Watoto watatu wateketea kwa moto Rombo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,386
8,135
Watoto watatu wa familia moja katika kijiji cha Lessoroma wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro wameteketea kwa moto baada ya nyumba yao wanakolala kushika moto.

Akizungumzia tukio hilo leo Januari 21, Mtendaji wa kijiji hicho, Emma Mosha amesema tukio hilo limetokea usiku wa saa mbili Januari 20, 2023 wakati mama yao alipotoka nje kumpelekea wifi yake simu jirani kidogo na nyumba wanayoishi ndipo aliporudi akakuta moto umeshika kasi.

Amewataja watoto waliofariki dunia kuwa pamoja na wa miaka saba na wa miaka mitano wanaosoma katika shule ya msingi Kiraro, huku wa tatu aliyeteketea akiwa na miaka miwili.

Mkuu wa wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema chanzo cha moto huo ni baada ya kibatari walichokuwa wakikichezea kudondoka na kushika moto kwenye nyumba hiyo.

"Hawa watoto kuna kibatari walichokuwa wanakichezea na kilidondokea sehemu ambayo ilishika moto ambao uliunguza nyumba nzima wakati mama yao àkiwa hayupo," amesema Kanali Maiga.

MWANANCHI
 
Yaani unaacha Kibatari kikiwa kimewashwa na watoto wako ndani peke yao, anyway, Acha Mungu afanye anavyopenda
Kweli duniani kunamaeneo yapo nyuma sana hdi miaka hii mtu bado anatumia kibatari! uwelewa finyu wa wazaz umeondoa Roho za malaika
MUNGU AWAPUMZISHE MALAIKA WATOTO HAO.
 
Back
Top Bottom