Watoto wa masikini kutwa wanabishana kuhusu mpira, wasanii na mapenzi. Umasikini ni laana

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Nimejaribu kufanya utafiti mdogo juu ya hili jambo na kubaini kuwa watoto wengi wa masikini muda mwingi wapo vijiweni wanabishania mambo ya ovyo kabisa.

Mambo wanayobishania ni pamoja na;
1. Mpira - Simba vs Yanga, Manchester United Liverpool Chelsea Arsenal Real Madrid n.k.

2. Muziki - Diamond vs Harmonize, Ally Kiba, Zuchu vs Nandi n.k.

3. Mapenzi

Wakati watoto wa masikini wanapoteza muda wao kwa kubishania ujinga na upumbavu huo, watoto wa matajiri, wanasiasa na wafanyabiashara wapo kama sio kwenye ajira tena za Serikalini au Mashirika walizotafutiwa na baba na mama zao basi watakuwa wamejiajiri kwa kufanya shughuli zao zenye mitaji mikubwa na kuendelea kula maisha.

Nawakumbusha watoto wa masikini kuwa umasikini ni laana, wakifanya mzaha wa kupoteza muda kwa kujadili hayo mambo ya ovyo hiyo laana itaambaa mpaka kwa uzao wao.
 
Daaah!, Kiongozi andiko lako Kama lina Ka-ukweli vile !!! Watoto wa Masikini Chukueni Hatua, it will be too late kama Mtaona mmedharauliwa ....
 
Ni ukweli ulio wazi mkuu.

Nilionaga picha moja wakati vunja bei alileta jezi mpya (timu siikumbuki).

Jinsi ambavyo vijana wengi walikuwa wanapambana kupanda zile ngazi kuingia dukani kununua jezi mpaka unajiuliza Inakuaje unakuwa mtumwa wa mipira kiasi hiki mpaka unahatarisha maisha yako kwasababu ya jezi? Tena una nunua kwa pesa yako na siyo ya kupewa bure.

Lile tukio Kuna mengi kuonyesha ni kwa namna gani tulivyo na jamii ya vijana ambao wamekuwa watumwa wa Kifikra.

Ukweli ni kwamba Tanzania bado tuna WAJINGA wengi sana na Hii ni fursa kubwa sana.

Kijana jichimbie sehemu Jifunze ujuzi mpya baada ya miaka mitatu maisha yako yatabadilika.

Ujinga wako na Uvivu wako ni fursa kwa wengine.

JICHUNGUZE!
 
Upo sahihi mkuu Asante kwa kuchangia Andiko
 
Back
Top Bottom