Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,413
WATU HUJA NA KUONDOKA, UTABAKI WEWE NA FAMILIA YAKO. HATA MTI HUCHIPUSHA nà KUPUKUTIAHA MAJANI. USING'ANG'ANIE WATU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Moja ya kosa ambalo utalifanya ni kutokutambua kuwa watu ulionao sasa hivi wapo lakini hautakuwa nao siku zote. Watu huja na kuondoka.
Kanuni hii ni universal Law, Ni kanuni ya Asili. Huwezi kuizuia. Ipo hivyo hivyo.
Kanuni za asili ndio Katiba ya viumbe. Ndio muongozo wa watu wote wenye Akili, malengo na wenye kutaka kujenga Future Bora Kwa vizazi vyao.
1. Kamwe usijefanya jambo lolote kujiumiza Kwa sababu ya watu ambao wanakuja na kuondoka. Kamwe!
2. Kamwe usifanye mambo kuwafurahisha watu ikiwa hayana maslahi kwako na familia Yako.
3. Mkeo/mumeo na watoto usiwaweke kwenye kimoja na watu watakaokuja na kuondoka.
Hiyo ni familia Yako. Hao ndio utakaokuwa nao nyakati nyingi kama sio zote.
4. Usifanye makubaliano na mtu back alafu maslahi aanze kupata yeye Kisha wewe baadaye. Nope! Hilo ni kosa kiufundi ambalo nature haitakusamehe.
Makubaliano lazima uyaweke yawanufaishe wote Kwa wakati husika.
Usipange Future yenye maslahi ya watu back. Mfano, Mtu anataka kukuajiri anakuambia nitakulipa mshahara huu(mdogo) vumilia alafu kampuni ikikua nitakuongezea mshahara. Kamwe usikubali hilo Dili hasa kama hujaridhika na haikutoshi. Watibeli hatufanyi hivi.
5. Usibetie Kwa watu wasiowako.
Watu huja na kuondoka.
Usijewekeza ukibeti Kwa mtu asiyewako.
Mfano Kusomesha Mchumba, nope!
Somesha mkeo ambaye Tena unawatoto naye. Hapo wekeza. Huyo ni mwenzako Hana ujanja. Uwekezaji usipoufaidi wewe utamnufaisha mwanao.
Usimlinganishe mtoto wako na mtoto wa kambo. Usibeti kwa mtoto wa jambo. Huyo huja na kuondoka. Sio wako.
Usiwe kama wale watu wajinga ambao hawajui Dunia ikoje. Nature haitambui Msaada unaoutoa Kwa watu wasiokuhusu. Nature haitambui kitu kama hicho.
Labda ufanye Biashara. Hapo sawa.
Watu huja na kuondoka.
6. Trust no one lakini Kwa vile mwanadamu hawezi kukaa kila kuamini. Basi chagua kuamini katika Familia Yako.
Muamini Mkeo/mumeo. Kmaa huyo utamhofia, mwamini mzazi wako, kama naye utamhofia, mwamini mtoto wako.
Lakini kwenye kuamini kwako jipe 70 hao wengine 30.
7. Mwanamke au Mwanaume uliyewahi kuishi naye na kuzaa naye watoto, ukakaa naye zaidi ya miaka kuanzia Saba. Huyo ni sehemu ya familia yako hata ikitokea mumeachana.
Ni Bora umuamini huyo kuliko Mwanamke au Mwanaume utakayekutana naye barabarani.
8. Kamwe Rafiki hawezi kuchukua sehemu ya mzazi, Mke/mume au watoto wako.
Ila mzazi, Mke/mumr au watoto wanaweza kuchukua nafasi ya rafiki Yako. Hivyo kuwa mwenye hekima.
Mzazi, Mke/mume na watoto mpo Connected.
9. Kila mtu huja Kwa sababu maalumu lakini si yakudumu. Lakini familia yako ipo kwaajili ya kudumu.
Mkeo/mumeo hata muachane kwa namna yoyote Ile. Ndio huyo huyo ambaye usipokuwepo Watoto wako au wajukuu zao wanaweza kuishi kwao na wanauhalali wa kuishi kwao. Na kule watoto wako wakawaita ndugu Kwa sababu wapo Connected na aidha Mama yao au Baba Yao.
Hivyo sio hekima kumdharau Mke au mumeo, au Baba au Mama au Mama mkwe, au Baba mkwe. Mpo Connected. Na ninaposema connected namaanisha wewe, watoto wako au wajukuu zako ni sehemu yako, wametoka kwako.
Hii ni kumaanisha, Watu huja na kuondoka lakini wapo watu ambao upo connected nao ambao wao sio Majani yanayopuputika wakati wa kiangazi. Wanaweza wasiwe active lakini haimaanishi hawapo kwaajili Yako. Hata kwenye mwili wako kuna viungo vipo passive lakini haimaanishi havina kazi au havitakuwa na umuhimu baadaye.
Ushaambiwa Ndugu wakigombana shika jembe ukalime Kwa sababu wewe ni mtu Back kwao. Wewe unakuja kwao na utaondoka utawaacha. Na watapatana tuu kwa sababu wao wapo connected.
Ni kosa kubwa utalifanya kupukutisha Majani yasiyosahihi.
Kuna matajiri au viongozi wakubwa au watu wenye akili hujua kanuni hii. Wanapokuwa na marafiki walioshibana sana. Huamua kuruhusu watoto wao waoane na kuunganisha undugu.
Taikon Master labda ninarafiki yangu aitwaye Evelyn Salt na hatutaki siku Moja tuwe mbali, basi mtoto wangu anamuoa/kuolewa na mtoto wa Evelyn Salt na hapo sio tuu tunakuwa marafiki bali tunaunganishwa tunakuwa Ndugu. Na jina La Family Friend linakuwa na nguvu sana.
Kwa taifa la Tanzania ni ngumu kupambana na Dola kwa Sababu wengi wa watawala wameunganisha unganisha undugu. Na hiyo kufanya wasiwe watu wakuja na kuondoka.
Hii ni kusema, hawawezi kusikiliza wewe mtu wa barabarani ambaye hawakujui, na hata kama wanakujua lakini wanajua ni mtu back wakuja na kuondoka na kuacha kusikiliza familia zao.
Kwa Watawala na wafanyabiashara wakubwa, mtoto anapoenda Kuoa au kuolewa ni kama dirisha la usajili la wachezaji wapya limefunguliwa. Hivyo wanazingatia Quality ya anayesajiliwa kwa mustakabali wa familia zao.
Unapowaza Mafanikio Yako, huwezi kuacha kuwaza kuhusu Familia Yako, yaani Mume/Mke na watoto.
Huwezi tenganisha Mafanikio Yako na Familia. Labda kama huna akili sawasawa.
Sustainable development Yako huwezi kuepuka familia.
Mke Bora, mume Bora ambao watazaa na kulea watoto Bora kufuata malengo na utamaduni wenu.
Mafanikio sio tukio la akilli Bali tukio la kinidhamu ambalo hutokana na utamaduni.
Sio ajabu watu wakilalamika oooh! Familia zinazoongoza ni zilezile.
Sijui Makampuni makubwa yanaongozwa na watu Fulani. Tangu miaka na miaka. Sijui wanaajiriwa ndugu.
Wewe ni mtu back. Hata ukiajiriwa utapewa nafasi kama mtu back.
Kila kampuni inamission na Visions. Hizo vision haziwezi kutimizwa na watu back.
Acha nipimzike tuu. Wakinipopoa mnaruhusiwa.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa Sasa Dar es salaam