Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Wateja wa Taifa Gas tuwe makini

Itakua ni kweli kuna siku wife kamtuma mtu akachue gas ila akamwambia kwamba usinunue kwa " muha nunua kwa mangi sio majina halisi ya wahusika.

Nikamuliza kwann akasema hapo kwa muha inaisha haraka nikambishia na kumwambia una sababu zingine binafs kumbe kweli mambo haya yapo!!

Xmcha ajabu ni kwamba hawa wanauza huku mtaan hawana hiyo mizani unayosema
Hapa ninaponunu ni home boy wangu, niliposikia agizo la serikali kuwataka wauza gesi waweke mizani ya kupimia nilimtahadharisha na akalifanyia kazi.

Vv
 
Mkuu sijapinga wazo, bali nimekataa packaging ya wazo kwa namna lilivyoletwa hapa jukwaani. Yaani wazo limetetwa likiwa na mapungufu ya ushahidi. Na ushahidi ni jambo muhimu Sana katika kutafuta suluhisho la changamoto inayojitokeza popote!

Binafsi naona ni jambo jema sana kuleta tuhuma hizi zikiwa na ushahidi timilifu ili tuhuma hii ifanyiwe kazi na wahusika au Mamlaka husika (Weight and Measures Authority).
Alete ushahidi gani wakati ni wengi wanalalamikia huu wizi? Mamlaka husika ndizo zenye jukumu la kufuatailia na kupata ushahidi. Hata mwenye kampuni anatakiwa afuatilie na siyo mteja. Kama anasubiri apelekewe ushahidi aendelee kusubiri tu lakini ajue wateja atawapoteza.
 
Hauna conflict of interest kweli mleta mada kwenye Biashara hii?
===
Hii ni tuhuma nzito, na unampaka kazi nzito Meneja masomo wa Taifa gesi. Kubwa kabisa, hii tuhuma ilitakiwa iambatane na ushahidi usiotiliwa shaka.kwa kueleza, ulinunua mitungi hiyo kwa duka la nani, mtaa gani, wilayagani. Pia ungeweka na ushindi wa picha ama video wakati unafanyia matukio yote haya.

Tujiepushe kutoa taarifa bila ushahidi. Na tuache kugombanisha makampuni. Suala la kuitaja Oryx gas moja kwa moja kwa mlengo huu katika uzi huu inaonyesha Nia ovu uliyonayo dhidi ya makampuni haya.

Yeye kahimiza watu watumie mizani wakati wanainunua. Hamna conflict of interest hapo. Wewe yule au mm tunaweza thibitisha asemacho popote tulipo kwa kutumia mzani kwa kila nunuzi
 
TBS na Watu wa taasisi ya vipimo na mizani waingie kazini haraka

Waende na mizani yao kila kona ya nchi kwa kuvamia maduka ghafla wapime
Yaani wamdhibiti mfuasi, mwanamikakati na mfadhili wa CCM? Mmiliki ana wajibu wa kimaadili kwa wateja wake, atimize wajibu vinginevyo tutamkimbia na kampuni itakufa.

Vv
 
Mkuu sijapinga wazo, bali nimekataa packaging ya wazo kwa namna lilivyoletwa hapa jukwaani. Yaani wazo limetetwa likiwa na mapungufu ya ushahidi. Na ushahidi ni jambo muhimu Sana katika kutafuta suluhisho la changamoto inayojitokeza popote!

Binafsi naona ni jambo jema sana kuleta tuhuma hizi zikiwa na ushahidi timilifu ili tuhuma hii ifanyiwe kazi na wahusika au Mamlaka husika (Weight and Measures Authority).
Mkuu mbona nimeleta ushahidi kuwa ninatumia, nimefanya utafiti na nimeshapima mara kadhaa? Unataka nikuletee ushahidi nyumbani kwako? Wewe unayepinga ushahidi wangu una jukumu la kukanusha kwa kufanya utafiti pia. Nenda kwa muuzaji na chukua mitungi mitatu uipime uone kama tuhuma zangu ni uongo.

BTW bado natumia Taifa Gas, nachofanya ni lazima niipime na kuchukua mtungi wenye ujazo sahihi.

Vv
 
.... NDIYO HABARI YA MJINI. KATAA UTAPELI WA .....
Ninachokiona hapa nimeisha kieleza lakini hutaki kukuelewa.

Umetoa mfano wa ufisadi. Kama Kuna ufisadi mahali; ninachojua hatua zinachukuliwa ni mtuhumiwa ama kusimamishwa kazi na wakuu wake wa kazi ili uchunguzi ufanyike ( uchunguzi wa kupata ushahidi, msisitizo ushahidi)ama ukamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande kisha polisi ukusanya ushahidi; ushahidi ukitimia mtuhumiwa upelekwa Mahakamani kwa mashtaka.

Vivyo hivyo, na kwa yule aliyesimamishwa kupisha uchunguzi ripoti ya uchunguzi ikitoka na ikawa na ushahidi wa kutosha basi upelekwa Mahakamani kwa mashtaka.

Sasa mkanganyiko wa ninyi Wakuu kukataa kutoa ushahidi ili hawa wahujumu wateja kwenye huduma mnautoa wapi???

Umenipata lakini, Mkuu.
 
Siku hizi Wana mtindo mmoja ukihitaji kubadilisha wanakuletea mtungi wa gesi mpaka unapoishi na ni free of charge ww ni kupiga simu tu sasa hapo lazima Kuna upigaji tu.

Naomba kufaamishwa vizur unajuaje mtungi wa gesi kwamba umechakachuliwa?
Hii mbinu ni nzuri sana.
 
Yeye kahimiza watu watumie mizani wakati wanainunua. Hamna conflict of interest hapo. Wewe yule au mm tunaweza thibitisha asemacho popote tulipo kwa kutumia mzani kwa kila nunuzi
Asante sana mkuu, wewe umesoma vizuri kwa utuo na kituo, hujakurupuka kunijibu.

Vv
 
Mamlaka husika ndizo zenye jukumu la kufuatailia na kupata ushahidi.
Unajua Mkuu nipo upande wako sema haujanipata. Yaani hapa, kama tumedhamilia kuondoa hujuma hii dhidi ya haki ya Huduma kwa mTeja, tunatakiwa kutoa ushahidi usiotiliwa shaka wa uwepo wa hujuma hii ikiwezekana kwa Mamlaka ama mtoa huduma ili hujuma hii ikomeshwe.

Mamlaka, ndiyo ni wajibu wake, lakini kwa nini tujicheleweshe kisubiri Mamlaka ijekukusanya ushindi yenyewe wakati sisi tunaweza kufanya kazi hii kwa haraka?

Nadhani hapa umenielewa.
 
Mkuu mbona nimeleta ushahidi kuwa ninatumia, nimefanya utafiti na nimeshapima mara kadhaa? Unataka nikuletee ushahidi nyumbani kwako? Wewe unayepinga ushahidi wangu una jukumu la kukanusha kwa kufanya utafiti pia. Nenda kwa muuzaji na chukua mitungi mitatu uipime uone kama tuhuma zangu ni uongo.

BTW bado natumia Taifa Gas, nachofanya ni lazima niipime na kuchukua mtungi wenye ujazo sahihi.

Vv
Kuna mawili, ama uandishi wangu mbovu, ama umesoma bandiko langu kwa hasira baada ya kusoma Aya ya kwanza ya bandiko inayohoji kama una mgongano wa kimaslahi katika Biashara hii ya gesi.

Kama utatulia, ukasoma vizuri bandiko langu, endapo tu ulilisoma kwa hasira mara ya kwanza, basi utapata maelezo ya kutosha juu ya ni ushahidi wa namna gani nimependekeza uulete hapa jukwaani.

Asante Jioni njema.
 
Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa gesi ya Taifa Gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wiki 4 zilizopita nilienda dukani kununua gesi [kubadilisha mtungi]. Wakati nauinua nikasikia kimiminika [gesi] ikicheza ndani kwa ombwe kubwa.

Kwa kuwa mwenye duka anao mzani [nilimshauri hivyo kufuatia agizo la serikali kuwa wauzaji wa gesib lazima waweke mizani ili wateja wahakiki ujazo] ilibidi niupime pale pale. Huwezi kuamini, kulikuwa na upungufu wa gm 950, yaani karibu kilo nzima! Akanipa mtungi mwingine, nao ukawa umepungua pia! Mtungi wa tatu ndio ukawa sawa.

Wiki iliyopita gesi ikawa imeisha, kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutosha ikabidi nichukue mtungi mdogo kabisa, na kwa kuwa imani yangu kwa Taifa Gas ilikuwa imepungua nikaamua kuupima. Amini usiamimini, nao ukawa umepungua! Nikachukua mtungi mwingine, nao ukawa umepungua vilevile hadi nilipopata mtungi wenye uzito sahihi.

Kwa uzoefu huu nawafahamisha wateja wenzangu wa Taifa Gas kuwa makini wanapobadilisha mitungi hiyo. Wito wangu kwa Taifa Gas ni kuwa watutendee haki wateja wao, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.

Vv
Tutumie oryx tu kwa kweli
 
Hauna conflict of interest kweli mleta mada kwenye Biashara hii?
===
Hii ni tuhuma nzito, na unampaka kazi nzito Meneja masomo wa Taifa gesi. Kubwa kabisa, hii tuhuma ilitakiwa iambatane na ushahidi usiotiliwa shaka.kwa kueleza, ulinunua mitungi hiyo kwa duka la nani, mtaa gani, wilayagani. Pia ungeweka na ushindi wa picha ama video wakati unafanyia matukio yote haya.

Tujiepushe kutoa taarifa bila ushahidi. Na tuache kugombanisha makampuni. Suala la kuitaja Oryx gas moja kwa moja kwa mlengo huu katika uzi huu inaonyesha Nia ovu uliyonayo dhidi ya makampuni haya.

Taifa gas ni wahuni
 
Kampuni zote Zina ubabaifu nakumbuka nlikuwa natumia Mihan gas mara ya kwanza ikawa inadumu ila kadiri siku zinavyoenda siku zikawa zinapungua ! Nikamwambia wife hizi gesi watakuwa hawaweki kilo SAHIHI
 
Kwa hio unashaurije 🤔
Kampuni gani hii nchi haifanyi uhuni ? Tunaenda nao hivo hivo ila hata wew

Am sure ulikoajiriwa/jiajiri unafanyia watu uhuni,

Nchi hii kila mtu muhuni sema tunaenda hivo hivo, hakuna malaika kabisa, tumpe nafasi Rostam, licha ya uhuni ila anasaidia, Voda ipo nchi nzima inapata mawasiliano kwa ajiili ya kazi yake kubwa, saizi tigo pia kwa ajiili yake, uhuni upo ila tunavumiliana na kukosoana tupatapo nafasi

Acha hizo , hutaki watu waongee kisa kila mtu muhuni?
 
Mimi ni miongoni mwa watumiaji wa gesi ya Taifa Gas kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Wiki 4 zilizopita nilienda dukani kununua gesi [kubadilisha mtungi]. Wakati nauinua nikasikia kimiminika [gesi] ikicheza ndani kwa ombwe kubwa.

Kwa kuwa mwenye duka anao mzani [nilimshauri hivyo kufuatia agizo la serikali kuwa wauzaji wa gesib lazima waweke mizani ili wateja wahakiki ujazo] ilibidi niupime pale pale. Huwezi kuamini, kulikuwa na upungufu wa gm 950, yaani karibu kilo nzima! Akanipa mtungi mwingine, nao ukawa umepungua pia! Mtungi wa tatu ndio ukawa sawa.

Wiki iliyopita gesi ikawa imeisha, kwa kuwa sikuwa na pesa ya kutosha ikabidi nichukue mtungi mdogo kabisa, na kwa kuwa imani yangu kwa Taifa Gas ilikuwa imepungua nikaamua kuupima. Amini usiamimini, nao ukawa umepungua! Nikachukua mtungi mwingine, nao ukawa umepungua vilevile hadi nilipopata mtungi wenye uzito sahihi.

Kwa uzoefu huu nawafahamisha wateja wenzangu wa Taifa Gas kuwa makini wanapobadilisha mitungi hiyo. Wito wangu kwa Taifa Gas ni kuwa watutendee haki wateja wao, mwenye duka aliniambia Oryx ndio mitungi ya uhakika, Oryx sio kampuni ka kizalendo, faida yao kwa sehemu kubwa inaenda kwa Wazungu, sasa huyu Mtanzania mwenzetu wa Taifa Gas anavyotufanyia uzalendo unaanza kunishinda.

Vv
Ni kweli aisee
 
Back
Top Bottom