Watu wa mabondeni tunateseka, msaada tafadhali

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Waungwana, leo naandika kichwa kikiwa kinaniuma sana na sina raha hadi nimepungua kwa sababu ya mawazo, hata vidonda vyangu vya tumbo vimeanza tena, yaani huyu Magufuli bora tusingemchagua kabisa. Kama ni namba tunaisoma kwa sana tu, hivi ingekuwa ni yeye hii hali jamani kweli angefurahia?

Leo hii tunaambiwa tarehe 5 mwisho wa kuishi kwenye nyumba zetu, hivi anajua adha na mateso tunayoyapata sie?? Leo hii mtu unaambiwa uhame na mahali pa kwenda huna, watoto wanahitaji ada, uniform, madaftari n,k na pesa huna hivi kweli ni haki?

Kuna wengine wamezoea kuishi nyumba za mabondeni, sio kwamba wanapenda kupanga huku bali kipato chao hakiruhusu kuishi ma kupanga sehemu nzuri, asilimia kubwa ya wapangaji wa nyumba za mabondeni ni makapuku wa kutupwa, yaani huku vyumba ni elfu 20 hadi 25, kwa hiyo mtu nikiwa na laki na nusu naishi miezi sita, laki tatu naenjoy mwaka mzima, sasa leo hii vyumba vinabomolewa tutaishi wapi sie tuliozea kupanga nyumba za bei nafuu? Hivi hii serikali inamuangalia mtu wa hali ya chini kweli?

Yani leo tar 2 na 5 ni mwisho nawaza hadi nashindwa ntaishije na hawa watoto wawili jaman. Wenye nyumba wao mnadai wamepewa viwanja, je vipi kuhusu sisi wapangaji ambao tumezoea nyumba za bei chee kutokana na kipato chetu kidogo? Safari hii tutaumwa wengi sana kwa sababu ya serikali ya Magufuli lakini pia Magufuli sie hatukukuchagua ili ubomoe nyumba zetu bali tulihitaji utuboreshee maisha yetu na je ni kweli huyu Rais hajaona kitu kikubwa cha kuanza nacho hadi aje abomoe nyumba zetu wajamaneni??

Mimi huu mwaka wa 3 naishi bondeni na sijawahi kuona maji yameua kabisa, maana sie ikija mvua huwa tunahama na ikiisha tunarudi, maji yakijaa huwa tuanayapisha na mvua ikikata huwa tunarudi kusafisha vyumba vyetu na kuishi, bora ya Kikwete kuliko Magufuli
 
tatizo ni kupenda vya bure, chee na bidhaa feki!, shauri yenu mkikoswa na wabomoaji wa tar5, inakuja TBS
 
Nilipita Kinondoni wakati tingatinga linapita, ni huruma sana. Nadhani Serikali ingewapa muda baada ya kutoa agizo hasa ikiingatiwa January ni mwezi wenye majukumu mengi kwa watu wengi...
 
Mvua ikija unahama.unapohamiaga ndo ukapange huko.PAMBANA NA HALI YAKO CHALII ANGU
 
Kukitokea mafuriko nyie ndiyo watu wa kwanza kuomba msaada,sijui jema kwenu ni lipi.Hameni mnachafua mji sana
 
Hakuna namna.ONDOKENI.mafuriko yakija mnailaumu serikali haiwasaidii.Ondokeni banaa kwanini tunasumbuwana?
 
kama huko mjni mnaishi kwa tabu tena mabonden, kwa nn msirud huku kijjn mje 2lime?, yaan mliondoka 2kiwapgia simu mnasema mko mjini kumbe mko mabonden? ona sasa mmekaliwa koon na MAGU, nawaomben mrud kijjn hata huku pia maisha yapo jaman
 
Usijali mtafikiliwa na histoshe wezio wameshahenda kwa mufti mkuu na kwa kadinali pengo wameambiwa wasubili wataongea na mweshimiwa jumaa tatu
 
Pole braza. ..tatizo likija akili ndo inawaza vizur. UTAHAMA TU NA WATOTO WATAENDA SHULE AT THE END. usituchoshe fata sheria za nchi
 
Huku kituo cha simu2000 kuna mto unapita kutokea Kimara unakatiza Ubungo darajani unateremka kupitia usawa wa kilipo hicho kituo tajwa hapo juu,unakatiza Shekilango unaendelea unakatiza karibu na shule ya mama Salma nk nk..Mwezi wa nne kopindi cha mvua kubwa kulijaa mafuriko kwenye nyumba karibu na mkondo wa huu mto,ilikuwa ni balaa!kuna nyumba kama 3 hizi msingi umekula sehemu ya mto wenyewe so mvua ikinyesha kubwa tu maji yanahama yanapitia nyumba za jirani na kusababisha mafuriko.Wapangaji wa hizi nyuma hukimbia na kuacha kodi kila mafuriko yakitokea ila mmaji yakiisha wanaingiza wapangaji wapya!Hili ni jipu Mh Magu tunaomba vijana wako wapite na huku waisome namba!
 
Mafuriko yakiwashtukiza mtaililia serikali tena iwasaidie jamani nyie vipi???
Mmengangania kwenye kingo za mito kama mamba mnaboa
 
Afrika inaangamia kwa sababu ya waafrika kuendekeza ubishi wa kijinga!. Nyakati za mafuriko wanaoweza kujiokoa kwa kupanda juu ya dari ni vijana peke yao, wale wazee wenye kuhitaji msaada hawawezi kujiokoa. Serikali inaposema mvua zilizonyesha mwishoni mwa wiki zimesababisha vifo vya watu watano, ujue kwamba kinachosemwa ni vifo vya watu wengi zaidi ya idadi rasmi inayotajwa. Tusidanganyane na hali ya joto la Dar kwa sasa tukaanzisha hoja za kutetea uholela wa nyumba za mabondeni. Hatuna vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya uokoaji wa watu wakati wa mvua zenye madhara. Wale wanaosema kuwa hawana ndugu wa kuwasaidia, hicho sio kigezo cha kutaka kuleta usumbufu wakati wa masika. Sio kila kinachosemwa na serikali baso kipingwe tu, angalau hoja za msingi ziwepo.
 
Back
Top Bottom