Festo Sanga: Watu Milioni 3 ndio wanaolipa kodi kati ya Milioni 30+ wanaostahili kulipa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,971
12,291
CASHLESS ECONOMY-DIGITAL ECONOMY (Uchumi wa Kidijitali, matumizi ya fedha kielectroniki kwenye shughuli za kiuchumi).

Leo (16/05/2024) nimesimama Bungeni kuomba ufafanuzi kwa serikali, Katika Dunia ya sasa, uchumi umehamia kwenye mifumo (elekroniki) iwe kununua au kulipa au kupata huduma yoyote ile.
Cashless Economy imekuwa mwarobaini kwa kiwango kikubwa kwenye kupambana na kupunguza ;
-Rushwa
-Matukio ya Ukabaji na yanayovutia kuiba
-Ukwepaji kodi n.k

Cashless Economy, imesaidia kwenye.
-Mudhibiti mienendo ya matumizi ya fedha haramu.
-Kumarisha ukusanyaji wa mapato.
-Uwazi kwenye matumizi ya fedha
-Uwajibikaji kwenye matumizi ya fedha.
-Zaidi imerahisisha huduma za kulipa, kununua na kupata huduma kwa wakati.

Ulimwengu umehamia huko, kitendo cha kutumia keshi kwenye manunuzi,malipo n.k kimekuwa ni uchochoro wa wizi, rushwa na upotevu wa mapato.

Hoja yangu kwa serikali imekuwa ni nini mkakati wa kuondoakana na matumizi ya keshi (fedha taslimu) kwenye uchumi wetu kama mkakati wa kuongeza wigo wa kukusanya mapato nchini?.

Naipongeza sana Wizara na majibu ya Mh @napennauye kwamba,
-Jambo hilo linawezekana kwa watanzania wote kuachana na natumizi ya keshi.
-Jambo hilo litawezekana kwa kuhakikisha upatikanaji wa mtandao ni wa uhakika nchini kote na maeneo yote.
-Uimarishaji wa mifumo ya kiusalama ya fedha kwenye mifumo, ili kujenga imani ya watu kuweka fedha huko.
-Kuweka namna mtu aone kupata huduma kwa keshi ni gharama zaidi kuliko kupata huduma kwa keshilesi (mtandaoni).

INAWEZEKANA, wenzetu wameweza, na sisi tunaweza. Taifa lolote linajengwa kwa kupata makusanyo yakutosha ya fedha na udhibiti wa mianya ya upotevu wa mapato na rushwa.

By.
Festo Sanga
 
Sawa

Wakinga ni jiwe lililokataliwa sasa limekuwa jiwe Kuu la pembeni

Ndio wanaendesha uchumi kwa sasa wakifuatiwa na Wapemba 😂😂🔥

Kwako Bilionea Sugu 🤣
 
Wakulima mnawatesa mpo humo kuudanganya umma…
WAZIRI WA KILIMO - WAKENYA WANAWADHULUMU WAKULIMA WA MAPARACHICHI NJOMBE MAFINGA MAKAMBAKO UPO BUNGENI UNASHINDWA KUTOA MUONGOZO
MKULIMA AUZE KILO MOJA YA PARACHICHI SHILLINGI 800 Hii imekaa sawa kweli?
Mods tafadhalini msifute hii
Wakulima wanateseka sana
Parachichi zinaozea shambani wakulima wamegoma kuuza
Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume Martin Maranja Masese
 
Wakulima mnawatesa mpo humo kuudanganya umma…
WAZIRI WA KILIMO - WAKENYA WANAWADHULUMU WAKULIMA WA MAPARACHICHI NJOMBE MAFINGA MAKAMBAKO UPO BUNGENI UNASHINDWA KUTOA MUONGOZO
MKULIMA AUZE KILO MOJA YA PARACHICHI SHILLINGI 800 Hii imekaa sawa kweli?
Mods tafadhalini msifute hii
Wakulima wanateseka sana
Parachichi zinaozea shambani wakulima wamegoma kuuza
Mshana Jr Bujibuji Simba Nyamaume Martin Maranja Masese
Adui namba moja wa Mtanzania ni CCM na viongozi wake
 
Back
Top Bottom