Watoto wa kariakoo mpo jf?

Watoto wa kariakoo mpo jf?

KIFILI

Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
87
Reaction score
20
Leo nataka tukumbushane mji wetu mkongwe,mji maarufu wenye historia kubwa ndani ya nchi hii lakini inayoelekea kupotea.Mko wapi watoto wa kariakoo wa ukweli mtueleze tuijue kariakoo iko vipi,ilikua vipi,raha na karaha za mitaa ya kariakoo,na je kariakoo ya zamani na ya sasa zinalingana?karibu sana maskani mnaoijua kariakoo kiundani mtujuze sie wakuja maana ndo kwanza tunaishi kwenye maghorofa mapya baada ya wenye mji kuukimbia mji wao,maana tumekuwa tukiyasikia mengi kuhusu mitaa hii ilivyokua zamani.
 
kaangalie kwenye kamusi ya kiswahili utaona maana yake halisi...mzee,usikurupuke.

Sijakurupuka hapa tatizo ni mkanganyiko mpaka mtu afukunyue kamusi sio leo kwa hiyo inabidi uendane na mabadiliko ya kwenye jamii
 
Sijakurupuka hapa tatizo ni mkanganyiko mpaka mtu afukunyue kamusi sio leo kwa hiyo inabidi uendane na mabadiliko ya kwenye jamii

Kiswahili kina utajiri mkubwa sana wa maneno tatizo watu wavivu wanakopa maneno kwenye lugha nyimgine wakati kiswahili kinajitosheleza,mimi nimeamua kuonyesha mfano ili watu wajifunze na kuyajua maneno yakiyosahaulika kama hili la id yangu
 
Hiyo misheni kota bado kuna utata kama iko ilala au kariakoo,maana ilala hawaikubali na kkoo haijakubalika sana
 
Hiyo misheni kota bado kuna utata kama iko ilala au kariakoo,maana ilala hawaikubali na kkoo haijakubalika sana

Sasa kama haikubaliki kwa ilala na kariakoo pia basi haina nima sie tuna mji wetu Ndio huu Misheni Kota...

Zamani nilikuwa naishi Upanga Tukapata Jirani Mzee Flan alihamia na Mtoto wake anaitwa Perry huyo Dogo alikuwa anajua aina zote za matusi ya kkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkkmdomoni tokea siku hizo nilikuwa najua matusi ni jadi ya Watu wa Kariakoo but miaka hii wengi weshahama na kuhamishwa matusi hakuna maisha ni raha kwa sie tuliyehamia miaka kadhaa iliyopita..

FF bado anayo yamemkaa mdomoni ukimgusa hata kwa bahati mbaya anakumwagia mitusi
 
Kulikuwa na Mwizi Maarufu alikuwa anaitwa Ali Gulu.. Cha kushangaza alikuwa ana mguu mbovu anachechemea lakini ni mwizi tena yule wa kukaba na anaondoka pole pole hakimbiii alikuwa anakuja hadi mitaa a kwetu kuba na wenzake mitaa tote ya Upanga kawaliza sana wahindi na waswahili...

ukisiikia mtu anataka kwenda kariakoo unamshangaa na kumuuliza wewe humuogopi Ali Gulu
 
Watu wa upanga nao bwana kweli wahindi,yani mlikua mnamuogopa mlemavu eti anawabia then hakimbii anatembea tu,kweli nyie ni watu wa upanga.
 
Kariakoo ilikua zamani,siku hizi wamevamia wageni na kuondoa radha yote ya kariakoo,sasa hivi wamejaa wachagga na wakinga na wapemba!bora wapemba walikuja siku nyingi kidogo
 
sina maana hiyo,hiki ni kiswahili fasaha kaka,tafuta kamusi tu utaelewa na kufurahi na roho yako

Kwa nini utulazimishe kutafuta kamusi toa maana yake basi wewe au ibadilishe
 
Back
Top Bottom