Juzi nimeona clip ya Lissu akiwa Kariakoo akinunua maparachichi pilipili hoho na nyanyachungu, nikajiuliza hivi kweli mtu unatoka Kimara kwenda Kariakoo kununua parachichi na nyanyachungu? Huko Kimara hakuna soko? Hakuna genge? Nikajiuliza inawezekana akina Lissu wako wengi mjini wanatoka Chanika, Mbagala, Kimara Mbweni kwenda Kariakoo kununua nyanyachungu ndio maana daladala zinasomba watu tangu saa tisa usiku hadi saa saba usiku. Wapo wanaopeleka biashara na wapo wanaoenda kununua.
Je, sababu za mtu kutoka huko na kwenda Kariakoo ni nini? Kariakoo bei nafuu? au Kariakoo kuna uhakika wa kupata bidhaa za kila aina? au parachichi la Kariakoo liko fresh halijakaa muda mrefu kwenye tenga? au nitabia tu kuwa ukitaka kuhemea lazima uende Kariakoo? Na tukijenga masoko yenye hadhi ya Kariakoo, Mbagala, Kimara na Pugu kajiungeni watu watazidi kwenda Kariakoo?
Tukumbuke idadi ya watu mijini inaongezeka kila siku na hatuwezi kwenda kuhemea Kariakoo miaka yote.