Watoto wanamkataza baba kuoa???

JF kuna mbaba amefiwa na mwenzake some 2 years ago..ana watoto wakubwa age between 12-16 (three of them), wanamkataza huyo mbaba asioe...alipojaribu kuwa-introduce hiyo issue watoto hawataki??
mzee yuko between 45-56 years of age. hii imekaaje...vipi watoto siku hizi wana mamlaka..jamaa anampango wa kuwapeleka wote boarding schools wakirudi likizo wanamkuta mama yao mdogo..what do you think???

Mkuu Tumaini,
Uharamia wa asilimia kubwa ya mama wa kambo (step mothers) ndiyo inawafanya watoto wapate hofu. Ni nyumba chache sana ambazo mama wa kambo ametenda haki kwa watoto waliowakuta.

Ni vema baba aoe ila awe makini sana kumtafuta mwenza wa umri pia ila descent na aweke wazi kabisa kuhusu watoto wake kuwa they are his priority number one. Ikiwezekana wa sign mkataba kabisa kuhusu watoto wake.

Kwa upande mwingine, inaelekea watoto wana bond au walikuwa na bond nzuri na wazazi wao. Na wanaogopa kupoteza bond hiyo pindi baba akileta mwanamke mwingine tofauti na mama yao marehemu.

Anyway, inauma sana kufariki na kuacha watoto katika umri mdogo, iwe kwa mume au mke. Kuna mambo mengi, specifically socially associated with this.
 
Kwa nini wengi tunafikiria kwamba sababu atakuwa mama wa kambo basi ndio sababu kubwa inayowafanya hawa watoto wasitake baba yao aoe. Maoni yangu nadhani watoto walipashwa kukaa na baba yao na kumweleza kwa nini hawataki yeye aoe labda wana sababu ya msingi zaidi kuliko ya kuwa atakuwa mama wa kambo atawanyanyasa etc. Pili malezi ya mama wa kambo kwa watoto msingi mkubwa ni mwanaume kama mwanaume huna mapenzi na mkeo basi matokeo yake yanakuwa ni hayo mama wa kambo kuwanyanyasa watoto.
 
Mkuu Tumaini,
Uharamia wa .....mama wa kambo (step mothers)

Jamani si wote wanakua maharamia, kuna wengine wanajitahidi sana kuwa wazuri, ila ugumu ni kwamba mama wa kambo anatakiwa kuwa mwema kupindukia ndo watoto wanaweza ko notice, akiwa mwema kawaida mara nyingi watoto wanakuwa wepesi kuona ubaya.

kuhusu huyu mzee, pole kwake inabidi afanye kazi ya ziada kuwaelewesha watoto kumkubali huyo mama ama sivyo atampata mke lakini atapoteza uhusiano na watoto wake.
 
swala kubwa hapa nadhani ni hisia za watoto kwa mama yao bado hazijaisha na itakuwa ngumu sana kwao kumudu hali hio kwani miaka miwili ni michache mno kukabiliana na swala la mama wa kambo.labda wanaona hakuna ambaye anaweza kuziba pengo la mama yao au wanaogopa wanaweza kunyanyasika.kitu kingine hapa pia hatujui je uhusiano wa baba na huyu mama mpya umeanza kwa mda gani? na je alikuwa anajificha kwa watoto wake? ni vizuri kama alikuwa anajificha kidogo angewapa watoto upenyo wa kujua kinachoendelea hili waweze kujiandaa na nini kinachokuja lakini sio ghafla baba anataka kuoa.lazima watoto watamchukulia huyo mama kama stranger kwenye nyumba yao na wanaogopa uhuru wao.


hili swala sio dogo kwa watoto na nazungumza hivi kwa vile nimepitia na ilinichukua mda kukubaliana na hali alisi.swala la kunyanyasika wala sio kubwa hapa swala kubwa ni kukubali kwamba baba/mama yuko na mtu mwingine sasa hivi.baadae ukikua ndio unajua kwamba baba/mama nae anahitaji mtu hili hawe na furaha.ushauri wangu hawape mda watoto hao kidogo.
 
Back
Top Bottom