Watoto na vijana wote wapo hatarini

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,056
2,000
Nguvu kubwa inayotumika katika matangazo ya bia na kondoms hadharani, watoto na vijana wengi sidhani kama watasalimika na kua walevi na wazinifu. Pombe inatangazwa kua ni haramu tu kutumia ukiwa chini ya miaka kumi nane. Na tumia kondums na sio usifanye mapenzi kabla ya ndoa.

Kwa hiyo baada ya miaka kumi, au zaidi ijayo, tanzania itakua niya kizazi cha pombe na zinaa. Achilia mbali mapenzi ya jinsia moja.

Viongozi wa dini inaonekana wamezidiwa na wengineo wanajivinjari katika hayo vilevile.
 

PhD

JF-Expert Member
Jul 15, 2009
4,279
2,000
Kondom, pombe zote ni biashara.

sioni tatizo la kondom wala pombe kutangazwa, ni vema matangazo yatolewe kwa uwazi kabisa watoto waelewe mapema, usiri kwa kujidai kutowafundisha watoto ndio kuna liangamiza Taifa. Nitakupa mfano mdogo ukienda Nchi kama uingereza teenagers wanaanza ngono mapema sana wakiwa high school na vyuoni lakini cases za mimba na magoinjwa ya zinaa ukiwamo ukimwi ni ndogo sana, sababu wanajitambua na kondomu inazunguzmwa kwa uwazi, no condom no sex.
 

makeda

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
276
225
Duu bado kuna watu wana matumaini na hawa jamaa wanaoitwa viongozi wa dini?
Kichwani mwangu nina picha kwamba mungu aliewatuma kawapa maagizo ya kukamua watu na kutafuta sifa za nani zaidi hapa duniani.

Kama watakuwepo waliotumwa na Mungu kweli basi watakuwa kwenye mtihani wa kupambana na (wachungaji)watafuta shekeli km waganga wa kienyeji. infact ninawasiwasi kama some of them
Nature ya madhabahu zao si za kiganga.

Nguvu kubwa inayotumika katika matangazo ya bia na kondoms hadharani, watoto na vijana wengi sidhani kama watasalimika na kua walevi na wazinifu. Pombe inatangazwa kua ni haramu tu kutumia ukiwa chini ya miaka kumi nane. Na tumia kondums na sio usifanye mapenzi kabla ya ndoa.

Kwa hiyo baada ya miaka kumi, au zaidi ijayo, tanzania itakua niya kizazi cha pombe na zinaa. Achilia mbali mapenzi ya jinsia moja.

Viongozi wa dini inaonekana wamezidiwa na wengineo wanajivinjari katika hayo vilevile.
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,056
2,000
kondom, pombe zote ni biashara.

Ndio ni biashara, hata Ukahaba nao ni biashara. Nadhani tunakoelekea tuta anza kuona matangazo ya majumba ya ukahaba katika vipindi vyetu vya tv. Maana kwenye internet tayari ni halali.
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,863
2,000
Hayo ndiyo matokeo ya kuwa na watawala wazinzi na wasio na fikra zaidi ya kufikiria chini. Watakufa wengi hapa. Isitoshe wengi wameishapotea na watapotea wengi.
 

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,056
2,000
sioni tatizo la kondom wala pombe kutangazwa, ni vema matangazo yatolewe kwa uwazi kabisa watoto waelewe mapema, usiri kwa kujidai kutowafundisha watoto ndio kuna liangamiza taifa. Nitakupa mfano mdogo ukienda nchi kama uingereza teenagers wanaanza ngono mapema sana wakiwa high school na vyuoni lakini cases za mimba na magoinjwa ya zinaa ukiwamo ukimwi ni ndogo sana, sababu wanajitambua na kondomu inazunguzmwa kwa uwazi, no condom no sex.

sasa nani atakae lea watoto wa mitaani? Kwa taarifa yao vidume vidogo vidogo na vijike vidogo vidogo hua havitumiagi kondom zao. Wana pata exposure ya ngono basi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom