Watoto wanamkataza baba kuoa???

Tumain

JF-Expert Member
Jun 28, 2009
3,154
70
JF kuna mbaba amefiwa na mwenzake some 2 years ago..ana watoto wakubwa age between 12-16 (three of them), wanamkataza huyo mbaba asioe...alipojaribu kuwa-introduce hiyo issue watoto hawataki??
mzee yuko between 45-56 years of age. hii imekaaje...vipi watoto siku hizi wana mamlaka..jamaa anampango wa kuwapeleka wote boarding schools wakirudi likizo wanamkuta mama yao mdogo..what do you think???
 
asewapeleke shule ili apata nafasi ya kuoa ila awapeleke shule ili waache kumtegemea, watoto wanahisi akioa mali zote zitakuwa chini ya mama yao mdogo.
 
Huyo mwanamke pole yake, watoto wameshaanza kuonyesha chuki mapema kwa mama wa kambo kabla hajafika.
Muhimu huyo baba inabidi awakalishe chini na kuwaeleza umuhimu wa yeye kuwa na mke na wao kuwa na mama mlezi. Maana nyumba bila mwanamke bado haijakamilika.
 
bond baina ya watoto na mzazi ni muhimu sana. ingawa hao watoto ni wadogo lakini nadhani si vyema kuwakimbiza kwani wanaweza wakamchukulia baba yao vyengine na hivyo kusababisha mapenzi yao kupungua kwa baba yao. kwavile hao watoto ni wadogo nadhani angewatumilia ujanja wa kuwalainisha kwa vizawadi na ajaribu kuwafahamisha umuhimu wa yeye kuwa na mwenza . inawezekana watoto wana kasumba ya kwamba kila mama wa kambo ana mateso, hivyo pia awathibitishie usimamizi wake kwao kwamba hawatateseka na atakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha mapenzi baina yao na mama mpya.huenda ikasaidia

ni ushauri wangu tu. kama mbovu tia kwenye taka.

quiet
 
asewapeleke shule ili apata nafasi ya kuoa ila awapeleke shule ili waache kumtegemea, watoto wanahisi akioa mali zote zitakuwa chini ya mama yao mdogo.
Hakuna mali za kihivyooo..just average earning (working class)..mawazo yao ni manyanyaso unajua hizi film za ki-nigeria ..
 
bond baina ya watoto na mzazi ni muhimu sana. ingawa hao watoto ni wadogo lakini nadhani si vyema kuwakimbiza kwani wanaweza wakamchukulia baba yao vyengine na hivyo kusababisha mapenzi yao kupungua kwa baba yao. kwavile hao watoto ni wadogo nadhani angewatumilia ujanja wa kuwalainisha kwa vizawadi na ajaribu kuwafahamisha umuhimu wa yeye kuwa na mwenza . inawezekana watoto wana kasumba ya kwamba kila mama wa kambo ana mateso, hivyo pia awathibitishie usimamizi wake kwao kwamba hawatateseka na atakuwa nao bega kwa bega kuhakikisha mapenzi baina yao na mama mpya.

ni ushauri wangu tu. kama mbovu tia kwenye taka.

quiet
Nakubaliana nawe kwa sehemu kubwa watoto wanamuitaji baba yao wakati huu kuliko wakati wowote, atakuwa amefanya kosa kubwa kuwapeleka boarding ili tu yeye apate kuoa. Jambo la kufanya ni kuendelea kuwafahamisha umuhimu wa yeye kuoa, huku akiwaonyesha kuwa hatakuwa mbali nao. Maana tofauti na inavyoweza kuonekana hawa watoto wala hawakatai baba yao kuoa kwa ajili ya mali, bado ni wadogo kuthamini mali kiasi hicho, kinachowasumbua ni security yao. Kama baba atatumia hekima ambayo itawafanya wajenge imani kuwa hawatakuwa peke yao baada ya baba yao kuoa, hawatakuwa na taabu.
 
na huyo mama akiingia ndani ya hiyo nyumba awe mpoleasilete ukorofi wa kimama kambo la sivyo ataipata joto ya jiwe
kuna wanawake wengine hawapendi kulea vizuri watoto wa wanawake wengine
na hivo vitoto vinaonekana vilikuwa na mapenzi mazito na mama yao vina ufahamu mkubwa sana

Baba atumie muda mrefu kuongea na watoto wake na kwa upole na imani watakubali asifanye kitu cha ghafla
 
Inavyoonekana hao watoto eitha walishaona watoto wenzao wanavyonyanyasika na mama wa kambo,au wameshaona filamu ambazo zina parts ambazo kuna manyanyaso,sasa hiyo naona kama vile imewa-affect na wanahisi kuwa labda mama atakaeletwa hapo nyumbani anaweza kuwanyanyasa.

Nionavyo hao watoto wanatakiwa wapate ushauri kuwa sio kila mama wa kambo ni mnyanyasaji.
 
msindima nakubaliana na wewe , lkn 99% ya wanawake wa siku hizi wana roho mbaya na isitoshe inawezekana huyo mama hajawaonyesha mapenzi ndiyo maana wanamkatalia baba yao kuo. na Wewe baba kupeleka watoto bording ili uoe haisaidii sanasana unawajengea watoto chuki kati yako na mkeo huyo mtarajiwa.Ongea nao na waeleze vizuri kuwa utawalinda na hawatanyanyasika na huyo mama mpya na watakuelewa tu.
 
baba awaweke watoto chini azungumze nao. nafikiri watoto pia wanataka baba yao kuwa happy, so akiwaeleza kuwa anajiona hajatimilia bila mwenza watamuelewa.

muhimu pia awahakikishie kuwa atakuwa nao pamoja hata akija mama mpya, na atajitahidi kuhakikisha maisha yao yanakuwa kama mama yao alipokuwa hai.

nafikiri akizungumza nao kiutuuzima masuala haya, haitokuwa suala gumu sana kwao kumuelewa.
 
Huyo mwanamke pole yake, watoto wameshaanza kuonyesha chuki mapema kwa mama wa kambo kabla hajafika.
Muhimu huyo baba inabidi awakalishe chini na kuwaeleza umuhimu wa yeye kuwa na mke na wao kuwa na mama mlezi. Maana nyumba bila mwanamke bado haijakamilika.
....Yawezekana watoto wameona mama mwenyewe ni mjasiria mali sana anaweza kumfilisi baba yao na wao wakalost jumla..So they are right...reaction ya watoto inategemea sana na mama mwenyewe!!! akina mama wengine hapendi kuwalea watoto wa mke mwenzake aliyetangulia!!!
 
na huyo mama akiingia ndani ya hiyo nyumba awe mpoleasilete ukorofi wa kimama kambo la sivyo ataipata joto ya jiwe
kuna wanawake wengine hawapendi kulea vizuri watoto wa wanawake wengine
na hivo vitoto vinaonekana vilikuwa na mapenzi mazito na mama yao vina ufahamu mkubwa sana

Baba atumie muda mrefu kuongea na watoto wake na kwa upole na imani watakubali asifanye kitu cha ghafla

Ngojeni amlete huyo mwanamke halafu azae mtoto wa kwanza muone! Mama wa Kambo si MAMA
 
yaani huwa nashindwa kuelewa huwa ni Ibilisi anawaingilia au??
Kila kitu mbona anasingiziwa ibilisi?? Si Yeye! Bali Kiburi,. Akishazaa ndo atajiona amefika!Mnyanyaso kwa watoto wa kambo Kwenda mbele! mimi kama huyo mwanaume nafunga kizazi changu! eti? si watoto tayari nakuwa ninao???
 
Duh wamama wa Kambo nuksi sana ndo utaona ukatiri wa mwanamke watoto wameshtuka hilo bora mzee asioe kama vp huyo mama kama atamuoa awe anakaa nyumba tofauti na watoto.
 
lakini yote haya mnayataka wanaume huwa hamuwapi watoto nafasi ya kuwasikiliza kila mama kambo anachosema nyie mnakubali tuwafanyeje sasa???
 
Back
Top Bottom