Watu 120 wakiwemo wapenzi wa jinsia moja wakamatwa kwenye kilabu cha usiku Uganda

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,279
Polisi nchini Uganda wamesema wamewakamata watu 120 katika Baa moja mjini Kampala na kukamata dawa za kulevya katika operesheni hiyo. Baa hiyo inaruhusu wapenzi wa jinsia moja kuburudika katika sherehe maarufu usiku wa kila jumapili. Lakini polisi wamekana kuwa walikuwa wamewakusudia watu wa jinsia moja.

Polisi wamesema walidokezwa kuwa dawa za kulevya zilikua zikivutwa kwenye baa hiyo. Kisha wakaamua kufanya uvamizi wakati wa usiku.

Watu waliokutwa hapo waliamriwa kuvua viatu vyao na kuketi wakati ukaguzi ulipokuwa ukifanyika. Mamlaka zimesema walikuta dawa za kulevya ikiwemo opium.

Waliokamatwa wanashikiliwa kwa 'kulifanya eneo hilo sehemu ya kuvutia madawa' na watashtakiwa baadae.

Frank Mugisha, mwanaharakati maarufu wa haki za watu wa mapenzi wa jinsia moja, anadai kuwa watu wengi walikamatwa kwenye bar hiyo inayoruhusu watu wa mapenzi ya jinsia moja ,hali inayoashiria vitisho dhidi ya watu wa jamii hiyo.

Lakini msemaji wa jeshi la polisi mjini Kampala amekana kuwa walikuwa kwenye operesheni dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Serikali ya Uganda imekataa kuwa ina mpango wa kuweka sheria mpya ya kuwalenga watu wa mapenzi ya jinsia moja, Baadhi ya wabunge wamesema wataweka mezani muswada utakaopendekeza adhabu ya kifo kwa watu wanaojihusisha na mapnzi ya jinsia moja.

Tarehe 16 mwezi Oktoba, wanaume 16 walikamatwa kwa madai kujhusisha na mahusiano kinyume cha sheria.

Sheria inasema nini?

Sheria inaelezea kitendo cha ngono kinyume na maumbile kama mwanamume kushiriki ngono na mwanamume mwengine au mwanamke kwa mwanamke.

Miezi kadhaa iliyopita waziri wa maadili nchini Uganda alisema kuwa shughuli zote za wapenzi wa jinsia moja ni haramu na kinyume na tamaduni za watu wa Uganda.

Simon Lokodo aliuambia mkutano wa waandishi habari kuwa shughuli za wapenzi wa jinsia moja haziruhusiwi kamwe Uganda.

Katika jamii yetu maswala ya ngono huwa ni ya siri mno, itakuwaje kuwa sasa masuala ya ngono yanawekewa gwaride?, aliuliza Simon Lokodo , Waziri wa maadili Uganda

Waziri huyo alikuwa akitoa sababu iliyosababisa polisi kupiga marufuku mkutano wa wapenzi wa jinsi moja katika klabu moja ya usiku mjini Kampala.
 
YOWERI KAGUTA MUSEVEN KAKAANGU KAMA UNANISIKIA, ... TAFADHALI KANYAGIA CHINI HIZO PANYA ZISIENEE UKANDA WA AFRICA MASHARIKI.

USHOGA HAUKUBALIKI.
 
Back
Top Bottom