watu wa Dar na zawadi za mikate.

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,657
20,940
watu wa Dar kwanini mnapenda kubeba zawadi ya mikate mkienda mikoani? nilijua siku hizi mmeacha lakini kumbe mnaendelea. wote mnabeba mikate utafikiri mmeambizana. mbaya zaidi ikifika na nyie mnakula hiyohiyo! kwanini mnapenda hiyo zawadi?
 
Duuu mikate nazani ndo kitu kinacho patikana kiuraisi maeneo ya dar na huku mikoani mahindi na bata ndo vinapatikana kiuraisi kwa hiyo kila mtu hubeba kile kilichopo katika eneo lake
 
Mikate inatosha sasa,siku nyingine mkija huku kijijini pitieni hapo ofisini kwa Mbowe mtuletee Unga huku kwetu njaa imezidi.
 
Watu wa mikoani mnataka tuwaletee nn sasa?!
pweza tunawasikia tu kwenye mitandao ya kijamii. tuleteeni hao(tuwaonje tu si kwaajili ya matumizi kama yenu). mikate hata huku ipo. leteni hata vibua, sijui jodari au dagaa mchele.

mnaongoza kwa kuleta zawadi mbaya. watu wa Mwanza huleta sato, Mbeya mchele na maparachichi hata Zanzibar huleta mashokishoki. kwanini mnabeba kitu ambacho kipo uendako?:):)
 
Back
Top Bottom