Watu hao wanatafutwa jeshi la polisi kokote walipo

Watu hao wanatafutwa jeshi la polisi kokote walipo

LUPPO G

Member
Joined
Mar 6, 2013
Posts
60
Reaction score
8
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
​
Kwamba, Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizi picha, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribú, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria. Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.

picha za washukiwa 117.jpg picha za washukiwa 133.jpg
Imetolewa na:- Advera Senso - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)

Attachments

duh sijui walifanya makosa gani watanzania hawa???
 
View attachment 100297 View attachment 100300
Imetolewa na:- Advera Senso - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)

ingekuwa vizuri, tungejua Uharifu na matukio mbalimbali wanayotuhumiwa kufanya
 
Mbona hawaonekani kama ni "hatari" ?

Hata bunduki ukiishika huwa hainekani kama hatari kwa jinsi ilivyo tofauti na kisu kikali kinachong'aa, lakini shughuli itokanayo na bunduki ndio utaona jinsi ilivyo balaa. Watu hatari siku zote wanamwonekano wa kiungwana tofauti na jinsi tulivyozoea siku zote mtu mwenye sura nzito ndio bandidu
 
duh sijui walifanya makosa gani watanzania hawa???

Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizi picha, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.
 
kumbe nao wana taarifa tu,! mi mwenyewe nina tetesi za kuaminika upatikanaji wao ni mgumu
 
wangewakamata kipindi wanawapiga picha.

Unanikumbusha utani wa JAMBAZI SUGU aliyeona tangazo la ANATAFUTWA NA ZAWADI NONO ITATOLEWA; jamaa akenda kituoni na kuwambia maafande NIMEKUJA KUCHUKUA ZAWADI YANGU:A S wink:
 
Hivi hili jeshi la polisi intelijensia yao iko wapi? Kila kitu wanategemea taarifa kutoka kwa wananchi. Wao kazi yao nini hasa? Aarghhhhhh!! Pinda
 
Jana kwenye habari itv ilionyeshwa na picha ya mwanamke.Jumla zilikuwa picha tatu. Mbona leo zimewekwa picha mbili?
 
Donge Nono ndio ngapi bhana? si aweke kabisa mpunga mezani watu waingie chaka? unaweza kutoa ushirikiano wa hali ya juu ukaambulia buku kumi kisha wanakwambia ndio RATE za serikali
 
Back
Top Bottom