Watu 128 wanufaika na Huduma ya Kupunguza uzito uliopitiliza kwa kutumia Puto Maalum katika Hospitali ya Mloganzila

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila hadi sasa imetoa huduma ya kupunguza uzito kwa watu 128 wenye uzito uliopitiliza kwa kutumia puto maalum (intragastic balloon), ambapo huduma hiyo pamoja na kupunguza uzito imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuwawezesha wateja hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa awali.
87b8effc-2804-4f24-a689-f4a25d7eb3c9.jpg

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Upasuaji MNH-Mloganzila, Dkt. Erick Muhumba na kubainisha kuwa kati ya watu hao 128 waliofanyiwa huduma hiyo wanawake wanne (4) wamefanikiwa kupata ujauzito ambapo mmoja wao alikaa zaidi ya miaka sita bila kupata ujauzito kutokana na tatizo la uzito uliopitiliza.

Dkt. Muhumba ameongeza kuwa zaidi ya watu 12 wameondolewa puto hilo kutokana na uzito wao kupungua na wachache wameondolewa kutokana na maudhi madogo madogo waliyoyapata kutokana na kuwekewa puto hilo hivyo kupelekea kuliondoa.
922cb941-8c4e-453e-9681-ed8006a83b08.jpg

“Wapo baadhi ya wateja wetu takribani wanne tuliwawekea puto lakini tumelazimika kuliondoa kutokana na maudhi madogo madogo ikiwemo kutapika, lakini wengi wao huduma hii imekuwa rafiki na yenye mafanikio makubwa na wapo ambao wametoa baada ya uzito kupungua” amesema Dkt. Muhumba

Dkt. Muhumba amefafanua kuwa wapo ambao wameongeza maji au kupunguza maji kwenye puto kulingana na mahitaji ya wateja, ametoa mfano kuwa miongoni mwa waliongezewa maji kwenye puto kwa lengo la kuendelea kupunguza uzito ni msanii na balozi wa puto Mloganzila Bw. Peter Msechu.

Kwa upande wake msanii na balozi wa puto Peter Msechu amesema kwa kipindi cha miezi sita amepunguza takribani kilo 17 kutoka 144 alizokuwa nazo awali na ameona umuhimu wa kuongeza maji kwenye puto kutokana na kuwa na kasi ndogo ya uzito kupungua.

Msechu ameongeza kuwa tangu awekewe puto ameweza kufanya majukumu yake kwa muda mrefu bila kuchoka, pia amebainisha kuwa uzito wake haujapungua kwa kasi kama alivyotarajia kutokana na kutofanya mazoezi kama alivyoshauriwa na wataalamu hali iliyotokana na ratiba yake kusongwa na majukumu mengi ya kitaifa.
 
Puto mbona haionekani? Hata hivyo, Hongera Mloganzila kwa ubunifu wa huduma hiyo.
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila hadi sasa imetoa huduma ya kupunguza uzito kwa watu 128 wenye uzito uliopitiliza kwa kutumia puto maalum (intragastic balloon), ambapo huduma hiyo pamoja na kupunguza uzito imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo kuwawezesha wateja hao kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi tofauti na ilivyokuwa awali.
View attachment 2704408

Kwa upande wake msanii na balozi wa puto Peter Msechu amesema kwa kipindi cha miezi sita amepunguza takribani kilo 17 kutoka 144 alizokuwa nazo awali na ameona umuhimu wa kuongeza maji kwenye puto kutokana na kuwa na kasi ndogo ya uzito kupungua.

Msechu ameongeza kuwa tangu awekewe puto ameweza kufanya majukumu yake kwa muda mrefu bila kuchoka, pia amebainisha kuwa uzito wake haujapungua kwa kasi kama alivyotarajia kutokana na kutofanya mazoezi kama alivyoshauriwa na wataalamu hali iliyotokana na ratiba yake kusongwa na majukumu mengi ya kitaifa.

Kilo 144 kha
Alikuwa kazidisha sana uzito
 
Kilo 144 kha
Alikuwa kazidisha sana uzito
Kwa maisha haya ya gari, ndani, bar, kitimoto, bia, gari, ndani, ofisini, gari,ndani.

Wengi wanelekea huku.

Nilikuwa naongea na cousin wangu masaa machache yaliyopita.

Nikakumbuka siku moja kaka mkubwa Poppy Hatonn aliniambia katembea kutoka Msasani mpaka Upanga.

Kwa sababu ilikuwa ndiyo style yake tu.

Leo nani anafanya hivyo?
 
Kilo 144 kha
Alikuwa kazidisha sana uzito

nadhani ni abdormal hizoo kiloo nyingi sana asee mafuta matupu. huo moyo mirija imebanwa na mafuta mshtuko kidogo tuu heartattack.

uzito huo unatakiwa uwe na mke mvumilivu dakika 1 uko hoi. kupiga pushup ukiwa na kilo 144 sio kazi ndogo.
 
Kwa maisha haya ya gari, ndani, bar, kitimoto, bia, gari, ndani, ofisini, gari,ndani.

Wengi wanelekea huku.

Nilikuwa naongea na cousin wangu masaa machache yaliyopita.

Nikakumbuka siku moja kaka mkubwa Poppy Hatonn aliniambia katembea kutoka Msasani mpaka Upanga.

Kwa sababu ilikuwa ndiyo style yake tu.

Leo nani anafanya hivyo?
Vifo visivyoeleweka haviko mbali sana

Uzembe sana kujiachia kilo nyingi
 
Naomba mwenye ufahamu atueleze madhara hasi ya kuwekewa puto kwa ajili ya kupunguza uzito.Nauliza hivyo kwa sababu Ulaya na Marekani kuna watu waliozidisha uzito lakini hawakimbilii sana kuwekewa maputo.
 
Back
Top Bottom