Watawala wa kike katika nchi za Kiislamu

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,571
19,453
Watu wengi huamaini kuwa nchi za kiislamu huwa haziwaheshimu wanawake na haziwezi kutawaliwa na wanawake. Hata hivyo miaka ya hivi karibuni imeonakana kuwa hilo siyo kweli kwani kule Pakistani walitawaliwa na mwanamke Benazir Bhutto kwa muda mrefu kabla hawajamuua.

Ninataka kuchokonoa historia ya mtawala mmoja wa kike kule Nigeria ya kaskazini kwenye jamii ya wahausa ambayo ni ya kiislamu kwa muda mrefu sana aliyekuwa akiitwa malkia Amina. Mama huyu alitawala takriban miaka 200 kabla ya ujio wa Usman dan Fodio ambaye ndiye anyejulikana sana eno hilo kihistoria. Amina alikuwa ni mtoto kwanza wa mfalme Nikatau aliyekuwa anatawala kule kaskazini mwa Nigeria. Alikuwa na wadogo zake watatu; mdogo wake wa kiume alikuwa mtoto wa pili wa mfalme Nikatau alikuwa akiitwa Karama, halafu mdogo wake wa kike alikuwa akiitwa Zaria; leo hii kuna mji kule kaskazini mwa Nigeria unaitwa Zaria kwa sababu ya huyu mdogo wake wa kike.

Amina alijifunza kupigana vita angali kigoli wakati akiwa anaishi na babu yake; baada ya baba yake kufa, mdogo wake wa kiume ndiye aliyerithi ufalme wakati Amina akiwa anendelea na maisha ya kijeshi ya kupigana vita aliyokuwa amejifunza kutoka kwa babu yake; alikuwa msichana mrembo sana ambaye pamoja na ushujaaa wake wa kijeshi wanaume wengi walitaka kumwoa lakini hakuna aliyefanikiwa. Baada ya kukaa madarakani kwa miaka kumi, kaka yake, yaani mfalme Karama, naye alifariki, na hivyo Amina kuchukua mamlaka ya kuwa mtawala wa eneo hilo akijulikana kama malkia Aminatu.

1604302827912.png

Malkia Aminatu anakumbukuwa sana kwa kuliendeleza eneo la Zaria hadi kuwa kitovu kikubwa cha biashara kaskazini mwa Nigeria kama ilivyo leo.
 
Kumbuka huyu alitawala Nigeria kaskazini ikiwa ni hapa Afrika, tutajie watawala wanawake wa nchi za Kiarab....!
Nimesema nchi za kiislamu, siyo nchi za kiarabu. Ukishasema uarabuni, usisahau kuwa hata israel ni sehemu ya uarabuni ambayo licha ya wayahudi ina pia waislamu wengi sana na iliwahikutawaliwa na mwanamke Golda Meir
 
Nigeria si nchi ya Kiislam, au ulikuwa hujuwi hili? Nothern Nigeria ni kama jimbo ndani ya nchi na si nchi.
 
Ya tano; karne hukamika baada ya miaka 100. Samahani kule nyuma nilisema karne ya nne.
Hiyo ni karne ya sita...
hakukuwa na karne ya zero kwahyo
1-100 karne ya kwanza
100-200 ya pili
200-300 ya tatu
300-400 ya nne
400-500 ya tano
500--600 ya sita
600-700 ya saba

Na bado sio kwamba alizaliwa tu na uislam ukaanza...ulianza akiwa na 40+years kwhyo ni kwenye miaka ya 600's karne ya saba
 
Hiyo ni karne ya sita...
Na bado sio kwamba alizaliwa tu na uislam ukaanza...ulianza akiwa na 40+years kwhyo ni kwenye miaka ya 600's karne ya saba
Mimi siyo mwanahistoria ya dini ya kiisalamu ila Malkia Amina alikuwa mwislamu. Inawezekana nimekosea kwenye miaka ila eneo lote kaskazini mwa Nigeria ni waislamu kutokanana uzawa huo. Malkia yule alitawala kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1500 hadi katikati ya miaka ya 1600. hHiyo ni zaidi ya miaka1000 tangu kuzaliwa kwa mwanzilishi wa uislamu!
 
Okay sawa...lakini pia unapoweka makala jaribu kutoa conclusion yenye logic katika maoni yako.
Umeanza kwa kusema watu husema nchi za kiislam zinakandamiza wanawake(ukaonesha nia ya kutaka kuipinga hii notion)
Ukatoa mfano wa mtawala wa nigeria miaka 1000 iliyopita

kabla watakaokupinga hawajaenda kuhakiki facts kama (kweli huyo Amina aliexist? au alikuwa muislam? au alisilimu akiwa tayari malkia au aliweza kutawala kwasababu Waislam walikuwa wachache hawakuweza kumpinga nk. nk.)

kabla watu hawajafanya hivo ungeweka conclusion yako
Je, nchi za kiislam hazikandamizi wanawake kwasababu ya Amina?

Mfano: Mtu akisema Wakatoliki wanavaa rozali mimi nikapinga kwasababu jirani yangu ni mkatoliki ila havai nitakuwa sahihi?
Njia pekee ya kupinga ni kurejea maandiko ya kikatoliki kama yanasapoti/kupinga uvaaji wa rozali ndipo hoja yangu itakuwa na mashiko

Nawewe naomba uconclude habari yako kuhusu Amina inatufundisha nini?
Na je, marejea ya uislam yanasapoti alichofanya amina au La
 
Hukumu za kiislamu hazitenguliwi wala kubadilika kwa yale wanayoyafanya waislamu.

Uislamu unasemaje kuhusu kutawaliwa na mwanamke?

Ishu sio watu wanatawala,ishu je uislamu unasemaje kuhusu wanawake kutawala?

Tukiangalia nini wanafanya waislamu mwishowe tutakuja kusema zinaa sio haramu kwa sababu waislamu wengi na Nchi nyingi za kiislamu zinaa inafanyika,sasa tukiangalia watu hatutajua uislamu.

Tusiangalie waislamu wanafanyeje,Tuangalie uislamu unasemaje?
 
Maswali yako yote ni magumu sana kwangu; hebu saidia kutupa ufumbuzi wake!
 
Back
Top Bottom