Kutolelewa Na Baba na Mama humfanya mtoto asiwe na Upendo, hii ni sababu upendo wa ndani ya jamii Zama hizi kupungua

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,882
Kwema Wakuu!

Ni ngumu Sana kukuta upendo Kwa watoto ambao hawajalelewa na Baba na Mama, hiyo ndio sababu siku hizi kwenye jamii upendo wa wengi umepoa.

Mtoto asipolelewa na wazazi wawili, Baba na Mama yake hisia na vyanzo vya upendo hufa POLEPOLE Kwa uhakika.

Kuachana Kwa wenza, Baba na Mama huathiri hisia za mtoto.
Huwezi ukamlea mtoto wewe mwenyewe bila mwenza wako alafu akakupenda huyo mtoto, labda mwenza wako awe amekufa, hiyo ni tofauti na kutengana.

Moyo wa mtoto aliyelelewa na wazazi waliotalakiana umepasuka mapande mawili, ni ngumu Sana kukuta upendo wa kweli kwake, Labda iwe Exceptional

Hivyo, ni vyema Kama wazazi kuhakikisha tunalea watoto wetu tukiwa Baba na Mama.

Usiku mwema!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
 
Ni kweli mkuu bt maisha ya Sasa na utandawazi unachangia hata Mimi nimeachana na mwenza wangu na mtoto Yuko nae na hakuna mawasiliano na mama Wala mtoto na wazaz wengi huwa mama anampa maneno ya kupandikiza chuki na unakuta hata mtoto anakosa upendo na wewe
 
Hii nikweli kabisa, mbaya zaidi mtengane hata kama niyeye kaamua kuondoka kwasababu zake, afu wewe mambo yakunyokee... Atamwambia alikukataa na ndo alifanya niwe maskini namengine mengi.
Ni kweli mkuu bt maisha ya Sasa na utandawazi unachangia hata Mimi nimeachana na mwenza wangu na mtoto Yuko nae na hakuna mawasiliano na mama Wala mtoto na wazaz wengi huwa mama anampa maneno ya kupandikiza chuki na unakuta hata mtoto anakosa upendo na wewe
 
This is me, I can feel it. Sina upendo kabisa, I don't do love things.Situlii kwenye mahusiano, I can't feel someone's pain, Kuna kipindi mpaka one of my girlfriends alikuwa analia na kunyong'onyea sana daah..., ila kwasasa nimelitambua hili baada ya kutafakari kwa kina. I am working on it, I am trying to change it, I know I'll succeed.
R.I.P my lovely mama

Sent from my SM-J415F using JamiiForums mobile app
 
Upo sahihi .. Mimi huyu mwanangu hapa Nipo naye na Mama Yake sometimes anakuwaga na Vitabia Fulani Ambavyo mama Yake hamkoromei (nahisi hii wanwake wengi wanaona Sawa kwa Baadhi ya vitabia). Ila kwa ss wanaume hasa kwa mtoto wa kiume tunaona Anakuwa mjinga.

Wazazi wawili ni muhimu. Ingawa Kwa Sasa Waafrika wengi wameharibikiwa
 
True wengi huwa na changamoto za kimaadili, kama ni wanawake huwa pasua kichwa sana.
Sababu ya ukosefu wa kubalance. Ni labda tu mzazi awe na hekima ya malezi
 
Kuachana uathiri zaidi watoto na ndo lengo la shetani.
 
Attachments

  • VID-20220515-WA0028.mp4
    12.5 MB
  • VID-20220515-WA0030.mp4
    12.9 MB
Kumbukatia mtoto mdogo kifuani kuna faida kubwa Sana kiafya hata kwenye usawaziko wake ukubwani.
 
Kwema Wakuu!

Ni ngumu Sana kukuta upendo Kwa watoto ambao hawajalelewa na Baba na Mama, hiyo ndio sababu siku hizi kwenye jamii upendo wa wengi umepoa.

Mtoto asipolelewa na wazazi wawili, Baba na Mama yake hisia na vyanzo vya upendo hufa POLEPOLE Kwa uhakika.

Kuachana Kwa wenza, Baba na Mama huathiri hisia za mtoto.
Huwezi ukamlea mtoto wewe mwenyewe bila mwenza wako alafu akakupenda huyo mtoto, labda mwenza wako awe amekufa, hiyo ni tofauti na kutengana.

Moyo wa mtoto aliyelelewa na wazazi waliotalakiana umepasuka mapande mawili, ni ngumu Sana kukuta upendo wa kweli kwake, Labda iwe Exceptional

Hivyo, ni vyema Kama wazazi kuhakikisha tunalea watoto wetu tukiwa Baba na Mama.

Usiku mwema!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Kwa upande mmoja ni sahihi unachokisema. Kwa upande mwingine siyo. Hata wale wanaoelelewa na wazazi wote wawili baadhi yao wamegeuka kuwa monsters katika dunia hii. Hii inaleta mashaka kwa ukweli wa hoja yako. Labda tatizo ni mazingira: mtoto anayelelewa na kukua katika mazingira mazingira mazuri kuna likelihood ya kuendelea kuwa mtoto na mtu mzima mzuri. Wakati yule anayelelewa katika mazingira duni/ovyoovyo hata kama yuko mikononi mwa wazazi wake wawili kuna likelihood ya kuwa monster.
 
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom