Watu jamii ya Lissu wako wengi mjini

Watu jamii ya Lissu wako wengi mjini

Juzi nimeona clip ya Lissu akiwa Kariakoo akinunua maparachichi pilipili hoho na nyanyachungu, nikajiuliza hivi kweli mtu unatoka Kimara kwenda Kariakoo kununua parachichi na nyanyachungu? Huko Kimara hakuna soko? Hakuna genge? Nikajiuliza inawezekana akina Lissu wako wengi mjini wanatoka Chanika, Mbagala, Kimara Mbweni kwenda Kariakoo kununua nyanyachungu ndio maana daladala zinasomba watu tangu saa tisa usiku hadi saa saba usiku. Wapo wanaopeleka biashara na wapo wanaoenda kununua.

Je, sababu za mtu kutoka huko na kwenda Kariakoo ni nini? Kariakoo bei nafuu? au Kariakoo kuna uhakika wa kupata bidhaa za kila aina? au parachichi la Kariakoo liko fresh halijakaa muda mrefu kwenye tenga? au nitabia tu kuwa ukitaka kuhemea lazima uende Kariakoo? Na tukijenga masoko yenye hadhi ya Kariakoo, Mbagala, Kimara na Pugu kajiungeni watu watazidi kwenda Kariakoo?

Tukumbuke idadi ya watu mijini inaongezeka kila siku na hatuwezi kwenda kuhemea Kariakoo miaka yote.
Kama hukuelewa alienda kufanya nini Kariakoo basi hicho kichwa kakikusaidii zaidi ya kubeba meno ya kula.
 
2015 Lowassa nae alipanda daladala kabisa,ni vituko tu vya wanasiasa katika kipindi cha kampeni.
Kumbuka Lisu ni mpinzani Wa kweli na anachukua kura za kutosha,Lowassa tuliokota garasa,ingawa nae alimshinda magu matokeo yakageuzwa.tumejifunza kutokana na makosa.
Kipindi cha Lowassa magu alikuwa anapiga push up.
Kipindi hiki anapiga magoti,kakutana na mwamba anampeleka kikamanda.
 
Bila kusahau aliyepiga push up awamu hii anapiga magoti [emoji1787][emoji1787] nimekumbuka adhabu za shule enzi zile.
Dunia nzima hiki ni kituko cha aina yake toka kwa mgombea urais.
Amiri jeshi mkuu (Commander in Chief) kuonekana umepiga magoti kizembe ni dalili mbaya na ya kinyonge sana. Hata askari wako wanakudharau.
IMG_20201001_031244.jpg
 
Kumbuka Lisu ni mpinzani Wa kweli na anachukua kura za kutosha,Lowassa tuliokota garasa,ingawa nae alimshinda magu matokeo yakageuzwa.tumejifunza kutokana na makosa.
Kipindi cha Lowassa magu alikuwa anapiga push up.
Kipindi hiki anapiga magoti,kakutana na mwamba anampeleka kikamanda.
Hoja yangu hao wote ni wanasiasa na huu ndio wakati wao wa kufanya vituko,hiki kipindi kikiisha hutoona tena mambo kama hayo.
 
Kariakoo vitu vinauzwa Bei rahisi

Hata hao wafanyabiashara wa kimara wanavitoa kariakoo

Case closed
Wafanyabiahara wananunua jumla utalinganisha na Lissu anayeenda nunua fungu mbili za nyanya na hoho? mafuta ya gari kachoma shilingi ngapi? utumie mafuta ya gari elfu 20 ukanunue vitu vya elfu tatu? Lissu ana matatizo
 
wafanyabiahara wananunua jumla utalinganisha na LIsu anayeenda nunua fungu mbili za nyanya na hoho? mafuta ya gari kachoma shilingi nngapi? utumie mafuta ya gari elfu 20 ukanunue vitu vya elfu tatu? Lisu ana matatizo
Huyu jamaa katumia V8 tatu na walinzi cameraman na crue nzima ya CDM kwenda kununua wine, tena kanunua chupa moja ya st Anne, akili au matope? Halafu ndio awe Rais? Hapana
 
Huyu jamaa katumia V8 tatu na walinzi cameraman na crue nzima ya cdm kwenda kununua wine, tena kanunua chupa moja ya st Anne, akili au matope? Halafu ndio awe Rais? Hapana
Huyu yeye alienda na passo sio?
Screenshot_2020-09-29-15-08-54-1.jpg
 
Kwa mwanasiasa anayeyegombea nafasi ya kitaifa ni vizuri ku-interact na watu wote na siyo majirani tu..!! Matarajio ni kuongoza taifa na siyo majirani. Huo ushauri ungemfaa kiongozi wa mtaa. Mpaka hapo hoja yako inabaki kuhesabika kuwa ni hoja ya mtu mwenye akili ya bata[emoji1787]
Anafake maisha tu
 
Back
Top Bottom