Watoto wa sikuhizi hawawezi kuelewa

Hahahah imenikumbusha mbali sana kipindi hicho mtaa mzima mimi tu ndo nina laptop nikafahamika kama "mchizi mwenye laptop"
 
Hehehehhe Enzi hizo nilikuwa nalala na Saa 12 Alfajiri ili tu kudownload vitu.
 
Nimeingia kazini tulikuwa na Windows NT, ndo ilikuwa advance 2002 hiyo. Shuleni ilikuwa Windows 95 ikaja Windows 98. Nilisoma windows NT administration, na vikorokoro vyake. Floppy disk zilitutesa sana wakati Ile. Tunafanya project shuleni unasevu kwenye floppy km kumi hivi. Dial up connection za internet yaani ilikuwa balaa. Social media yetu ilikuwa Dar hotwire, msn messenger a yahoo chat. Ilikuwa balaa.
 
Wazee wa MS Dos nao hawajaja bado na zao. Chumba cha kompyuta mnaongia bila viatu na kina AC kali balaa
 
Ilikuwa ukiwasha PC kama vile umewasha feni inavyounguruma.

Hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…