Watoto na UFO (Unidifined Flying Objects) Aliens

RoadLofa

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
1,856
Reaction score
4,085
Baada ya kusoma kitabu cha messengers of deception by an UFO investigator Jacques Valley, akielezea uwepo wa viumbe kutoka sayari nyingine baadhi ambazo hazijavumbuliwa wanaokuja mara kwa mara kutembea duniani kujifunza vitu vilivyopo duniani na kuwafunza vitu vipya vilivyopo kwa vinavyohusu vitu mbalimbali kama technology, nimejikuta najua vitu vingi ambavyo watu wengi hawavijui kuhusu dunia na siri zake, baadhi ya vitu ambavyo kitabu kimeelezea kuhusu U.F.O baada ya kuwafanyia interviews baadhi ya observes wa vyombo ambavyo wamewahi kuviona vikipaa angani kutoka sehemu mbalimbali za duniani kama Egypt na America wamesema sifa za hivyo vyombo ni kama zifuatazo

1. Vina umbo la saucers
2. Ndani yake huwa kuna viumbe ambao wamevaa mavazi kama wanayovaa wazamiaji majini
3. Huongea lugha za ajabu zisizoeleweka
4. Baadhi ya watu huwaelekeza vitu vipya vya kufanya
5. Wakimaliza duties zao upaa na chombo ( saucers) huku wakikuacha na mshangao

Kwa nilivyosoma hiyo investigation book kuhusu U.F.O iliyofanyiwa utafiti kwa miaka kadhaa na kwa sample kubwa tu ya watu ambao ni zaidi ya watu 3000 na kwa population zaidi ya 300,000 kwa knowledge yangu nahisi hao viumbe wapo kwenye sayari ambazo wanasayansi bado hawajafanikiwa kuzivumbua, na inasemekana izo U.F.O mara nyingi utokea sehemu zenye vitu vipya na gunduzi nyingi kama Sourthen Calfornia na sehemu nyingi za majangwa kwenye kitabu Jacques ameandika muda ambao hutokea ni kuanzia saa 4 usiku muda ambao watu wengi huwa ndani kwa hiyo watu wachache hupata bahati ya kuona hivyo vyombo vikipaa kwa kasi angani huku vikitoa mwanga mkali,

Kwa maoni yangu na lengo la kuandika uzi huu naomba mwana Jamiiforums kutushirikisha kama umewahi kuona kitu kama U.F.O ili tupate ufahamu kama Africa je huwa tunatembelewa na U.F.O, kwa mimi nimewahi kuona kitu kama U.F.O kikiwa kinaenda kwa kasi usiku kipindi nikiwa na miaka kama 10 na kadhaa, nachohisi huja Africa sana sema NASA na watu wanaodeal na research zihusuzo aliens hawajaamua kuweka kambi Africa, maana nishawahoji baadhi ya watu wazima wanadai katika enzi zao za utoto wanakumbukumbu walishaona U.F.O , Pia nadharia yangu nyingine inaniambia U.F.O hupenda kuwapa bahati watoto kwa sababu maranyingi huwa akili zinakuwa bado na pia wanakuwa bado hawana dhambi sana, maana Aliens hupenda siri wanapokuja duniani ndio maana inaonekana hutumwa duniani kwa projects maalumu .

Samahani sana kama nimepangilia hovyo uzi wangu .

Je umeshawahi kuona U.F.O enzi za utoto wako au utu uzima? maana watoto hupata bahati ya kuona vitu vingi vya siri duniani kabla ya kupata akili ya kutambua vizuri vitu na kujiingiza kwenye dhambi" watu na mimi pia naamini Watoto ni malaika" KWA MTU AMBAYE AAMINI MSAADA WA KITABU ICHO ASOME
istockphoto-590147780-612x612.jpg
istockphoto-1054137738-612x612.jpg
 
Attachments

Baada ya kusoma kitabu cha messengers of deception by an UFO investigator Jacques Valley, akielezea uwepo wa viumbe kutoka sayari nyingine baadhi ambazo hazijavumbuliwa wanaokuja mara kwa mara kutembea duniani kujifunza vitu vilivyopo duniani na kuwafunza vitu vipya vilivyopo kwa vinavyohusu vitu mbalimbali kama technology, nimejikuta najua vitu vingi ambavyo watu wengi hawavijui kuhusu dunia na siri zake, baadhi ya vitu ambavyo kitabu kimeelezea kuhusu U.F.O baada ya kuwafanyia interviews baadhi ya observes wa vyombo ambavyo wamewahi kuviona vikipaa angani kutoka sehemu mbalimbali za duniani kama Egypt na America wamesema sifa za hivyo vyombo ni kama zifuatazo

1. Vina umbo la saucers
2. Ndani yake huwa kuna viumbe ambao wamevaa mavazi kama wanayovaa wazamiaji majini
3. Huongea lugha za ajabu zisizoeleweka
4. Baadhi ya watu huwaelekeza vitu vipya vya kufanya
5. Wakimaliza duties zao upaa na chombo ( saucers) huku wakikuacha na mshangao

Kwa nilivyosoma hiyo investigation book kuhusu U.F.O iliyofanyiwa utafiti kwa miaka kadhaa na kwa sample kubwa tu ya watu ambao ni zaidi ya watu 3000 na kwa population zaidi ya 300,000 kwa knowledge yangu nahisi hao viumbe wapo kwenye sayari ambazo wanasayansi bado hawajafanikiwa kuzivumbua, na inasemekana izo U.F.O mara nyingi utokea sehemu zenye vitu vipya na gunduzi nyingi kama Sourthen Calfornia na sehemu nyingi za majangwa kwenye kitabu Jacques ameandika muda ambao hutokea ni kuanzia saa 4 usiku muda ambao watu wengi huwa ndani kwa hiyo watu wachache hupata bahati ya kuona hivyo vyombo vikipaa kwa kasi angani huku vikitoa mwanga mkali,

Kwa maoni yangu na lengo la kuandika uzi huu naomba mwana Jamiiforums kutushirikisha kama umewahi kuona kitu kama U.F.O ili tupate ufahamu kama Africa je huwa tunatembelewa na U.F.O, kwa mimi nimewahi kuona kitu kama U.F.O kikiwa kinaenda kwa kasi usiku kipindi nikiwa na miaka kama 10 na kadhaa, nachohisi huja Africa sana sema NASA na watu wanaodeal na research zihusuzo aliens hawajaamua kuweka kambi Africa, maana nishawahoji baadhi ya watu wazima wanadai katika enzi zao za utoto wanakumbukumbu walishaona U.F.O , Pia nadharia yangu nyingine inaniambia U.F.O hupenda kuwapa bahati watoto kwa sababu maranyingi huwa akili zinakuwa bado na pia wanakuwa bado hawana dhambi sana, maana Aliens hupenda siri wanapokuja duniani ndio maana inaonekana hutumwa duniani kwa projects maalumu .

Samahani sana kama nimepangilia hovyo uzi wangu .

Je umeshawahi kuona U.F.O enzi za utoto wako au utu uzima? maana watoto hupata bahati ya kuona vitu vingi vya siri duniani kabla ya kupata akili ya kutambua vizuri vitu na kujiingiza kwenye dhambi" watu na mimi pia naamini Watoto ni malaika"
View attachment 1438135View attachment 1438136
Kuna tetesi Corona ni Aliens
 
Mkuu share link ya hiko kitabuu na ss tu enjoy the situation
 
Nimevutiwa na namba 4!
Unaweza ukaielezea...??
Wanajaribu kusema nini..?

Uzi wako unazungumzia nadharia,hili sio tatizo ila unataka kuaminisha watu kwa kupitia watoto kuwa ni malaika na wanaona hizo UFO!!... Nawakati huohuo unasema zinaonekana usiku kuanzia saa nne!,Sasa mida hao malaika wako watoto si wanakuwa wamepiga mbonji(wamelala)..

Hilo la watoto nalo naliona nadharia!
Au unataka kutuaminisha kwa kuwa Zimbabwe kulishawahi tokea tukio la watoto kuona UFO na hivyo viumbe..??

Nami ninalo la kusimulia ila kidogo mi ni tomaso! Kuamini vitu kidogo mgumu😅
Hili ni tukio nililoliona mwaka 2006 nilikuwa darasa la 4.. ilikuwa usiku wa saa nane ama saa tisa hivi.. tulikuwa tunatoka kwenye harusi bahati mbaya gari tukiwa tunakaribia kufika nyumbani gari iliishiwa mafuta! Ikabidi tutulie kidogo huku jamaa mwengine akielekea kufata mafuta.. Sasa wakati tukisubiri ghafla tu tulishangaa mwanga mkali wa kijani ulimulika lile eneo utafikiri ka mchana fulani hivi!!
Kuangalia juu tuliona hicho kilichokuwa kikitoa mwanga kikielekea juu kwa kasi!!
Sijui ilikuwa ni nini ile mpaka leo,nimejaribu kufatilia lkn jibu sikuwahi kulipata lkn ile hali ilileta mshtuko maana ilikuwa ghafla na wengine walikuwa wameshuka kwenye gari walirudi fasta😂😅

Hili tukio lilinitatiza maana sikuelewa kilikuwa ni nini kile ila hii hainifanyi mimi kuamini kuwa ni UFO ila nitaita UFO kwasababu kwetu tuliokuwa pale tulikuwa hatujui ni nini!!
Wengine walisema ni satellite lkn lini tz tumerusha satellite sisi..? Tena mwaka 2006.. labda nitaje na eneo husika kabisa ili kama Kuna mtu pia alishuhudia tuweze kushea,Eneo ilikuwa ni Mwanza maeneo ya ghana ndipo tukio lilipojiri.
 
Hii mpya,labda tuanze na ww huwa wanafanyj wanazunguka tuu na kugeuza?au kuna zawadi walikupa? Wanapenda mapori au majengo wanapotua au sehm wazi? Kuna wenyeji wao au wao tu hujifanyia mishe zao na kwenda?
 
UFO ku-exist haimaanishi kuna ulazima wa viumbe wa sayari nyengine kuja duniani.

Unafahamu kuwa Avro Canada Canadian aircraft manufacturing company mwaka 1953 ilitoa siri kuwa walikuwa wanatengeneza flying vehicle? Kwenye kuielezea walisema ni circular jet aircraft ambayo yenye uwezo wa kukimbia kwa mwendokasi wa 1,500 mph (2,400km/h).

Baada ya hiyo kampuni kuzungumza hivyo Bw.Georg Klein ambaye ni German engineer alisema hiyo kampuni haitengenezi kitu chochote kipya bali kiuhalisiya wana copy and engineering UFOs that were developed during Nazi Germany.

Flying saucer zilianza kuonekana miaka ya mwishoni ya ww2 ambapo meli za jeshi la US na Soviet kama sijakosea walienda bara Antarctica ambapo kulikuwa na base nyengine ya siri ya kijeshi ya Nazi ambapo walishambuliwa na hizo flying saucer. Tena kilikuwa na uwezo wa kuzama majini na kupaa kwa kasi kuliko ndege vita ya kipindi hicho. Hitler alikuwa yupo mbali kiteknolojia ndiyo maana US na Soviet walikuwa wakipigania kuwapata scientis wa Hitler. Hiyo documentary inayooyesha hizo saucer zikishambulia meli nilikuwa nayo video za black and white ila sasa hivi sina.

Hii ni nyaraka ya CIA kuhusu flying saucer.
Screenshot_20200503-144239.png

Inshort CIA hii ajenda wameibeba kupotosha watu kwa nia nzuri ya wao kutengeneza vifaa vita vya ajabu vya siri na kuvifanyia majaribisho. Kwa vile ni kifaa kilicho na muundo tofauti na watu walichokizoea kitakuwa tu Unidentied Flying Object. Hakuna cha Alien! Watu wanakamilisha mipango yao tu.
 
Are we alone? Huwa nikitazama nyota zilivyo nyingi angani wakati wa usiku wa giza nene huwa siamini kama tupo peke yetu.

#Sijawahi kuona UFO
Nachoamini mkuu hatupo peke yetu mana kuna sayari kibao ambazo wanasayansi bado hawajazivumbua
 
UFO ku-exist haimaanishi kuna ulazima wa viumbe wa sayari nyengine kuja duniani.

Unafahamu kuwa Avro Canada Canadian aircraft manufacturing company mwaka 1953 ilitoa siri kuwa walikuwa wanatengeneza flying vehicle? Kwenye kuielezea walisema ni circular jet aircraft ambayo yenye uwezo wa kukimbia kwa mwendokasi wa 1,500 mph (2,400km/h).

Baada ya hiyo kampuni kuzungumza hivyo Bw.Georg Klein ambaye ni German engineer alisema hiyo kampuni haitengenezi kitu chochote kipya bali kiuhalisiya wana copy and engineering UFOs that were developed during Nazi Germany.

Flying saucer zilianza kuonekana miaka ya mwishoni ya ww2 ambapo meli za jeshi la US na Soviet kama sijakosea walienda bara Antarctica ambapo kulikuwa na base nyengine ya siri ya kijeshi ya Nazi ambapo walishambuliwa na hizo flying saucer. Tena kilikuwa na uwezo wa kuzama majini na kupaa kwa kasi kuliko ndege vita ya kipindi hicho. Hitler alikuwa yupo mbali kiteknolojia ndiyo maana US na Soviet walikuwa wakipigania kuwapata scientis wa Hitler. Hiyo documentary inayooyesha hizo saucer zikishambulia meli nilikuwa nayo video za black and white ila sasa hivi sina.

Hii ni nyaraka ya CIA kuhusu flying saucer.
View attachment 1438725

Inshort CIA hii ajenda wameibeba kupotosha watu kwa nia nzuri ya wao kutengeneza vifaa vita vya ajabu vya siri na kuvifanyia majaribisho. Kwa vile ni kifaa kilicho na muundo tofauti na watu walichokizoea kitakuwa tu Unidentied Flying Object. Hakuna cha Alien! Watu wanakamilisha mipango yao tu.
Hapana mkuu katafute kitabu kinachoitwa the messengers of deception by jacques valley , ningekuwa na softcopy ningewatumia lakini nina hardcopy tu.softcopy inauzwa amazon ni investigative book ambayo imefanyiwa research kwa interviews mbalimbali kwa mashuhuda waliowahi kuziona U.F.O pia kushilikishwa vitu na aliens kutoka nchi mbalimbali na ni watu na akili zao na proffessionalism zao.
 
Hii mpya,labda tuanze na ww huwa wanafanyj wanazunguka tuu na kugeuza?au kuna zawadi walikupa? Wanapenda mapori au majengo wanapotua au sehm wazi? Kuna wenyeji wao au wao tu hujifanyia mishe zao na kwenda?
Huwa wanakuja duniani kwa missions maalumu ni kama messengers huja kujifunza vitu vipya duniani na kuwapa vitu vipya binadamu, hupenda sehemu ambazo watajifunza vitu vipya na kwenye deserts na kuna tetesi marekani kuna eneo wametengewa ili kuwavutia lipo kama kumbukumbu zangu zinaniambia san Diego,California,linaitwa Area 51
 
Hao UFO ni waoga sana.
Yah aliens nahisi hufanya vitu vyao kwa siri na mpaka uione flight yao ni mpaka wakuselect, na ni bahati ukifanikiwa kuwaona hata maisha yako nahisi yatakuwa ya tofauti sana
 
Nimevutiwa na namba 4!
Unaweza ukaielezea...??
Wanajaribu kusema nini..?

Uzi wako unazungumzia nadharia,hili sio tatizo ila unataka kuaminisha watu kwa kupitia watoto kuwa ni malaika na wanaona hizo UFO!!... Nawakati huohuo unasema zinaonekana usiku kuanzia saa nne!,Sasa mida hao malaika wako watoto si wanakuwa wamepiga mbonji(wamelala)..

Hilo la watoto nalo naliona nadharia!
Au unataka kutuaminisha kwa kuwa Zimbabwe kulishawahi tokea tukio la watoto kuona UFO na hivyo viumbe..??

Nami ninalo la kusimulia ila kidogo mi ni tomaso! Kuamini vitu kidogo mgumu😅
Hili ni tukio nililoliona mwaka 2006 nilikuwa darasa la 4.. ilikuwa usiku wa saa nane ama saa tisa hivi.. tulikuwa tunatoka kwenye harusi bahati mbaya gari tukiwa tunakaribia kufika nyumbani gari iliishiwa mafuta! Ikabidi tutulie kidogo huku jamaa mwengine akielekea kufata mafuta.. Sasa wakati tukisubiri ghafla tu tulishangaa mwanga mkali wa kijani ulimulika lile eneo utafikiri ka mchana fulani hivi!!
Kuangalia juu tuliona hicho kilichokuwa kikitoa mwanga kikielekea juu kwa kasi!!
Sijui ilikuwa ni nini ile mpaka leo,nimejaribu kufatilia lkn jibu sikuwahi kulipata lkn ile hali ilileta mshtuko maana ilikuwa ghafla na wengine walikuwa wameshuka kwenye gari walirudi fasta😂😅

Hili tukio lilinitatiza maana sikuelewa kilikuwa ni nini kile ila hii hainifanyi mimi kuamini kuwa ni UFO ila nitaita UFO kwasababu kwetu tuliokuwa pale tulikuwa hatujui ni nini!!
Wengine walisema ni satellite lkn lini tz tumerusha satellite sisi..? Tena mwaka 2006.. labda nitaje na eneo husika kabisa ili kama Kuna mtu pia alishuhudia tuweze kushea,Eneo ilikuwa ni Mwanza maeneo ya ghana ndipo tukio lilipojiri.
Mkuu namba nne kuna witnesses kadhaa walitokewa na izo U.F.O kisha kuingizwa ndani na kupewa technology za kutengeneza vitu ambavyo ni bora kuliko vilivtopo duniani kwa mfano mmoja walimwelekeza jinsi ya kutengeneza motor bora zaidi ,.
Pili, kuhusu watoto sometimes hutokea maramoja moja kutoka nje wakati wa usiku na kujaaliwa bahati ya kuviona hali kadhalika watu wazima, nakumbuka mimi niliiona Saucer kwa bahati na sikuwa na mtu mwingine nikabaki nashangaa ,
 
Back
Top Bottom