Watu pekee ambao huwa nasikiliza hotuba zao kwaajili ya kujifunza maneno ya hekima yenye kuleta furaha na amani

Watu pekee ambao huwa nasikiliza hotuba zao kwaajili ya kujifunza maneno ya hekima yenye kuleta furaha na amani.

Siku zote watu wanasema ukitaka kuwa na hekima jifunze kutoka kwa wenye hekima.
Wasikilize watu wenye hekima.
Hata ukipata nafasi basi ongea na kuzungumza na watu wenye hekima.

Hii ndio orodha ya watu wangu pekee ambao huwa najifunza kutoka kwao, ili nipate maneno yenye hekima.

1.Obama
2. Steve Jobs
3. Bill Gates
4. Dkt. Magufuli
5. Watu waliosomea Havard University.

Ukifuatilia hotuba za Obama, alikua anazungumzia maneno yenye hekima sana na ya kujenga na sio kubomoa. Si hivyo tu alikuwa kila akihutubia pia lazima aingizie maneno machache ya kuchekesha. Lazima ujue kuchekesha unapo hutubia hiyo ni mbinu ya uhutubiaji kama unaongea ongea tu bila kuchekesha wewe sio mhutubiaji bali nimwongeaji.

Ukimusikiliza Dkt Magufuli hotuba zake zinafanana sana na hotuba za Obama. Hakika ukimsikiliza lazima upate maneno ya hekima na ya kuchekesha yenye kuleta amani na furaha moyoni.

Ukifuatilia hotuba za Steve Jobs naye hivyo hivyo. Lazima achekeshe kidogo.

Natamani sana na mimi niwe kama Dkt Magufuli, kama Obama wa Tanzania, kama Steve Job kama wale vijana wa Harvad. Nihutubie watanzania maneno yenye hekima yenye kuleta amani na furaha na kabla sijamaliza hotuba yangu niingizie kidogo na maneno ya kuchekesha.

Siasa sio vita bali ni mchezo tu kama basket ball.

View attachment 1588928

View attachment 1588930

View attachment 1588931

Wewe hauko sawa kichwa. Huyu magufuli aliyejaa roho mbaya, mshenzi na hasiyekuwa na hekima hata moja unamfananisha na Obama kweli???

Huyu huyu ambaye anasema " Sileti maendeleo kwasababu munachagua chama tofaiti na ccm"
 
Wewe hauko sawa kichwa. Huyu magufuli aliyejaa roho mbaya, mshenzi na hasiyekuwa na hekima hata moja unamfananisha na Obama kweli???

Huyu huyu ambaye anasema " Sileti maendeleo kwasababu munachagua chama tofaiti na ccm"
ndiyoo
 
Wewe hauko sawa kichwa. Huyu magufuli aliyejaa roho mbaya, mshenzi na hasiyekuwa na hekima hata moja unamfananisha na Obama kweli???

Huyu huyu ambaye anasema " Sileti maendeleo kwasababu munachagua chama tofaiti na ccm"
Hata unitukane Magufuli for life, ww utakua uliwahi kuwa fisadi
 
Proffesor Patrick Lochi Otieno Lumumba.. hutajuta kumsikiliza, japo kuna wakati ana vocabularies ngumu,.. amewahi kutoa speech udsm watu wanaiita "the magulification of Africa". . unaweza kuichek youtube pia
 
Mmmmh nina wasiwasi kidogo na Mh Magufuli, Magufuli kabla hajahutubia, hotuba yake unaweza kuitabiri kwa 80% yaani ukajua kile anachoenda kuongea kwa asilimia kubwa kabla hajaanza kuongea. Huu ndo ukweli wa moyo wangu juu ya hotuba za mheshimiwa Rais Magufuli. Kwa upande wangu anakuwa ameshakosa sifa za kuwa na hotuba nzuri.
 
Sasa katika watu siwasikilizagi na naona ni mzigo nchi hii ni huyo mgombea,huyu huwa ni muigizaji na mkurupukaji na hajuagi njia ya kutatua jambo
 
Back
Top Bottom