Watu 17 wahofiwa kufa maji kisiwani Pemba

BOLT

Member
Jan 25, 2011
38
1
Watu 17 wahofiwa kufa maji kisiwani Pemba

Na Salma Said,
WATU 17 wanahofiwa kufa maji katika kisiwa cha Pemba baada ya jahazi waliokuwa wakisafiri kuelekea Tanga kupasuka vipande viwili huko Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Ajali hiyo inaelezwa kutokea jumapili iliyopita ambapo watu 18 walikuwa wanasafiria chombo hicho aina ya jahazi ambalo haikufahamika mara moja kama lilikuwa limeondoka kwa ajili ya kusafirisha abria au kwa ajili ya ya shughuli za uvuvi.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa kaskazini Pemba Yahya Rashid Bugi amehibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo alisema mtu mmoja amepatikana akiwa hajitambui ambapo aliganda katika mikoko katika bahari ya hindi eneo la Wete.
“Tumepata taarifa hiyo kwamba kuna mtu ameokotwa katika mikoko akiwa amefariki lakini baada ya kufika tukamchukua na kumpeleka hospitali na kukaguliwa kumbe ni mzima kwa hivyo amepatiwa matibabu na sasa anaendelea vizuri” alisema Bugi.
Kamanda Bugi alimtaja Mussa Shamim Juma (15) Mkaazi wa Kangagani mkoa wa kaskazini ambaye ameokolewa ambapo alipelekwa katika hospitali ya Wete baada ya kuokolewa na sasa amepatiwa matibabu na hali yake inaendelea vyema lakini bado ameachwa apumzike hospitalini hapo.
Alisema kwa mujibu wa maelezo ya Juma, chombo hicho kiliondoka katika bandari ya Wete tokea jumapili iliyopita kikiwa na jumla ya watu 18.
“Tumemhoji ametwambia yeye alikuwa na watu wengine 18 katika chombo hicho lakini wenzake hawajui ila amemtaja mtu mmoja kwa jina la Kassim ambaye anamtambua alikuwemo kwa sababu yeye alikuwa hajui wenzake wanakwenda wapi ila alidandia tu” alisema Kamanda Bugi.
Kamanda Bugi amesema chombo hicho hadi sasa hakijajulikana na chombo cha aina gani na jina la chombo hicho kwa kuwa mtu aliyeokotwa hajajua na wamejaribu kuulizia katika bandari ya Wete kujua kwamba chombo hicho kina usajili aua laa.
“Tumeulizia kuhusu usajili lakini bahati mbaya hatujajua kama ni mashua ya aina ani na hatujui usajili wake wala jina lake maana mtu tuliyemuokoa hajui chombo hicho kinaitwaje wala hamjui nahodha wa chombo hicho maana baadhi ya watu hutumia vyombo hivi kienyeji bila ya kutoa taarifa pale wanapoondoka” alisema Kamanda huyo.
Ajali hiyo imetokea saa nane za usiku ambapo chombo hicho kilipasuka baada ya kutokea dhuruba ya upepo mkali na kusababisha chombo hicho kupasuka vipande vipande na watu 17 kusambaratika baharini hapo.
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vikosi vya serikali ya mapinduzi zanzibar linaendelea kuwatafuta watu hao ambao hadi sasa haijafamika wamepotelea wapi na haijajulikana kama wahai au wamefariki.
Aidha kamanda Bugi alishauri wasafiri na manahodha wa vyomvo hivyo kutumia utaratibu mzuri wa kutoa taarifa wanapoondoa vyombo baharini kwani kufanya hivyo kutasaidia iwapo chombo kimepatwa na matatizo kikiwa baharini kwa kuwa kina usajili na taarifa za kuondoka zitakuwa zinafahamika na wahusika.


 
Back
Top Bottom