Watoto wa miaka ya 2000 hamtaelewa

Watoto wa miaka ya 2000 hamtaelewa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,286
Reaction score
10,831
Watoto wa miaka ya 2000 watadhani umaskini ulifanya nivae yale "matambala" yanayotumika kwenye mashine za kusaga na kukoboa wakati watu wazima waliponiona na suruali hiyo waliwaambia madogo niliowaacha shule ya msingi wakomae ili wafaulu na kuja kuvaa vizuri kama mimi.

Hapo nimeenda skuli kwa ajili ya mahafali yetu ya kidato cha nne saa mbili nikijua nimechelewa nikakuta ndiyo kwanza madogo wanafanya usafi, nikaona nirudi zangu home kunywa chai.

Ningeitunza hii suruali mpaka leo nina UHAKIKA ingekuwa kubwa tu kwangu.
Ukisoma kitabu cha Luah sura ya tatu mstari wa saba, imeandikwa, "enyi KIZAZI cha modo, heshimuni komenti zenu kwenye picha hii kwa maana mkienenda kinyume, hasira za wavaa bwanga hazitawaacha salama."
356414351_1437861533424404_5084408970739180369_n.jpg
 
Mapana 60'urefu hapa na kigoma. Wengine tulianza nazo msingi unashonewa kaptula ambalo mnaweza ingia wanne, halafu unakua nalo, langu nilishonewa dasara la nne ila nilimaliza nalo la Saba na bado lilikuwa kubwa sana, nashukuru sekondari ilikuwa suruali la sivyo pengine ningeendelea nalo.
 
Back
Top Bottom