Wakuu nimefanya utafiti wangu nimegundua hapa Tanzania Jiji la pili kwa Ukubwa Tanzania halina sapoti ya serikali isipokua biashara na nguvu za wazawa ni Mwanza,wilaya tajiri na yenye pato kubwa kuliko wilaya zote Tanzania na haina promotion ya serikali ni Kahama.Nimegundua kitu kimoja,wasukuma si walalamishi na wakujisifu bali ni wapiga kazi balaa na waaminifu sana,mikoa yao ukitoa Dar ndio inayoongoza kwa kuchangia pato la Taifa.
Mwanza hakuna makao makuu ya Taasisi yoyote ya Serikali au Umma km Arusha,lakini Bado mwanza ni Kinara.Mwanza haina uwanja mkubwa wa ndege km Arusha na Kilimanjaro (KIA) na Arusha Airport lakini ndio jiji lenye route nyingi za ndege zaidi kuliko mikoa mingine ukitoa Dar.
Mwanza haina maukumbi makubwa ya serikali na binafsi km Arusha,haina mbuga za wanyama wala vivutio vingi vya watalii lakini bado ndio jiji la pili kwa ukubwa.
Siri ya Wasukuma ni wapiga kazi sana na siwalalamishi,hata ukimdhulum msukuma halalamiki,hana kesi na wewe ataondoka na kwenda kufanya kazi nyingine tu.Tatizo kubwa la hawa jamaa wanaoa sana,cha ajabu kila mtoto wa kila mke ni copy ya baba yao yaani wanafanana sana.Hii inamaanisha jamaa wa kule ni wacheza shoo wazuri sana hawatumii pweza wala viagra km wanaume wa kule kwa akina Scorpion.
Juzi nilikua Mwanza,nimezunguka sehem zote muhimu anayefananisha Mwanza na mikoa mingine atakua BAVICHA ama UVCCM ******!