Watoto wa Mahaouse Girls: Mama bizi, Baba bizi

Petu Hapa

JF-Expert Member
Jan 2, 2008
714
55
Ni dhahiri wazazi wengi ambao ni wafanyakazi waishio mijini watoto wetu wanakuzwa na madada wa kazi ama chekechea. Hali hii ni tete sana, hasa katika makuzi na maadili - pia ni kumnyima mtoto kujifunza kutoka kwa wazazi wake!

Tunaenda kazini asubuhi tunarudi jioni! Haki tumechoka! Tunalea saa ngapi? Ulezi wetu upo katika maudhii gani? Madhara ya
ni nini? Je tunawapenda hao wasadizi wetu ili kujisikia huru kupeleka mapenzi hayo kwa watoto wetu?

Kizazi cha watoto wa mahouse girl!

Tujadili
 
kwa hali ya maisha ilivyo wakati mwingine inabidi mahousegirl wakae na watoto na wazazi kwenda kutafuta riziki,,ila tuwe na ratiba maalum ya kutumia siku za weekend na watoto wetu.
 
Na inabidi kuwapenda hao ma yaya ili wa reproduce hiyo love kwa wanetu (though not guaranteed) otherwise ukiwa mkali sana na maonevu yasiyo na maana eti kwa sababu unamlipa then expect revenge itaenda kwa mwanao

Muumba atuepushe na madhila haya
 
Ni kweli aisee, tunatakiwa nyakati za weekend na off za makazini, plus likizo tuwe tunazitumia vzr pamoja na watoto wetu vinginevyo, watoto wetu watabeba tabia za mahouse gels. Tujitahidi hata kama tupo bizee!
 
sawa house girl anafanya lakini ndio substitute ya mama? sasa baba substitute yuko wapi?
 
kwa hali ya maisha ilivyo wakati mwingine inabidi mahousegirl wakae na watoto na wazazi kwenda kutafuta riziki,,ila tuwe na ratiba maalum ya kutumia siku za weekend na watoto wetu.

Kwahiyo tunakuwa wazazi wa weekend tu! kwa mwezi ni siku 8 kwa mwaka ni siku 96 kweli?
 
Na inabidi kuwapenda hao ma yaya ili wa reproduce hiyo love kwa wanetu (though not guaranteed) otherwise ukiwa mkali sana na maonevu yasiyo na maana eti kwa sababu unamlipa then expect revenge itaenda kwa mwanao

Muumba atuepushe na madhila haya
Yaya hawezi kuwa mzazi jamani! basi tuwape na haki za kutambulika kwamba wao ndio wazazi wa msingi! maana mtoto anamsikiliza dada kuliko hata wazazi wake! ama wazazi wanageuka kuwa viraja mtoto anapoleta usumbufu!
 
Jirani zangu Wachagga.........mtoto wao anaongea lafudhi ya Kigogo
Ni hatari, halafu wazazi kwa moyo mweupe tunasema, yaani huyu mtoto anavyompenda dada yake we acha tu! Mimi nikijaribu kumlisha anasumbua hatari! kwahiyo, hilo la lafudhi zawadi nzuri ya mtoto kwa dada! Mtu ukimtunza si lazima akurande bwana! Ndio wale wanasema! yaani huyu mtoto hafanani tabia kabisa na wazazi wake
 
Kongosho hapo unakuwa umeruka maji umekanyaga moto,ni afadhali akawa nyumbani mtoto ili uweze kumuangalia hata kwa huo muda kidogo unaopata weekend kuliko aende boarding
 
ki ukweli kabisa katika wiki moja! unaweza kutumia masaa mangapi na mwanao? Na huwa mnafanya nini? Weekend je?
 
Back
Top Bottom