Watu wa Tanga ni noma

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
374,411
Reaction score
867,087
Achana na ushirikina
Achana na mapishi ya ukweli
Achana na matunda na mbogamboga
Achana na malovee na watoto wakali
Achana na slogan ya waja leo warudi leo
Achana na maneno kwamba Tanga kuna kibao cha karibu lakini hakuna kibao cha kwaheri
Salute kubwa kwa wakazi wa kicheba na Muheza kwa kuweza kumvuta tajiri namba moja ulimwenguni BILL GATES, ni mvuto wa ajabu wenye nguvu hasa! Kumbuka ndele za ukweli zinapatikana mitaa hiyo

Bongo bahati mbaya lakini sio TANGA currently speaking Muheza na Kicheba! Muheza yote mpaka kicheba bila kusahau Lusanga kwa marehemu Sharo milionea na magoroto kwenye uchawi kiboko na kijiji cha Mjimwema! Kijiji kisafi mpaka mtu anaogopa hata kutema mate lakini mpaka mazao shambani yamevikwa hirizi
Kicheba hiyo ya mganga Mariam (mashaulah mwanamke wa kibondei wewe) sijui hii ni kazi yako? Hongera mama nakuaminia.. Bila kumsahau babu Ukae njia ya kwenda Misozwe.,, hufiki kibaranga....
Muheza sio bahati mbaya sijui Bill kafikishwa msitu wa amani!? Bila kusahau mapango ya Amboni
Nimejiuliza tu kwanini isiwe Chattle! Jibu ni moja tuu... MVUTO kiroho safi kabisa...... [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Great sinking @ Work!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…