Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Watu watano wamenusurika kufa wilayani Songea mkoani Ruvuma baada ya roli lililoegeshwa kuporomoka bila dereva na kugonga maduka na nguzo za umeme na kusababisha taharuki kubwa na kujeruhi watu wawili waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Ruvuma huku shughuli zikisimama na barabara ya Songea-Mbinga kulikotokea ajali ikifungwa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wanaelezea jinsi tukio lilivyotokea na namna roli hilo lililoporomka bila dereva na kuparamia maduka na kugonga nguzo za umeme mjini Songea na kujeruhi watu wawili na kugonga kwenye duka la vifaa vya umeme la Bw. Henry Tweve aliyekuwemo ndani ya duka hilo na watu wengine wawili ambapo pia limejeruhi watu wengine wawili kabla ya kugonga duka hilo.
Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo cha kuegesha maroli mjini wakatiu serikali ilipiga marufuku maroli kuegeshwa mjini na kuitaka serikali kusimamia sheria zake ilizojiwekea za kuhakikisha maroli hayaegeshwi mjini ili kuepesha ajali kama hizo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Bw. Zuberi Mwombeji alipopigiwa simu yake ya mkononi ilipokelewa na mlinzi wake aliyesema yuko msibani huku waathirika wa ajali hiyo wakieleza hasara walizozipata.
Chanzo: ITV