Mbagala, Dar: Polisi yawanyakua watu 27 Walioiba Saruji kwenye ajali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
KUKAMATWA WATU 27 KWA TUHUMA ZA KUIBA MIFUKO YA SARUJI BAADA YA AJALI YA MALORI MBAGALA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linawashikilia watu 27 kwa tuhuma za kuiba mifuko ya saruji baada ya ajali ya malori mawili eneo la Mbagala Mission.

Mnamo tarehe 04/10/2021 saa 04:30 asubuhi eneo la Mbagala Mission, Lori lenye namba za usajili T 164 DKC aina ya Horse na tela lake namba za usajili T 342 DJZ likiwa limebeba mifuko ya saruji lilipata ajali na kutumbukia kwenye mtaro kutokana na tairi kupasuka.
Baada ya ajali hiyo kutokea zaidi ya watu 50 walijitokeza na kuiba mifuko ya saruji.

Aidha, tarehe 05/10/2021 majira ya saa 06:40 usiku eneo la Mbagala Mission, Lori lingine lenye namba za usajili T 705 AUE lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 911 ATR likiendeshwa na MUHIDINI HUSSEIN (39),mkazi wa Morogoro, likitokea Mbagala kuelekea mjini likiwa limebeba zaidi ya mifuko 700 ya saruji nalo lilipata ajali.

Polisi walifika mapema eneo la tukio na kuwakuta watu 27, wakiwa wanaiba saruji kwa kuipakia kwenye Pikipiki na Bajaji. wote walikamatwa na jumla ya mifuko 368 iliokolewa ikiwemo 10 iliyokutwa kwenye nyumba za watu.

Watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Onyo;-
Jeshi la Polisi halitasita kushughulika kikamilifu kwa mujibu wa sheria na watu wote wenye tabia ya kukimbilia kwenye matukio ya ajali badala ya kuokoa watu na mali, wao wanageuka kuwa wahalifu/wezi.


MULIRO J. MULIRO
KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUM DAR ES SALAAM

Pia soma;

Thread 'Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji' Mbagala: Lori lililobeba saruji laanguka, Wananchi wajibebea mifuko ya saruji
 
Kuna mtu namjua ni mpigaji aliibiwaga mizigo
Yake sasa ilibd aingie front aende huko kutemesha,nlimsindikiza nlicheka sana
Mpigaji kpigwa😂😂😂
Tuliingia kijiji kimoja watu wote watu wa deal wezi

Ova
Haa Haa
Unamkuta Ustadh Na Sigida Lakini Mpigaji Mzuri
 
Back
Top Bottom