Watoto ni zawadi pekee

Wakishua org

Member
Feb 23, 2023
20
33
Habari wana jamii wenzangu...

Nipo hapa kukumbushana katika suala la malezi na makuzi ya watoto wetu. Ujumbe huu ni kwetu sote kwa sababu naamini ipo siku kila mmoja atasimama kuwa mzazi.

Jamii ya sasa kutokana na utandawazi unao endelea imetokea watoto kukosa mapenzi ya dhati na kupewa muda toka kwa wazazi wao kiasi kwamba wazazi tunashindwa kufatilia maendeleo ya watoto wetu aiseeee inasikitisha mnoo, kuna baadhi ya wazazi wameajiri watu wengine ili kusaidia jukumu la kulea watoto, kuna wazazi wanatingwa na kazi kiasi kwamba muda wa kutoka hawaonani na watoto pia wakati wa kurudi hawaonani na watoto, vile vile kuna wengine wameamua kuondoa kero za watoto kwa kuwapeleka shule za bweni.

Napenda kutazamia andiko la Robin Sharma katika kitabu chake cha NANI ATALIA, SIKU UKIFA? Nanukuu "Muda ni zawadi adhimu sana unayoweza kuwapatia watoto wako. Pia zawadi adhimu unayoweza kujipatia binafsi ni kufurahia namna halisi wanao walivyo na kuwatambua kwa undani zaidi: hii ni moja ya miujiza katika maisha."
Ndugu zangu naamini bado hatujachelewa katika hili, tunapaswa tuwajibika kutenga muda wa kuwa na watoto wetu ili kuwapa mapenzi, malezi na makuzi. Hii itasaidia kuwafanya watoto wetu kukua vizuri kisaikolojia na pia kuwa na mapenzi mazuri kwetu na jamii nzima kwa ujumla.

Namna tutakavyo walea vizuri watoto wetu basi na wao watakuja kuwa wazazi bora katika taifa la kesho.

Pia naunga mkono Juhudi za Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kutoa katazo la kulaza (bweni) watoto wa awali mpaka darasa la nne nadhani hii itatufanya wazazi tuwajibike katika kuwalea watoto wetu na kuwafatilia kwa ukaribu zaidi...
ASANTENI🙏🏾
 
Habari wana jamii wenzangu...

Nipo hapa kukumbushana katika suala la malezi na makuzi ya watoto wetu. Ujumbe huu ni kwetu sote kwa sababu naamini ipo siku kila mmoja atasimama kuwa mzazi.
Serikali inafanya Mambo Mengi kwa kukurupuka tu Mtoto kukaa mtaani day school ana %kubwa kuharibikiwa that way nasema ni Bora zitungwe sheria za kumlinda mtoto na sio kuwekeana Mipaka mfano Mimi nipo busy na Maisha na ni mke wangu niliye zaa naye ni Malaya anaishi kwa kudanga so unadhani it possible Mimi nimuachie mtoto wangu au mtoto wangu akae bording?
 
Serikali inafanya Mambo Mengi kwa kukurupuka tu
Mtoto kukaa mtaani day school ana %kubwa kuharibikiwa that way nasema ni Bora zitungwe sheria za kumlinda mtoto na sio kuwekeana Mipaka mfano Mimi nipo busy na Maisha na ni mke wangu niliye zaa naye ni Malaya anaishi kwa kudanga so unadhani it possible Mimi nimuachie mtoto wangu au mtoto wangu akae bording?
Ndugu tambua kuwa sheria hazitungwi kwa kuangalia shida ya mtu mmoja mmoja kama hiyo yako, pia kama umesoma vizuri hii sheria haijatungwa siku hizi za karibuni!!!

Tambua kwamba hizi sheria zishatungwa muda mrefu hivyo sasa hivi ni utekelezwaji pamoja na usimamizi.
 
Back
Top Bottom