Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Siku hizi Wana mtindo mmoja ukihitaji kubadilisha wanakuletea mtungi wa gesi mpaka unapoishi na ni free of charge ww ni kupiga simu tu sasa hapo lazima Kuna upigaji tu.

Naomba kufaamishwa vizur unajuaje mtungi wa gesi kwamba umechakachuliwa?
pima na mzani wako usiamini mzani wowote hata wa dukani usiuamini
 
R
Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa gesi ya Taifa Gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wiki 4 zilizopita nilienda dukani kununua gesi [kubadilisha mtungi]. Wakati nauinua nikasikia kimiminika [gesi] ikicheza ndani kwa ombwe kubwa.

Kwa kuwa mwenye duka anao mzani [nilimshauri hivyo kufuatia agizo la serikali kuwa wauzaji wa gesib lazima waweke mizani ili wateja wahakiki ujazo] ilibidi niupime pale pale. Huwezi kuamini, kulikuwa na upungufu wa gm 950, yaani karibu kilo nzima! Akanipa mtungi mwingine, nao ukawa umepungua pia! Mtungi wa tatu ndio ukawa sawa.

Wiki iliyopita gesi ikawa imeisha, kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutosha ikabidi nichukue mtungi mdogo kabisa, na kwa kuwa imani yangu kwa Taifa Gas ilikuwa imepungua nikaamua kuupima. Amini usiamimini, nao ukawa umepungua! Nikachukua mtungi mwingine, nao ukawa umepungua vilevile hadi nilipopata mtungi wenye uzito sahihi.

Kwa uzoefu huu nawafahamisha wateja wenzangu wa Taifa Gas kuwa makini wanapobadilisha mitungi hiyo. Wito wangu kwa Taifa Gas ni kuwa watutendee haki wateja wao, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.

Vv
Rostam ni fisadi papa
 
Mmmh hapa sio uzi wa afisa masoko kweli..sababu hawa taifa wanakimbiza
 
Mimi nimeshapata changamoto mara mbili kwenye mitungi yao unauchukua unahakiki ujazo alafu ukifika home unakuta hakuna raba kwene sehemu yabkutolea ambapo ndio unapachika kile ki reguleta sasa najiuliza wanajaza na kuhakiki kabla ya kuweka ile seal yao ila kunakua na mapungufu kivipi au ndio janja janja zinazoweza leta madhara
Unaweza n janja ya mwenye duka akiiba kg moja au nusu kg kwa mitungi 20 anapata mtungi mmoja extra na kuhamisha gas kutoka mtungi mmoja kwenda mwingine n simple tu
 
Tu kumbe tena!? Mimi pia natumia taifa gas japo situmii sana maana ubize mwingi.
Unapenda anasa sana. Acha kuendekeza anasa kwa kutumia gesi. Mbona babu zako hawakutumia gesi na maisha yalienda tu tena walikuwa na furaha kukuliko.
 
Unaweza n janja ya mwenye duka akiiba kg moja au nusu kg kwa mitungi 20 anapata mtungi mmoja extra na kuhamisha gas kutoka mtungi mmoja kwenda mwingine n simple tu
Na zile seal za taifa pia anakua nazo au
 
Yuko sahihi, Mitungi ya taifa gas wabadilike.
Wafanye suprise cheki kwenye wauzaji wao
Humu Jamii Forums wachukue kuwa lalamiiko limefika wachukue hatua

Yaweza kuwa agents ndio wanafanya huo.mchezo bila wao kujua
 
Hauna conflict of interest kweli mleta mada kwenye Biashara hii?
===
Hii ni tuhuma nzito, na unampaka kazi nzito Meneja masomo wa Taifa gesi. Kubwa kabisa, hii tuhuma ilitakiwa iambatane na ushahidi usiotiliwa shaka.kwa kueleza, ulinunua mitungi hiyo kwa duka la nani, mtaa gani, wilayagani. Pia ungeweka na ushindi wa picha ama video wakati unafanyia matukio yote haya.

Tujiepushe kutoa taarifa bila ushahidi. Na tuache kugombanisha makampuni. Suala la kuitaja Oryx gas moja kwa moja kwa mlengo huu katika uzi huu inaonyesha Nia ovu uliyonayo dhidi ya makampuni haya.
Nia yangu ni kuwafungua macho watumiaji wenzangu wa Taifa Gas na kuwasaidia wahusika wafanyie kazi na kurekebisha kasoro hiyo.
Mimi bado natumia Taifa Gas lakini lazima niupime na kuuchukua mtungi uliotimia.

Mwisho, hili ni rahisi sana kufuatilia, nenda duka lolote wanalouza gesi ya mtungi, chukua mitungi mitatu ya Taifa Gas na upime. Utajionea.

Vv
 
Siku hizi Wana mtindo mmoja ukihitaji kubadilisha wanakuletea mtungi wa gesi mpaka unapoishi na ni free of charge ww ni kupiga simu tu sasa hapo lazima Kuna upigaji tu.

Naomba kufaamishwa vizur unajuaje mtungi wa gesi kwamba umechakachuliwa?
Muuzaji anatakiwa kuwa na mzani wa kidigitali wa kupimia [ni agizo la serikali]. Kila mtungi juu pembeni umeandikwa ujazo wake, unapopima lazima uzito wa mtungi pamoja na gesi usome sawa na maandishi yaliyopo kwenye mtungi.

Vv
 
Nia yangu ni kuwafungua macho watumiaji wenzangu wa Taifa Gas na kuwasaidia wahusika wafanyie kazi na kurekebisha kasoro hiyo.
Mimi bado natumia Taifa Gas lakini lazima niupime na kuuchukua mtungi uliotimia.

Mwisho, hili ni rahisi sana kufuatilia, nenda duka lolote wanalouza gesi ya mtungi, chukua mitungi mitatu ya Taifa Gas na upime. Utajionea.

Vv
Ili kuwasaidia wengine.
  • Mtungi mdogo unatakiwa uwe kg ngapi?
  • Mtungi wa kati unatakiwa uwe kg ngapi?
  • Mtungi mkubwa unatakiwa uwe na kg ngapi?
 
Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa gesi ya Taifa Gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wiki 4 zilizopita nilienda dukani kununua gesi [kubadilisha mtungi]. Wakati nauinua nikasikia kimiminika [gesi] ikicheza ndani kwa ombwe kubwa.

Kwa kuwa mwenye duka anao mzani [nilimshauri hivyo kufuatia agizo la serikali kuwa wauzaji wa gesib lazima waweke mizani ili wateja wahakiki ujazo] ilibidi niupime pale pale. Huwezi kuamini, kulikuwa na upungufu wa gm 950, yaani karibu kilo nzima! Akanipa mtungi mwingine, nao ukawa umepungua pia! Mtungi wa tatu ndio ukawa sawa.

Wiki iliyopita gesi ikawa imeisha, kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutosha ikabidi nichukue mtungi mdogo kabisa, na kwa kuwa imani yangu kwa Taifa Gas ilikuwa imepungua nikaamua kuupima. Amini usiamimini, nao ukawa umepungua! Nikachukua mtungi mwingine, nao ukawa umepungua vilevile hadi nilipopata mtungi wenye uzito sahihi.

Kwa uzoefu huu nawafahamisha wateja wenzangu wa Taifa Gas kuwa makini wanapobadilisha mitungi hiyo. Wito wangu kwa Taifa Gas ni kuwa watutendee haki wateja wao, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.

Vv
Mkuu sio gesi tu, nakuomba uwe makini na vitu vyote vyenye mkono wa serikali kuanzia shule hospitali, maji nk. Kwa mfano, maji yanayotoka kwenye bomba la DAWASA sio salama kuyannywa moja kwa moja bila kuchemsha....yatakuja kukuua usipokuwa makini.

Shule na hospitali za umma nazo ni matatizo kwa kwenda mbele. Sina haja ya kueleza zaidi wala kuweka picha kwani kila mtu anafahamu hili. Kuweni makini na vitu vya serikali vitakuja kuwaua bure!
 
Muuzaji anatakiwa kuwa na mzani wa kidigitali wa kupimia [ni agizo la serikali]. Kila mtungi juu pembeni umeandikwa ujazo wake, unapopima lazima uzito wa mtungi pamoja na gesi usome sawa na maandishi yaliyopo kwenye mtungi.

Vv
Ni kweli kabisa mkuu lakini wananchi wengi hawazingatii hili. Tunapigwa mno!
 
Mkuu sio gesi tu, nakuomba uwe makini na vitu vyote vyenye mkono wa serikali kuanzia shule hospitali, maji nk. Kwa mfano, maji yanayotoka kwenye bomba la DAWASA sio salama kuyannywa moja kwa moja bila kuchemsha....yatakuja kukuua usipokuwa makini.

Shule na hospitali za umma nazo ni matatizo kwa kwenda mbele. Sina haja ya kueleza zaidi wala kuweka picha kwani kila mtu anafahamu hili. Kuweni makini na vitu vya serikali vitakuja kuwaua bure!
Hii nchi hatuaminiani kabisa
 
Back
Top Bottom