Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizi picha, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.[/uFONT]
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANIKwamba, Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wataje dau kabisa ili nikimlengesha niwe na uhakika napata milioni ngapi, mambo ya kwenda ku negotiate tena hayatakiwi.
Btw huyo msemaji wa jeshi la polisi anayejiita Advera Senso sijui kwanini simpendi, analeta mapozi kwenye kazi zinazohitaji umakini mkubwa.
ingekuwa vizuri, tungejua Uharifu na matukio mbalimbali wanayotuhumiwa kufanya
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANIKwamba, Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizi picha, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribú, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria. Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
View attachment 100297 View attachment 100300
Imetolewa na:- Advera Senso - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)
Inawezekana hawa wanaowatafuta waliwakamata na kuwapiga picha,lakini kwa uzembe wa polisiccm wakawaruhusu watoroke!!!!
Hivi hiki kituo cha polisi kilichopo "Caribu" kiko maeneo gani? Kipo kaloleni A town
Hahahahahaaaaaaaaaaaaa, umemaliza mkuu. Yaani picha wawapige wao, then taarifa tutoe sie haya sasa majanga!
Mbona hii nyingine kama picha yangu niliyoiweka kwenye Cv au application za kazi mtandaoni washaicopy na kupaste sasa ndio wananitafuta kuwa nishapata kazi manake niliapply na upolisi labda ndio wananitafuta nikaanze kazi ngoja niende kituo cha polisi kilicho karibu nami nikaanze kazi!
Hivi hili jeshi la polisi intelijensia yao iko wapi? Kila kitu wanategemea taarifa kutoka kwa wananchi. Wao kazi yao nini hasa? Aarghhhhhh!! Pinda
Madai yao ni kwamba wanataka watugaie hilo "Donge Nono" na sie wengine, what the hell