haraka ili iweje? Ungetulia kwanza ili ulete taarifa kamili, acha kukurupuka. Lete picha. Chanzo cha ajali, baada ya hapo nini kimeendelea. Au ulitaka kuwa wa kwanza kuanzisha thread? Acheni hizo, kuna mwenzio naye kaleta kama hii.
 
ImageUploadedByJamiiForums1403351118.516385.jpg

Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam imepata ajali mbaya leo mchana baada ya kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 18 katika eneo la Makongo Sekondari jijini Dar. Maiti bado zipo eneo la tukio, habari zaidi zitakujia hivi punde.
Source;GlobalHabari
 
Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam imepata ajali mbaya leo mchana baada ya kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 18 katika eneo la Makongo Sekondari jijini Dar. Maiti bado zipo eneo la tukio, habari zaidi zitakujia hivi punde.!

Aisee...

Makongo pale ni double road. Ni kwamba gari moja limevuka barabara upande wa pili au gari moja limegonga jingine kwa nyuma? watu 18 kufa kwenye ajali ya daldala si mchezo, lazima ilikuwa kasi ya ajabu.

Mungu awarehemu marehemu, na awape uponyaji wa haraka majeruhi wote.
 
View attachment 166217

Gari aina ya Toyota Coaster inayofanya safari zake kati ya Ubungo na Tegeta jijini Dar es Salaam imepata ajali mbaya leo mchana baada ya kugongana na gari lingine na kusababisha vifo vya watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 18 katika eneo la Makongo Sekondari jijini Dar. Maiti bado zipo eneo la tukio, habari zaidi zitakujia hivi punde.
Source;GlobalHabari
Kuna wenzio pia wameleta taarifa hii nusunusu kule habari mchanganyiko.
 
Aisee...

Makongo pale ni double road. Ni kwamba gari moja limevuka barabara upande wa pili au gari moja limegonga jingine kwa nyuma? watu 18 kufa kwenye ajali ya daldala si mchezo, lazima ilikuwa kasi ya ajabu.

Mungu awarehemu marehemu, na awape uponyaji wa haraka majeruhi wote.

imegongwa kwa nyuma
 
Back
Top Bottom