Watoto wa kambo

64Bits

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2012
Posts
961
Reaction score
565
Habari zenu wana MMU, wakubwa shikamooni.

Leo kuna jambo naombeni wenye uzoefu wanipe mawazo yao.

Mimi ni mama wa kambo kwa mtoto wa kiume wa miaka 8.

Nilimkuta baba yake amesha achana na mama yake kabla hatujaanza mahusiano.

Jamani mtoto huyu amekuwa mtihani kwangu, hata nimfanyie nini mimi mbaya tu kwake, nampenda, namjali namfanyia wema wote ambao mtoto anatakiwa afanyiwe lakini shukrani yake ni kunizulia uwongo wa kila aina.

Najisikia kumtazama tu nimuache afanye analotaka nisimuonye... asofunzwa na ***** atafunzwa na ulimwengu.


Halafu baadae nafsi inanisuta najirudi tena naambulia maneno tena.

Jamani si kila mama wa kambo mbaya na si kila mtoto wa kambo mzuri... kuna wengine wanaweza kukukalia kooni ka mwiba wa samaki.

Najuta akija weekend maanake sikai nae ila babake atamchukua tuishi wote soon.

Wakubwa nipeni mawazo yenu naishije kwa amani nae?

Kama kuna "mtoto wa kambo" humu ndani anaweza kushare experience yake labda itanisaidia kuelewa ni nini huwa kinapita kwenye akili zenu?
 
tatizo liko kwako na.mumeo, hakuamini vya kutosha kulea mwanaye. Ndio maana hakubaliani na adhabu zako.
 
Pole..thread za saa hizi ujue mtu kweli yamemkuta pole saana.......jifunze kwanza kumfurahisha.....na kumdharau...usipende kumpiga na kumfokea..you have to win his heart.....jua nini anapenda...ice cream? mpira? vijali hivyo pia.....mletee ice cream..na zawadi siku kukiwa hakuna mgogoro wowote....ila akikosea mchape au kumfokea kama kawa..wazungu wanaita 'carrot and stick'...
 
Pole sana, usikate tamaa hata biological children wengine wako hivyo wanaendesha wazazi mpaka unaweza kukufuru kwa kusema maneno mabaya. Jitahidi sana muone kama ni wako wa kuzaa mwenyewe muonyeshe pia upendo wa hali ya juu, na anapofanya kitu kizuri/vizuri basi usisite kumpa hongera pia. Wazazi wengi mara nyingi wanajisahau na kuangalia vituko vya watoto wao pale vinapowakera lakini wanapofanya vizuri wengi hujisahau kutoa pongezi/hongera. Ipo siku atakuja kukumbuka malezi yako na kukuona kama mama yake mzazi. Kila la heri.
 

ila mtu hukai nae inakuaje tena unataka kum discipline? why not muachie baba yake ya kum discipline' for now,wewe kuwa 'a good cop' muache baba awe 'the bad cop'
 
How is your relationship with his mother? I believe kids have pure and innocent hearts by nature unless we show them otherwise...
A child would always want to see his/her parents together.
Just give as much love and care as you can. Try to find better ways to corrent him when he is wrong...
 
Wakati unaingia kwenye maisha yao, mambo ya nidhamu na ufundishaji wake (kwa huyo mtoto) mliyajadili na baba'ake?

Baba wa mtoto hapo ana dhima kubwa ya kuhakikisha mwanae (mwanenu) anakuwa na adabu, heshima, na taadhima kwa wazazi wake wa kumzaa pamoja na wewe wa kambo.

Mtoto wa miaka 8 bado ni mdogo vya kutosha kuweza kurudishwa ndani ya mstari lakini ni lazima baba mtu ahusike kikamilifu.

Ongea na baba'ake na kama una uhusiano mzuri na mama'ake, ongea naye pia.
 
Aisee thats very complex sio siri, kwa wale mnaopanga kuolewa na watu wenye watoto be very careful. Haiwezekani 100% ukafit kumfutahisha likewise hawezi 100% kukufurahisha vumilia tu.

Sishauri kbs aina hizi za ndoa isipokuwa huyo mzazi alifariki! Vumilia tu, utafanyeje sasa?
 
Hili neno.
Mwanaume akihisi mwanae anaonewa. Bila kupima kosa na mwelekeo wa mwanae, ukizingatia kuna sumu kuhusu mama wa kambo basi atakosa sapoti na ataonekana mbaya haswa kama mama mzazi wa mtoto anamlisha sunu mwanae au anampa malezi mabaya.

Ndio maana wanawake wengine wakijionea hivyo wanakuwa wapole na kunyamaza kimya.... mpaka baba ashtuke tayari mtoto ashakua mwiba aka black sheep wa familia



tatizo liko kwako na.mumeo, hakuamini vya kutosha kulea mwanaye. Ndio maana hakubaliani na adhabu zako.
 
Mhh...anakuja wikend tu halafu mnakwazana? Pole..
Jaribu kuwa rafiki yake kwanza, usikimbilie kuwin nafasi ya u mama kwake, bado ana bond na mama yake..
Pia usijaribu kuongea vibaya kuhusu mama yake mbele yake atakuchukia milele (at that age anaelewa kila kitu na hasahau kirahisi so kuwa makini na unachoongea mbele yake)

Pia refer Sigmund Freud na psychoanalysis theory.....ukute dogo anafight na wewe for the sake of his mother...anaokuona adui wa mama yake, so huwezi kuwa mzuri kwake as long as he is in love with mum na wewe anaona umeingilia nafasi na furaha ya mama...!

Nakushauri anza kuwa rafiki yake, kama ni mama tayari anae na huwezi kuchukua nafasi ya mama kwake milele (nani kama mamaaaa by Christian Bella)
Jifunze kuongea nae...ongea nae kuhusu game, shule, homework, mfundishe hesabu na vitu vidogo vidogo ambavyo vitafanya akukumbuke...usimkaripie ovyo, mpe nafasi akae na baba yake, wape task ya pamoja yeye na baba...nk

Pia usisahau vijizawadi kwa mama yake....(hamtoelewana hadi uelewane na mama yake....kama uliingia kwa mapinduzi ya kumwaga damu...ndo pagumu kidogoo)
 
Pole sana, huyo mtoto bado ni mdogo, he can be tamed, tatizo liko ni hivyo anavyokaa wiki nzima kwa mamake hujui anakuwa anaambiwa vitu gani na akirudi baada ya weekend anaulizwa nini na jee comments atoazo mamake mbele ya huyo mtoto zikoje? Akishahamia kabisa itakuwa rahisi kumdhibiti mkishirikiana na babake.
 
Ki saikolojia miaka nane ni too late...

Mwisho wa kumnyoosha mtoto ni miaka saba...

Ila namimi nashangaa kama anakuja week end tu mnagombanaje sasa?

Lakini mi naona cha muhimu kaa na mume wako na mama wa huyu mtoto muongelee future yake...sidhani kama hata mama yake mzazi atapenda kuwa na jambazi as a son...

Communication itawasaidia nyote...maana akiharibika huyo jua na watoto wako watamuiga kaka yao...(most likely)


 
Na hili likitokea la Mwanaume kudhani mwanawe anapoadhibiwa ni kwa sababu anaonewa na "mama wa kambo" basi linaweza hata kuleta dosari kubwa ndani ya ndoa. Mwanaume anatakiwa kuwa muelewa sana vinginevyo mtoto ataharibikiwa na ndoa kuingia dosari. Si kila "mama wa kambo" anayemuonya mtoto kwa vitendo vyake anafanya hivyo kwa nia mbaya au chuki.

 
Huwa nanunua na kusoma vitabu vya malezi ya watoto vya wana saikolojia..
Yes miaka nane ni mdogo ki umri ila si mjinga...anakuwa ameshajua anachofanya na hata kama utampiga utaona reaction yake..anakuwa anatamani ku resist kwani anaona unamuonea na siyo fair...
Kwa hiyo wanasema kama umeshindwa kum mold mwanao unavyotaka awe before miaka 7 andika maumivu...


Kwa nini ni "too late"?



Hmm...kweli? Mwisho kwa mujibu wa nani? Manake kwangu mtoto wa miaka nane bado ni mdogo sana...
 
Kadiri mtoto wa kambo anavyokuwa ndio matatizo hayo yanavyokuwa...mi na miaka 21 now na mtoto wa kambo, amekuwa kama mume mwenzangu tukigombana na mamake wana side upande mmoja, vumilia tu dada ukipenda boga.
 
Mtoto sio mbaya bali anapata ubaya kutoka kwa mama ake. Kuna baadh ya akina mama wanatabia ya kuwafundisha mambo mabaya watoto zao ili wawafanyie mama zao wakambo hali wao wameachika.
 
Asante wote kwa mawazo yenu. Wengi wameuliza anakuja weekend tu tunagombanaje sasa?
Ni hivi mfano mtoto anaweza kutaka kucheza mahali hatarishi mfano jikoni etc, mtoto anaweza kugoma kula na vitu kama hivyo so kuna saa inabidi umueleze na ikibidi uwe mkali for his own sake. Kama hizo zawadi jamani nanua sana nikipita nikiona kinachomfaa na kama nina pesa namnunulia. Mi sio mchapaji kwa kweli wala sijawahi kumchapa na fimbo kuna siku nilimfinya kidogo kwenye makalio baada ya kuwa hasikii anacheza na mpira ndani na kuna saa unapitiliza jikoni na kulikuwa na mafuta ya moto. Mimi sipo hapa kuchukua nafasi ya mamake wala siitaki, ila ndo hivyo tena. Inaniuma sana kuona kila nilifanyalo kwake halina wema, so why bother? Nihangaike na mwanangu tu nijitazamie mambo yanavyokwenda manake mama mtu pia anawapigia simu ndugu za mume wangu kusema mi namtesa mtoto. Acha nikae nae tu kama yai, anachotaka atapewa, sitasema kitu labda aje anifunue sketi yangu ndo ntasema! Mweeee! Kua uyaone!
 

Kim nana nilikuwa nikiyafanya haya na mengine ila saivi kwa kweli moyo wangu unakufa ganzi kila kukicha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…