Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,412
WATAWALA WAFANYE MARIADHIANO NA REFORMS KWA FUTURE YAO. VINGINEVYO WANATWANGA MAJI KWENYE KINU.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
1. Fikiria unapigana kufa na kupona kujenga future yako na kizazi chako ndani ya nchi yako.
2. Mungu anakubariki katika uhalali au uharamu wako unafanikiwa kujenga miradi mikubwa ndani ya nchi ambayo inagharimu mabilioni ya pesa. Ili watoto mpaka vitukuu vyako viishi maisha mazuri
3. Alafu kumbe unachofanya Leo na nguvu zote unazotumia Leo ni Sawa na bure kwani miaka ijayo Kila kitu kutaangamizwa na kuharibiwa vilivyo.
4. Kama Mtibeli nimekuwa nikisikiliza mambo mengi yanayoendelea ndani ya nchi hii. Nikiwa huru bila upendeleo wala ushawishi. Ingawaje Siku zote mimi ni mfuasi wa HAKI.
5. Baba mwenye akili huacha urithi kwa watoto wake. Na vijukuu wake.
6. Kama Baba, lazima ujiulize hivi ikitokea sipo Leo watoto wangu wataishi vizuri? Wataishi salama?
7. Urithi (Legacy) namba moja ya Baba mwenye hekima ni Jina bora lenye heshima. Kwamba unajua nisipokuwepo mtoto au mjukuu wangu akisema yeye ni mtoto wako popote pale atapata msaada na watu watampa heshima kupitia jina lako. Huo ndio urithi namba moja wa Mzazi kwa watoto wake.
8. Leo Mtibeli nikifa, ikitokea umekutana na mtoto wangu na muda huo humjui. Umemkuta labda amepata ajali au yupo kwenye hali ya uhitaji. Atakapojitambulisha ni mtoto wa Mtibeli. Je nafsi yako itashtuka kwa furaha au kwa hasira na chuki?
Kama mtibeli alikuwa mshambenga, mtenda mabaya, huna haja ya kumsaidia mtoto wangu. Na mtemee mate ajue Mimi Baba yake nilikuwa mbaya.
9. Kwa watu wenye akili, huwezi ukaishi na unawatoto kwa kuiangalia Leo tuu.
Ukishazaa na kuitwa Baba lazima uishi kwa kujiangalia wewe na watoto wako, na wajukuu, na vizazi vyako.
10. Utajiri namba moja kwa MTU au binadamu ni kuwa na Jina lenye heshima na jina safi. Huo ndio utajiri namba moja.
11. Mali huja na kuondoka. Lamborghini na magorofa ya miaka hii hayatakuwa na thamani yoyote miaka 50 ijayo. Yote yatapitwa na wakati.
12. Miji huzaliwa na hufa. Leo kariakoo inathamani lakini usishangae miaka Mia ijayo inaweza kuwa mtaa uliozeeka uliosahaulika.
13. Lakini Jina Bora halifi.
14. Wayahudi kitu pekee Wanachoringia ni Jina la Baba yao Ibrahim, Isaka na Yakobo.
15. Waarabu nao hujihusisha na Ibrahim sio kwa sababu Ibrahim alikuwa tajiri nope! Bali jina lake alilijenga kwenye heshima na usafi.
16. Kuna mbinu nyingi ya kusafisha jina kabla hujafa. Mojawapo ni kuomba msamaha kwa yote.
17. Njia zingine za kusafisha jina lako ikiwa umetenda mabaya Sana au jamii inakuchukia ni pamoja na njia hizi
a) Kuomba Msamaha
Lazima ukiri kwamba ulikosea. Ulikuwa mbinafsi. Ulionea watu na kuwaumiza.
Maisha yako uliyatumia vibaya kudhuru wengine. Lazima u- submit
Kisha ufanye toba mbele za watu ikiwa wewe ni public figure. Kwani huenda umekosea wengi na huwezi kuwafuata mmoja baada ya mwingine.
Lakini kwa wale ambao sio public figures unaweza mfuata uliyemkosea Sana na kuharibu maisha yake. Kisha omba toba
b) Rudisha uliyochukua Kwa uliowakosea.
Hakuna msamaha bila kurudisha uliyoyaiba na kudhulumu. Huo msamaha haupo.
Kama ni public figures umefanya dhulma kwa watu wengi katika maisha yako. Na huwezi kuwakumbuka wote. Mbinu nzuri ni kuirudisha Mali hizo kwenye Jamii. Zirudishe zote ulizodhulumu.
Pesa zingine anzisha foundation za kusaidia watu hasa wenye Hali ulizowadhulumu.
Mfano; Kama ulikuwa unadhulumu haki za watu kisiasa, anzisha foundation ya kusapoti wanaharakati wa kutetea haki za kisiasa.
Kama ulikuwa unadhulumu haki za wanawake au makundi Fulani. Anzisha foundation za kupigania na kusaidia wanawake.
Motivation kubwa ya foundation na misaada ni hiyo. Kusafisha jina, kuomba toba na kuungama.
c) Kufanya Maridhiano na kuomba hukumu kwa wanadamu
Kama hutaki hukumu ya Mungu basi lazima ukubali hukumu ya wale uliowakosea.
Kikawaida ukishamalizana na uliowakosea Mungu hana muda na wewe
Unaomba omba msahama kule juu. Wapo watu watataka uadhibiwe. Kubali upo tayari kupewa adhabu kwa yote uliyoyafanya. Hiyo ndio toba ya kweli
Huwezi sema unataka toba alafu muda huohuo hutaki adhabu ya uliyoyafanya. Hiyo haipo.
17. Nasema hivi kwa sababu miaka yetu ni michache Sana. Leo tupo Kesho hatupo. Kuwa kiongozi sio kwamba mauti inakuchukulia tofauti.
18. Leo upo Kesho haupo. Nini kitatokea kwa watoto na wajukuu zao Siku ukuondoka?
19. Je jamii itaungana na kuwatetea watoto na kizazi chako? Au je ndio waatasema afadhali umeondoka, tazama watoto wake hawana tena mtetezi.
20. Unapoishi kwenye maisha lazima ujue maisha ya watoto wako msingi wake mkuu ni wewe. Sio ndugu wala Rafiki zako
21. Usipojiandaa sawasawa Kila kitu kitaisha. Kitaharibika. Na nguvu ulizotumia miaka yote itakuwa ubatilli mtupu. Sawa na bure.
Kufikia hapa sina la ziada.
Nawatakia maandalizi mema ya Sabato.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam