Watawala Wapya UKAWA 2015 na Ndoto za Wananchi

Watawala Wapya UKAWA 2015 na Ndoto za Wananchi

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,764
Yanaweza maisha yakabadilika iwapo watawala wapya watakuwa na msimamo wa dhati wa kuyasikiliza na kuyatii wayatakayo wananchi,wakiupiga vita ufukara na wakiwatia adabu wanaopatikana na hatia ya ufisadi. Wakati huohuo wawe na mkakati madhubuti wa kujiepusha na mitego ya ulibirali mamboleo.

Vyama vya upinzani kwa upande wao vitabidi vizidishe ushirikiano wao ili viweze na kuwa mbali kutofautiana na utawala wa kiccm.
Itafurahisha kwamba vinayaangalia matatizo ya Tanzania kwa mtazamo wa kitabaka kwa sababu Tanzania ni taifa lenye ufukara mkubwa na hali za maisha za wengi wanaoishi vijijini na mijini zinazidi kudidimia na za kukatisha tamaa.

UKAWA waonyeshe kama vina mikakati madhubuti ya kuwatetea wakulima wadogowadogo vijijini au wafanya kazi wa mijini wanaoishi katika makazi duni, yaani mitaa iliyoibuka ovyo ovyo bila ya mpango. Wenzetu wa Pwani ya Kenya kwa Kiswahili chao cha Mvita huiita mitaa aina hiyo "magengeni". Asilimia 70 ya wakazi wa sehemu za mjini hapa Tanzania wanaishi katika mitaa kama hiyo.

Ubaya wa mambo ni kwamba ukuaji wa nchi, kama ulivyo ukuaji wa nchi nyingine, hauendi sambamba na upangaji madhubuti wa miji. Mipango iliyopo ni ya kiholelaholela tu ,ya kiccm toa hela jenga popote. Matokeo yake ni kutanuka ovyo ovyo na mwishowe kugeukiana na kuvunjiana. Hakuna utaratibu au nidhamu yoyote inayofuatwa.

Ukawa wajikite zaidi katika kuweka mikakati ya muda mrefu sio ya kiccm baada ya miaka selasini ,kumfanya mwananchi aridhike na maisha ya mkoani au kijijini kwake na waiondoe tabia ya kushuka DSM au kwenye miji mikuu.

Kwani wengi wao wanapotelemka mijini kutoka vijijini huwa na matumaini makubwa kwamba hali zao za maisha zitatengenea wakitumai watapata uwezo wa kufanya hivyo. Lakini kila wakilala na kuamka polepole huanza kutanabahi kwamba huo uwezo unawapiga chenga. Hawapati uwezo wowote wa kufanya chochote ila kuendelea kuishi maisha ya dhiki.Mwaka unapita, mitatu mingine inapita na hapo ndipo inapowatwanga kwamba maisha yao yataselelea vivyo hivyo.

Licha ya yote yanayowakuta watu hao hawakati tamaa. Wanapojibwaga sakafuni kwenye vigodoro vembamba au mikeka bado hulala na ndoto na huamka na ndoto. Ndoto kwamba hali zao zitabadilika ili wao pia waweze kununua bidhaa katika maduka makubwa. Ndoto ya kuwa kuna siku watakuwa wateja wa halali na sio watu wenye kuzikodolea macho tu bidhaa za anasa. Kwa bahati mbaya, tamaa huwafanya baadhi yao wawe mabazazi na wezi.

Ukawa ni lazima mucwe mnachukua ahadi za kuinua maisha ya mwananchi kwa dhati kabisa sio zile blah blah za kiccm. mwisho wa siku mnatupiga virungu,mnatuletea mgambo wa jiji,mnatuvunjia nyumba ,mnatupeleka mahakamani kwa sababu za kiuonevu kabisa zinazoshinikizwa na wenye madaraka au wenye hela. Lazima mjenge misingi ya uongozi bora kuanzia sasa .

2015 I will vote for UKAWA representatives
 
Yanaweza maisha yakabadilika iwapo watawala wapya watakuwa na msimamo wa dhati wa kuyasikiliza na kuyatii wayatakayo wananchi,wakiupiga vita ufukara na wakiwatia adabu wanaopatikana na hatia ya ufisadi. Wakati huohuo wawe na mkakati madhubuti wa kujiepusha na mitego ya ulibirali mamboleo.

Vyama vya upinzani kwa upande wao vitabidi vizidishe ushirikiano wao ili viweze na kuwa mbali kutofautiana na utawala wa kiccm.Itafurahisha kwamba vinayaangalia matatizo ya Tanzania kwa mtazamo wa kitabaka kwa sababu Tanzania ni taifa lenye ufukara mkubwa na hali za maisha za wengi wanaoishi vijijini na mijini zinazidi kudidimia na za kukatisha tamaa.

UKAWA waonyeshe kama vina mikakati madhubuti ya kuwatetea wakulima wadogowadogo vijijini au wafanya kazi wa mijini wanaoishi katika makazi duni, yaani mitaa iliyoibuka ovyo ovyo bila ya mpango. Wenzetu wa Pwani ya Kenya kwa Kiswahili chao cha Mvita huiita mitaa aina hiyo “magengeni”. Asilimia 70 ya wakazi wa sehemu za mjini hapa Tanzania wanaishi katika mitaa kama hiyo.

Ubaya wa mambo ni kwamba ukuaji wa nchi, kama ulivyo ukuaji wa nchi nyingine, hauendi sambamba na upangaji madhubuti wa miji. Mipango iliyopo ni ya kiholelaholela tu ,ya kiccm toa hela jenga popote. Matokeo yake ni kutanuka ovyo ovyo na mwishowe kugeukiana na kuvunjiana. Hakuna utaratibu au nidhamu yoyote inayofuatwa.

Ukawa wajikite zaidi katika kuweka mikakati ya muda mrefu sio ya kiccm baada ya miaka selasini ,kumfanya mwananchi aridhike na maisha ya mkoani au kijijini kwake na waiondoe tabia ya kushuka DSM au kwenye miji mikuu.

Kwani wengi wao wanapotelemka mijini kutoka vijijini huwa na matumaini makubwa kwamba hali zao za maisha zitatengenea wakitumai watapata uwezo wa kufanya hivyo. Lakini kila wakilala na kuamka polepole huanza kutanabahi kwamba huo uwezo unawapiga chenga. Hawapati uwezo wowote wa kufanya chochote ila kuendelea kuishi maisha ya dhiki.Mwaka unapita, mitatu mingine inapita na hapo ndipo inapowatwanga kwamba maisha yao yataselelea vivyo hivyo.

Licha ya yote yanayowakuta watu hao hawakati tamaa. Wanapojibwaga sakafuni kwenye vigodoro vembamba au mikeka bado hulala na ndoto na huamka na ndoto. Ndoto kwamba hali zao zitabadilika ili wao pia waweze kununua bidhaa katika maduka makubwa. Ndoto ya kuwa kuna siku watakuwa wateja wa halali na sio watu wenye kuzikodolea macho tu bidhaa za anasa. Kwa bahati mbaya, tamaa huwafanya baadhi yao wawe mabazazi na wezi.

Ukawa ni lazima mucwe mnachukua ahadi za kuinua maisha ya mwananchi kwa dhati kabisa sio zile blah blah za kiccm. mwisho wa siku mnatupiga virungu,mnatuletea mgambo wa jiji,mnatuvunjia nyumba ,mnatupeleka mahakamani kwa sababu za kiuonevu kabisa zinazoshinikizwa na wenye madaraka au wenye hela. Lazima mjenge misingi ya uongozi bora kuanzia sasa .

Mwiba,hatutakiwi kuwasubiri UKAWA,UKAWA ni mimi,wewe na yule ambao tunataka mabadiliko chanya kwa TAIFA letu kisaikolojia,kisiasa,kiuchumi,kielimu na kiafya.Tunahitaji kufanya overhaul ya hawa watawala ili watuelewe lazima tubadilike,SISI WATANZANIA na siyo UKAWA kama viongozi wa vyama.

Inabidi tuwe wamoja tusiangalie dini,itikadi za kisiasa,uchumi,elimu au ukanda sasa ndiyo wakati m uafaka wa kuelimishana,kwanini tunaumuhimu wa kupiga KURA.Watanzania wengi wamekata tamaa na hili genge la wezi wa maliasili zetu,hawajui nini wafanye,kwa sasa ni wakati wa kuelimishana na kuamka toka usingizini.Ule wakati wa kusubiri matokeo kwenye LUNINGA umepitwa na wakati twendeni sote tupige kura.

Kwa wale wanasheria.vijana,wasomi,TLS.LHRC wote hawa wanatakiwa watafute mbinu hata kama ni kupeleka mahakamani kuilazimisha serikali ifanye marekebisho ya daftari la kupiga kura na watoe muda mrefu ili wengi tujiandikishe tupige kura.

Kama India waliweza kuwaandikisha watu 100,000,000 leo kwanini tushindwa wakati tupo chini ya watu 48,000,000 wenye haki ya kupiga kura?
 
Slaa(p), Duni (vp), Warioba (pm) Lipumba (mf&p), Mbatia (MEd),Mdee (MLan), Agustino Ramadhani (MDef), , Lissu (Mlaw& Consti), Msigwa (MTour), Polepole (Myouth&Sports), ....... ongezeeni baraza hili la mawaziri
 
Spina hii combination umeitoa wapi mkuu maana vijana wa Lumumba hapa wapo chooni mchafuko wa tumbo hapo
 
UKAWA - habari ya Mujini - hutaki ingia msituni.
 
Lazima waingiye hakuna wa.kuwazuwia hicho kimbunga ukawa ndani ya magogoni 2015 sijuwi kamati ya wezi wandishi wa katiba watakuwa wapi
 
Labda UKAWA mpya na siyo ya MBOWE, LIPUMBA na MBATIA.
Na kila siku UKAWA inakuwa mpya hao uliowataja hata nao wanazidi upya wao kila kukicha ,na jamii inawakubali na inaenda kuwasikiliza kila wanapotua ,ila huko miccm mlipo ni yale kwa yale ya kuwadanganya wananchi kwa mikakati ya miaka 50.

Kila siku zikienda Miccm haya zinawatoka hawaoni hata aibu kuwachangisha wananchi ,wameua shule za serikali na lengo ni kuziimarisha zao za kulipia ,wameua hospitali za serikali wanaimarisha zao za kulipia ,mbona kwenye bunge la KATIBA hamkusema kuchangia na badala yake mkijiwekea malipo ya kila siku ,Eti jamani Nchi masikini tunawachangisha wananchi na hata watoto wa shule kuchangia madarasa ,zahanati sijui maabara ,barabara ,maguzo ya umeme ,najiuliza kwanini hamkuchangishana kuliendesha BMK ??? Na badala yake mmeenda kuiba hazina !
 
UKAWA bado upo?

Nilisubiria jawabu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ,natumai utakuwa umepata jibu tena jibu sahihi,salaam zao miccm ! UKAWA wapo na watendelea kuwepo hadi Adui CCM ametokomezwa na mafisadi kukatwa shingo.
 
Back
Top Bottom