Watu Hupata Wapenzi Wanaowastahili

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Ule msemo wa 'people get the president they deserve' (watu hupata rais aliye stahili yao) una ujumbe muhimu katika MMU. Kama una mpenzi ujue yeye ndiye stahili yako. Hivyo, acha kudai eti oh huna bahati ya kuwa na mtu mzuri maishani. Hukulazimishwa kuwa naye. Na hulazimishwi kuendelea kuwa naye tu. Daima uamuzi ni wako. Tulia. Tafakari. Chukua hatua. Usihofu. Fanya maamuzi magumu. Ndio. Leo leo. Usisubiri kesho maana kesho haiji.
 
Compa are you in L.O.V.E ??? Umempata anayestahili eeh!

Upande wangu, nimempata mwenyewe..tunastahiliana:))
 
Ule msemo wa 'people get the president they deserve' (watu hupata rais aliye stahili yao) una ujumbe muhimu katika MMU. Kama una mpenzi ujue yeye ndiye stahili yako. Hivyo, acha kudai eti oh huna bahati ya kuwa na mtu mzuri maishani. Hukulazimishwa kuwa naye. Na hulazimishwi kuendelea kuwa naye tu. Daima uamuzi ni wako. Tulia. Tafakari. Chukua hatua. Usihofu. Fanya maamuzi magumu. Ndio. Leo leo. Usisubiri kesho maana kesho haiji.

Whaaaat?
Haiwezi kutokea kinyume chake?
 
Not always. . .
Unalosema lingekuwa kweli tu iwapo kila mtu angekua anamjua mwenzie kwa kila namna kabla ya kumkubalia/kumuomba mahusiano.
 
Not always. . .
Unalosema lingekuwa kweli tu iwapo kila mtu angekua anamjua mwenzie kwa kila namna kabla ya kumkubalia/kumuomba mahusiano.

hapo neno 'hupata' linamaanisha watu 'wapo' na wapenzi wanaowastahili hivyo wavumilie tu kama vipi watimue...in any case, as always, exception is not the rule...
 
Umenena vema, 'otherwise watimue'
Jana nimeskia radio clouds, 'ndoa haibadili tabia ya mtu, inabadili marital status tu!'
Wengi wetu tunaingia kwenye mahusiano kwa kutegemea mwenzangu tukioana atabadilika. Don't hang around for much longer, ujikubalishe hali iliyopo ama uchukue ndogo ndogo.

Swali la kukatisha tamaa: do people tend to attract the same kind of trouble?
 
mie ananikera wakati mwengine lakini bado nampenda vile vituko vyake ananichekesha mpaka basi,na sio mume tuu kwangu nirafiki vile vile nampenda kwa mengi mtoto wa ki znz inshallah mungu aniwekee tuzikane.
 
Bahati mbaya sana watu wanabadirika; yaani hawako static. Anaweza kuwa leo ni poa kwako, ila miaka kumi mbele ya safari akawa si stahili tena; yaani kabadirika mbaya. Ndo maana ndoa zinavunjika. Ni vizuri uwe tayari kutafsiri hali halisi na kuamua cha kufanya.
 
Not always. . .
Unalosema lingekuwa kweli tu iwapo kila mtu angekua anamjua mwenzie kwa kila namna kabla ya kumkubalia/kumuomba mahusiano.
Lizzy, huwezi kumjua mtu 100%, true that. Ila kuna mtu anaanzisha mapenzi na mwenzie wakati hata hawajafahamiana vya kutosha, halafu wanalalamika kua mpenzi wangu hayupo nilivo tarajia. Imagine watu wanakutana facebook na kuanzisha mapenzi hata kabla ya kuonana. Hapo akikuta mtu ni mbovu, si atakua amejitafutia? na atakua amestahili chochote kitakacho tokea?
 
Last edited by a moderator:

Ndo hapo sasa. . .
Au unamkubali mtu ukiwa unajua fika ni mnywaji ilaa baadae unaanza kulalamika kuhusu trip zake za bar.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom