Watoto wa viongozi bungeni: Makamba, Msuya, Kawawa(2), Sokoine, Mwinyi...

So what ????!!!!! crap

It is not crap, it makes a lot of sense to me. Hii inaonesha kuwa tayari tumeanza kufikia mji ambao tulikuwa hatuutaki. Kwamba tuna tabaka la watawala na la watawaliwa. Tuliona kuwa BOT walijazwa watoto wa vigogo hata wasiokuwa na qualification, kwenye chama au kwenye vyama it is repeating itself, tukianza kuingia kwenye majeshi hali itakuwa mbaya zaidi.

Maana yake ni kuwa waliojuu wataendelea kuwa juu na waliochini wataendelea kuwa chini. Tutakuwa Kingdom inayiotwa Republic..
 
It is not crap, it makes a lot of sense to me. Hii inaonesha kuwa tayari tumeanza kufikia mji ambao tulikuwa hatuutaki. Kwamba tuna tabaka la watawala na la watawaliwa. Tuliona kuwa BOT walijazwa watoto wa vigogo hata wasiokuwa na qualification, kwenye chama au kwenye vyama it is repeating itself, tukianza kuingia kwenye majeshi hali itakuwa mbaya zaidi.

Maana yake ni kuwa waliojuu wataendelea kuwa juu na waliochini wataendelea kuwa chini. Tutakuwa Kingdom inayiotwa Republic..
kweli kabisa,na BOT ni mfano hai,sasa tumeingia ktk utawala wa DOMOKRASIA.Sijui wajukuu zetu watatuonaje miaka ijayo
 
nampenda lowasa kwa kuwa mtu wa vision,yeye amemuwezesha mwanae kutoingia ktk politics za nchi hii.he will build the empire ambayo baba ameweka msingi madhubuti kuliko kurithisha watoto siasa kama akina Mubarak wa Egypt, and syria

Wewe nawe endelea kusinzia tu!! Hivi unafikiri mwisho wa Frederick utakuwa wapi kama siyo kwenye siasa? Sasa hivi yuko Ulaya anajipanga jinsi atakavyoingia kwenye siasa. Hivyo usitoe hitimisho kabla hakujacha!! Mwone Mubarak mtoto wake alikuwa anafanya kazi London akamwita na kuja kumpa madaraka makubwa kwenye Chama. Hivyo sikubaliani na wewe kuanza kumsifia Lowasa kungali mapema hivi. Naona unampigia debe ili aje awe Rais na matokeo yake utayaona.
 
mimi kwa intelijensia yangu mwenyewe naliona hili la vigogo na watoto wao ktk siasa kwa mitazamo tofauti kama ifuatavyo;-
1) Kuongezeka kw daraja kati ya walio nacho na wasio nacho. Kivipi?
Kwa hilo inaonesha kwamba watoto wa viongozi na watu wachache wenye uwezo wamepata elimu bora yenye vikorombwezo vyote, ambayo imeweza kupanua exposure yao pamoja na kuwaequip na knolwdge yao as well as leadership skils huku watoto wa watz wa kawaida wakipata elimu ya kimagumashi ambayo haimuequip na vitu vyote hivyo zaidi ya kusoma, kuandika, na kuhesabu, hata walewaliofika chuo bado huwezi linganisha na wa vigogo wa kwao wamesoma vyuo vya mbele bila tabu hawa wa kwetu mara bodi wamezingua! Sijui wahadhiri wamegoma yan full vikwazo ukikompea na wa vigogo.
Pili, ktk hili la gap kati ya matajiri na maskini kuongezeka limechangia kuongeza watoto wa vigogo madarakani kwa sababu michakato ya kusaka ridhaa kuteuliwa na vyama cha siasa, kugombea na hadi kuchaguliwa vimeghubikwa na rushwa, fitna, majungu, na michezo michafu yote unayoijua ambayo inawazuia watz wa kawaida coz hawana fedha za kuhonga na kugharamia takrima ya viongozi na wapiga kura, pia kama huna 'godfather' ka baadhi ya watoto wa vigogo hata ukishindwa utapokwa tu ushindi wako.
2). Kuporomoka kwa maadili ya uongozi.
Siku hizi uongozi si utumishi wa wananchi bali ni utwana, mchongo wa kutoka kimaisha na ulaji na hivi vitu hawa watoto wanaona kwa wazazi wao kwa hiyo na wao wanastruggle na wako radhi kufanya chochote ili na wao waje 'kula bata' kama wazazi na kwa kutumia chance, influence, na position za wazazi wao inakuwa easy sana kwa wao kupata uongozi unlike hawa watoto wa watz wa kawaida.
Pia kwa sababu viongozi wengi wamekuwa sio waadalifu, wamejilimbukizia mali na kuhujumu uchumi wanawapatia uongozi watoto na jamaa zao kwa sababu hao viongozi watakuwa loyal to them na watatetea na kufunika maovu ya wazazi wao bila aibu na bila kuathiri biashara na vipato vyao.
3). Ulevi wa madaraka na ulimbukeni wa siasa,
Viongozi wetu wamelewa madaraka yani wanajiona kama wao ndo tabaka lilioumbwa kutawala so after them wanalazimisha vitoto vyao navyo viwe vitawala hata kama havina uwezo, wamekuwa wakibeba kuanzia mashuleni kwa juhudi hata wengine kuthubutu kuwaibia mitihani! Wanapachikwa ktk idara nyeti ili kuandaliwa though hawana uwezo. Pia nimesema ulimbukeni wa siasa coz kuna wengine mbali kujiingiza ktk siasa kwa malengo maalum, au kutumikia matakwa ya watu wanajiingiza kutafuta umaarufu,kuonyesha their family superiority.
kwa hili la watoto wa viongozi kujikita ktk uongozi, sio vibaya ila cha kuangalia wameupataje? Na kwa malengo gani? Na wamepata advantages gani na mteremko gani dhidi ya wenzao ambao sio descendants wa viongozi was it fair challenge?
Hili tuliangalie kwa jicho la 3 linaweza ikawa ni ishara ya tatizo ktk jamii yetu,mfumo wa utawala, na hata mfumo mzima wa maisha au ndo tuchukue ile kauli ya makamba alivyongelea hili alijibu kirahisi tu eti 'hata watoto wa maderva huwa madereva' so it means wao watakuwa viongozi milele na sisi hivi hivi tulivyo
 
Sisi tuendelee tu na kazi za wazazi wetu, ni mwendo wa kurithishana tu.
 
Mimi sishangai kabisa kuwaona haya matoto ya wakubwa kwenye bunge kwani ccm na vyama vingine vine upeo mdogo sana wa kufikiri kuwa vyama siyo mali ya watu fulani au wanzilishi wa chama na pia vyama siyo monarchy kwani mambo haya ya kuridhishana uongozi yamekuwa kichechefu Afrika ya kaskazini na Middle East wananchi wamesema tumechoka. Na kuona mambo yamekuwa hot wakina Gadaffi wanataka dialogue na wananchi its too late na sasa Tanzania itafika wakati wananchi watasema sasa tumechoka then hapa patakuwa hapatoshi we wache waendelee kubunya matunda ya watanzania walio wengi.

Wana JF hii topic ni nzuri sana hongera mwanzilishi.
 
Back
Top Bottom