Watoto kukaa kwenye gari huku wazee wamesimama haifai

Watu wanataka kusema utamaduni wa ulaya na afrika ni sawa.
Mkuu japo tamaduni zetu hazifanani ila kuna vitu vya msingi ambavyo vinaingiliana na inatakiwa tuvipe vipaombele, maana kwenye jamii makundi yote ni muhimu na siya kudumu kama unavyojua kwenye maswala ya ukuaji wa binadamu na lazima hatua hizo tupitie, ni muhimu kuweka mambo sawa ila kila tunapoingia hatua hiyo kuwa imeandaliwa vyema
 
Mkuu japo tamaduni zetu hazifanani ila kuna vitu vya msingi ambavyo vinaingiliana na inatakiwa tuvipe vipaombele, maana kwenye jamii makundi yote ni muhimu na siya kudumu kama unavyojua kwenye maswala ya ukuaji wa binadamu na lazima hatua hizo tupitie, ni muhimu kuweka mambo sawa ila kila tunapoingia hatua hiyo kuwa imeandaliwa vyema

Umesema vema.
 
Hakuna mtu anayelazimisha mtoto ampishe na siwahi kuona, jambo jema ni kufikiria saikolojia ya mtoto ilivyo, yaani anajisikiaje yeye akiwa amekaa huku mzee sawa na babu au bibi yake amesimama.

kisaikolojia mtoto naye anaweza kuona anaonewa. Mtoto, mzee, mgonjwa, mjamzito na mlemavu ni watu walioko kwenye kundi maalum linalohitaji uangalizi wa ziada kutoka kwa jamii. Hizi daladala zetu zinavyojaa mtoto unamuweka katika hali gani kubanwa banwa, mara hana balance. Kwanza nilifikiri utawatetea wakae kwenye siti na kuwaasa watu wazima wawajali, ikiwa ni pamoja na kupunguza matusi kwenye daladala. Vijana ndo wasimame wapishe wazee, wenye afya wawapishe wagonjwa, wakubwa wawapishe watoto. Sisi wakubwa tukifanya mambo sahihi watoto wataiga. Tukiwajali watoto nao watatujali. Mtoto anaanza wapi kumheshimu mzee wakati huyo mzee hawezi hata kumtetea anaponyanyaswa na konda?
 
mi sikubaliani kwamba eti kumpisha mtu siti ni heshima. kwanza hao wazee unampisha hana hata ahsante. bora nikae tu hata kama mwanangu akae tu na yy atakaa baadae watu wakishuka. kama maadili na wao wajifunze kuwa na shukrani labda tutafika mbali.

na alosema eti tunaiga wazungu si kweli. kwa wenzetu ukipanda public transport kuna siti za mwanzo zimeandikwa kabisa kama ikitokea kapanda mtu mwenye special needs ni lazima kumpisha. labda waanze utaratibu huo na huku
 
miaka ya nyuma wakati nipo form three 2001 nilipanda daladala kurudi home nikiwa naumwa sana. nimekaa mda mrefu ndo ikawa imejaa iondoke. wakati tunataka kuondoka akaja mzee mmoja konda akaniambia mpishe. nikampisha ila nikashuka nikapanda gari nyingine kwa kuwa sikua na hali ya kusimama na kuanza kungoja upya. na mitaa yetu gari inachukua hata one hour kujaa. na mtu hata hana shukrani. kweli hiyo haki kumpisha mtu kisa kaenda age. watoto wao wenyewe hawapishi wazazi wetu kwenye magari. i dnt care no more
 
Taxi zipo ualipa 3,000/=
viBaby Walker vipo viauzwa 3,000,000/ lita moja 18km
Mimi km namsafirisha Bint yangu wa 5yrs kwenda Dar kwa Shangazi yake namchukulia siti yake kwenye Shabiby na namuagiza Konda asinyanyuliwe
Watoto waacheni wajinafasi km Daladala imejaa ipo nyingine
Swadakta..
 
anayewahi seat anakaa... period, hiyo haina exception na haimuharibu mtoto wala nini... uzembe wako kupanda bac mtoto ndo aulipe, kwanza mzee mzima unastahili kufanya mazoezi kuweka mwili safi
 
Nyie ndo mnaanzaga kula kabla ya watoto. yaani nimuche mtoto wangu 8 years asimame, mimi nikae. no noo....
 
Anaruhusiwa kukaa na ni jambo jema mtoto naye akakaa kwenye kiti lakini heshima ni jambo jema, hapa namaanisha mzazi anamlipia kiti mtoto huku mzee amesimama, kwanini asimpakate au kumwambia mkubwa akae kwenye siti na kumpakata mtoto? heshima haiendi na wakati mkuu.

Huyo mzee wakati anapanda aliona gari imejaa na akapanda hivyo hivyo..meaning alikuwa tayari kusimama, otherwise angesubiri gari nyingine.

Mtu akiwa tayari kumpisha mwingine kiti ndani ya gari either kwasababu ni mzee au ana mtoto ni vizuri lakini SIO LAZIMA.
 
Wakati mwingine mnawaonea sana watoto. Na wao ni binadamu, wanachoka sana wakati mwingine, au utakuta anaumwa lakini hasemi. Utakuta lijitu lina minguvu yake vizuri tu hlf linataka mtoto ampishe seat. Kuna heshima sawa lakini isiwe mazoea, km gari imejaa shuka upande lingine. Mi nikipanda daladala na mwanangu ht km ana miaka miwili namlipia seat na ole wako uniambie nimpakate!
 
samahani na wewe ulikuwa na siti au umesimama, mm Konda angerudisha Nauli kwani mtoto ana haki zote, Kupendwa matibabu na Uhuru wa kujieleza


sawa lkn km na mm nipo ndani ya Daladala kweli HUMPAKATI Mwanangu ntampakata mwenyewe
Hii Mkuu ilishanitokea mata nyingi, Binti wangu wa miaka 3 tulikaa naye siti ya watu wa2 nikampakata nikiwa na jaa mwingine na kwa vile dirishani kwenye daladala ilibidi mm nisimame mtoto akae ili aridhike
Safari zenyewe za Town hata dk 10 haziishi acheni watoto wakae waliokosa wasubiri usafiri mwingine lkn km ni Mwanafunzi nakubai ni kijana asimame tu na kupisha Wajawazito na vikongwe
Na mtu kuwa mjamzito sio adhabu matokeo ya furaha ya kuolewa sasa apishwe nn
 
Huu ni muda wa kuangalia pande zote mbili na si kusema adabu ya mtoto haipo, huo ni utamaduni tulioukuta miaka ile, ukute miaka hiyo hakukuwa na purukushani za madaladala kama za huku Dar, kwanza kipindi iko waende wapi wakati kazi zao ni kushika majembe na gesti za kina babu @Aspirin zilikua vichakani!!!!!
My point ni kwamba, mtoto mdogo anaposimama ndani ya daladala, wengi unawakuta ni wadogo, hata wakubwa kuwasaidia kuwapakata wanaona tabu, naomba mtoa mada unijibu ili swali kabla sijaendelea, ivi adabu ni kwa wakubwa tu ama hata watoto wanapaswa kuheshimiwa na wakubwa?
 
Tatizo hili liko katika nyanja mbali mbali na ni ngumu kulibadili. Hivi umewahi kujiuliza inakuwaje mwalimu afundishe amesimama na watoto/wanafunzi wamekaa tena wengine wakisinzia, wanafundishwa tabia gani?

Nawasilisha

Siku zote mwanamke ndiye mlezi wa kwanza wa mtoto. Hii maana yake ni kwamba mtoto mdogo mara nyingi anashinda na mama yake na ndiye anayetegemewa kumfundisha mtoto kipi chema na kipi kibaya ili aweze kujua kutokana na ugeni wake na uchanga wa ubongo wake.

Lakini cha wamama hawafanyi hivyo badala yake wanamuacha mtoto apambane na mazingira mageni kwake! nimeshudia wazazi wanawalipia siti watoto wao huku wazee wakisimama, mtoto unategemea ajifunze nini hapo?
 
kams sio sheria haina haja ya kupoteza mda hapa lkujadili.ni huruma na moral ya mtu ndio itakayoamua
 
hao wazee si wasubiri daladala zenye siti
tena kuna wengine wana makusudi anaona daladala limejaa nae huyo


Inakera sana! Tena unakuta mzee mzima anapanda daladala iliyojaa mwanzo wa safari! Na mijitu inarundikana hadi unashangaa. Yaani kama ingeshuka ni wazi wangejaza daladala inayofuata.

Kuna siku mzee kapanda katika daladala imejaa dogo kakaa katika siti, jamaa mwingine akumuwakia "dogo huoni wakubwa". Dogo akasema "Kuna daladala imeondoka nimeiacha. Ningepanda ningekuwa nimesimama peke yangu"
Jamaa akapiga kimya ila dogo alimpisha yule mzee.
Nililipenda tu lile jibu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom