Watu wa mabondeni tunateseka, msaada tafadhali

Watu wa mabondeni tunateseka, msaada tafadhali

Huko huko mnakoendaga wakati wa mafuriko ndo hamieni jumla
 
Nikusaidie mleta mada huku Tegeta vyumba vya elfu 20-25 vipo vingi mbona, au ndo unataka kukaa krb na posta .hameni
 
Afrika inaangamia kwa sababu ya waafrika kuendekeza ubishi wa kijinga!. Nyakati za mafuriko wanaoweza kujiokoa kwa kupanda juu ya dari ni vijana peke yao, wale wazee wenye kuhitaji msaada hawawezi kujiokoa. Serikali inaposema mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki zimesababisha vifo vya watu watano, ujue kwamba kinachosemwa ni vifo vya watu wengi zaidi ya idadi rasmi inayotajwa. Tusidanganyane na hali ya joto la Dar kwa sasa tukaanzisha hoja za kutetea uholela wa nyumba za mabondeni. Hatuna vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya uokoaji wa watu wakati wa mvua zenye madhara. Wale wanaosema kuwa hawana ndugu wa kuwasaidia, hicho sio kigezo cha kutaka kuleta usumbufu wakati wa masika. Sio kila kinachosemwa na serikali baso kipingwe tu, angalau hoja za msingi ziwepo.
Acha kuropoka,hakuna mtu anaekufa,sisi tunajua namna ya kujiokoa tunapopata mafuriko,
 
Last edited by a moderator:
Mafuriko yakiwashtukiza mtaililia serikali tena iwasaidie jamani nyie vipi???
Mmengangania kwenye kingo za mito kama mamba mnaboa
Acha uboya wewe.sisi hatuililii serikali
 
Mlitangulia mjini..Magufuli kawafuateni mjini hawaoni...kumbe hamuisgi mjini balu mabondeni.
 
Acha kuropoka,hakuna mtu anaekufa,sisi tunajua namna ya kujiokoa tunapopata mafuriko,
Kama mnajua namna ya kujiokoa msiwe mnaisumbua serikali wakati wa masika, miji inazo ramani tatizo mamlaka zetu zinanuka rushwa. Katika miaka ya 70 na 80 mabonde ya Dar hayakuwa na wakazi. Taratibu yalianza kuvamiwa na watu. Miundoi mbinu mingi ya uokoaji wa bara letu ni duni sana. Moto unaunguza jengo na watu wa fire wapo katika eneo la tukio lakini mabomba yao hayana uwezo wa kusukuma maji ya kuzimia moto!. Mnapendwa na serikali yenu ndio maana mnaondolewa kwa nguvu.
 
HAKUNA MSAADA TUNAWEZA KUWAPATIENI.KAMA SERIKALI TUKUFU HAITAKI MUWEKO HUKO MABONDENI HAMUNA BUDI KUHAMA NA TENA MURUDI MAKWENU VIJIJINI HARAKA.
 
Tatizo kama halijakupata wewe sio siri unachukulia poa,hata mwenzako ambae humjui ukiambiwa kafiwa na mama au baba yake au mtu wake wa karibu huwa huumii sana mana sio wewe,ila ngoja ufiwe wewe ndio utajua uchungu wake.imagine mtu huna pesa na miezi ya January ni ya majukumu afu unaambiwa unabomolewa,au fikiria nyumba yako inabomolewa ni namna gani utaumia
 
Ndio faida ya kupenda kukimbilia mijini.unalia lia uonewe huruma wakati kijijini kwenu kuna ardhi ya kutosha
 
Tatizo kama halijakupata wewe sio siri unachukulia poa,hata mwenzako ambae humjui ukiambiwa kafiwa na mama au baba yake au mtu wake wa karibu huwa huumii sana mana sio wewe,ila ngoja ufiwe wewe ndio utajua uchungu wake.imagine mtu huna pesa na miezi ya January ni ya majukumu afu unaambiwa unabomolewa,au fikiria nyumba yako inabomolewa ni namna gani utaumia
Pole lakini taarifa ya kuhama maeneo hayo si ipo toka 2012?
 
Acha kuropoka,hakuna mtu anaekufa,sisi tunajua namna ya kujiokoa tunapopata mafuriko,

Mwaka Juzi wewe ulikua kimbelembele kwenye kamera za BBC kulaumu serikali imewanyima msaada, kwa sasa hasikilizwi mtu tokeni huko madongo poromoka.
 
Wakati safari zanje na posho za watumishi zinaondolewa, hawa watumishi na familia zao imekua ni kilio, lakini hapo hapo wananchi haswa wa vipato vya chini walishangilia na kuwacheka watumishi, kwakifupi ni kwamba kila mwananchi kwa namna moja ama nyingine ataisoma namba na mwisho wa siku tatamkumbuka Mkwere tulie mdhihaki na kumsema vibaya
 
Tumechoka kusikia wahanga wa mafuriko,ondoken kazi zenyewe zinazowaweka mjini hamna,nyumba mlalamike,,sehem za biashara mkitozwa ushuru mnakimbia kimbia kukwepe ushuru kwa kisingizio mitaji yenu midogo.RUDINI VIJIJIN MJINI SHULE.
 

Attachments

  • IMG-20151208-WA0012.jpg
    IMG-20151208-WA0012.jpg
    41.6 KB · Views: 28
Acha uboya wewe.sisi hatuililii serikali


Ha ha haaaa!
Mie ninayekaa mahala pakueleweka nawewe mkaa bondeni mvua ikija wakimbia ikiisha warudi nani boya??

Na wawatoe tu!! tumechoka kuwaona kwenye tv mkipatwa mafuriko
 
Waungwana, leo naandika kichwa kikiwa kinaniuma sana na sina raha hadi nimepungua kwa sababu ya mawazo, hata vidonda vyangu vya tumbo vimeanza tena, yaani huyu Magufuli bora tusingemchagua kabisa. Kama ni namba tunaisoma kwa sana tu, hivi ingekuwa ni yeye hii hali jamani kweli angefurahia?

Leo hii tunaambiwa tarehe 5 mwisho wa kuishi kwenye nyumba zetu, hivi anajua adha na mateso tunayoyapata sie?? Leo hii mtu unaambiwa uhame na mahali pa kwenda huna, watoto wanahitaji ada, uniform, madaftari n,k na pesa huna hivi kweli ni haki?

Kuna wengine wamezoea kuishi nyumba za mabondeni, sio kwamba wanapenda kupanga huku bali kipato chao hakiruhusu kuishi ma kupanga sehemu nzuri, asilimia kubwa ya wapangaji wa nyumba za mabondeni ni makapuku wa kutupwa, yaani huku vyumba ni elfu 20 hadi 25, kwa hiyo mtu nikiwa na laki na nusu naishi miezi sita, laki tatu naenjoy mwaka mzima, sasa leo hii vyumba vinabomolewa tutaishi wapi sie tuliozea kupanga nyumba za bei nafuu? Hivi hii serikali inamuangalia mtu wa hali ya chini kweli?

Yani leo tar 2 na 5 ni mwisho nawaza hadi nashindwa ntaishije na hawa watoto wawili jaman. Wenye nyumba wao mnadai wamepewa viwanja, je vipi kuhusu sisi wapangaji ambao tumezoea nyumba za bei chee kutokana na kipato chetu kidogo? Safari hii tutaumwa wengi sana kwa sababu ya serikali ya Magufuli lakini pia Magufuli sie hatukukuchagua ili ubomoe nyumba zetu bali tulihitaji utuboreshee maisha yetu na je ni kweli huyu Rais hajaona kitu kikubwa cha kuanza nacho hadi aje abomoe nyumba zetu wajamaneni??

Mimi huu mwaka wa 3 naishi bondeni na sijawahi kuona maji yameua kabisa, maana sie ikija mvua huwa tunahama na ikiisha tunarudi, maji yakijaa huwa tuanayapisha na mvua ikikata huwa tunarudi kusafisha vyumba vyetu na kuishi, bora ya Kikwete kuliko Magufuli
Wenzako wanagawana Shamba la Mr zero wewe umekomalia mabondeni kutafuta nini.

Mimi hapa naelekea Tanga kwenda .kugawana Shamba la EDo
 
Ubomoaji ni sahihi tatizo ni ukosefu wa busara kwa viongozi wa sasa. Hili zoezi lingeenda kiutaratibu kwa kubomoa kotekote yaani wananchi wenye nyumba na maafisa waliohusika na kuruhusu ujenzi holela. Suala la kumkumkumbuka Mkwere halina mjadala.
 
Back
Top Bottom