Watasimama au hawatasimama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watasimama au hawatasimama?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Mar 5, 2008.

?

Je, walioiba fedha za EPA na kuamua kurudisha kiasi fulani:

Poll closed Mar 8, 2008.
 1. Watasimamishwa kizimbani kujibu mashtaka mazito?

  3 vote(s)
  17.6%
 2. Watashtakiwa kwa makosa madogo tu?

  2 vote(s)
  11.8%
 3. Hawatashitakiwa kwa vile wamerudisha fedha kiuungwana.

  9 vote(s)
  52.9%
 4. Sijui wala sijali - sina la kusema lolote lile halinihusu.

  3 vote(s)
  17.6%
 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Mar 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tunasubiri kuona kama ripoti ya EPA licha ya kutaja walioiba fedha zetu na kuzirudisha kinyemela itatuambia pia kuwa watasimamishwa mahakamani kwa kuhujumu uchumi, kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu, kuiibia serikali ya Jamhuri, kughushi, kukutwa na nyara za serikali, kutoa taarifa za uongo, na kuingilia upatikanaji wa haki (obstruction of justice - sidhani kosa hili lipo TZ.. wanasheria mtanisahihisha).

  Kwa vile tuko katika kusubiri naona tujaribu kupiga kura unafikiri vipi kuhusu uwezekano wa wezi wa EPA kusimamama mahakamani baada ya kurudisha kiasi kikubwa cha fedha?
   
 2. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Sheria inasema vipi??Maneno matupu hayavunji Mfupa
   
 3. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inavyoelekea hawa hawasimami kizimbani wala nini. Kama hukujua msanii namba moja ndiye yuko in control hapo Tanzania basi hii itkuwa moja ya uthibitisho wa haya!
   
 4. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  wewe unatoa Hoja Gani,Mbona haujasimama mbele ya watanzania kuelezea machungu yako??tusiwe wanasiasa wa huku kwenye majukwaa.tuwe kama ndugu yetu Mtikila.tujitokeze tuelezee ..mapambano ya kalamu tu hayatoshi..
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2008
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Mama aliyebeba mtoto mgongoni, kwa bahati mbaya akajamba mbele ya watu, anapeleka mkono nyuma, anampiga mtoto kidogo huku akisema 'we mtoto unajamba mbele za watu!' au Mtu mzima/anayejiona anastahili heshma, akijamba mbele za watu, anachukua kijiti kilichombele yake na kumpigia mbwa huku akisema 'we jibwa unachafua hewa hapa toka!'

  bila shaka hii ndiyo stahili itakayotumika hapa.
   
 6. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona unataka kubadili katiba ya Tanzania ili kila anayejadili maslahi ya nchi yake atakiwe kupanda majukwaani au kuwa mwanasiasa!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Mar 5, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Gembe, vitani siyo wote wapambanao wanashika Bunduki, na siyo wote wanaosababisha ushindi vitani wanakuwa mstari wa mbele!! Ukielewa hili utaona kuwa katika mapambano haya kuna wapambanaji tofauti na kwa kadiri siku zinavyoenda ndivyo ambavyo nafasi za wapambanaji hao zinavyobadilika na kuchukua sura tofauti tofauti.

  Wengine wanapambana mahakamani (kama kina Mtikila), wengine wanapambana kwenye sanduku la kura (kama wapinzani); wengine tunapambana katika kuteka fikra (kwenye vyombo vya habari) n.k Sasa ukitaka wote tuende mahakamani, nani ataripoti yanayotokea mahakamani na kuyakosoa au kuyapongeza?

  tukubali kwamba sheria ya "division of labour" applies pia kwenye mapambano ya kuliamsha Taifa; tusidhani kuwa walioko Mahakamani ni bora zaidi au waandishi ni bora zaidi; tukianza kufikiri hivyo, adui anaona udhaifu wetu na hivyo ni rahisi kwake kushinda.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  kuna dalili kuwa wahusika wetu wa EPA watafikishwa mahakamani wiki ijayo au ndani ya wiki mbili zijazo. Swali kubwa ambalo wachunguzi kama mimi tunajiuliza ni kwa kosa gani hasa baada ya kurudisha kiasi kingine kikubwa cha fedha wiki hii. Kuna mambo kadhaa yanayowezekana.

  a. Wale waliorudisha fedha (matajiri wakubwa) watafikishwa kwa kosa la kughushi au jingine dogo ambapo watatakiwa walipe faini nyingine ya tumilioni fulani na kukwepa kifungo.

  b. Wale visangara vidogo vidogo ambao kwa muda wa wiki zote hizi wameshindwa kurudisha fedha zozote na mali zao zisizohamishika (ambazo wao wamezitaja kwa hiari) zinachukuliwa na serikali na wao wenyewe watapa kibano cha miezi michache Maweni.

  c. Na wale ambao wanaona suala zima halina mpango ambao niliripoti siku uchunguzi wa EPA umetangazwa kuwa wameonekana wakitimka pale Kipawa; mtaambiwa watafikishwa mahakamani na hawapo nchini.

  Na watanzania mtatakiwa kupiga makofi!!!
   
 9. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #9
  Mar 8, 2008
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sheria ya uhujumu wa mali ya taifa inasemaje?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Mar 8, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Iko hapa na wanaweza kuitumia kwa "baadhi" yao... lakini sitoshangaa kwamba hawataitumia kwani Mwanyika alipoulizwa wakati mambo haya yanaanza alikuwa anajiuliza ni sheria gani ataangalia lakini hakuitaja hii...
   

  Attached Files:

 11. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #11
  Mar 8, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mapambano dhidi ya ufisadi ni popote na vyovyote.

  Si wote tutasimama mahakamani kupambana na ufisadi wala si wote tutaandika magazetini.

  Hata yule msomaji wa JF au gazeti lenye habari za mpambano aweza ingia vitani kwa kusambaza taarifa aloisoma afikapo kijiweni kwake.

  Kitendo cha wananchi kugoma kupiga makofi au kuguna na kuzomea katika mikutano ya hadhara inayohutubiwa na mafisadi ni mapambano tosha.

  Mafisadi nao walianza kwanza kudanganya majukaani kisha wakauona mwanya wa kutuibia mchana kweupe na kutufikisha hapa tulipo.

  Sisi pia tutapambana nao kwa mtindo huo huo,kwanza tunaanza kusema majukaani na mwisho tutachukua hatua madhubuti na kuwabana kisheria.

  Hakuna kokoto itabakia imesimama juu ya kokoto, sembuse jiwe

  Mapambano ni popote na vyovyote.
   
 12. M

  Masatu JF-Expert Member

  #12
  Mar 9, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  The fact kuwa mpaka leo hata kuwataja majina wanapatwa na kigugumizi, I really dont expect anything serious...
   
 13. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #13
  Mar 9, 2008
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  M.M.M, hapo nimeiona hiyo..... Duh, unajua hapo upo sawa kwamba kuna baadhi ya sheria ambazo tulizipitisha wenyewe......

  Mtego upo pale kwenye nani wa kukaa/kutoa hukumu, itakuwa kama kumfunga paka kengele manake anatakiwa a Saint (do we still have these in our legal system??)

  Haya tungojee wiki hizo mbili tuone yatakayojiri, pia nitakuwa kati ya wale tutakao angalia kama AG atatumia sheria yetu hii ya 1984!!
   
 14. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2008
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,042
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tusubiri Tuone.......is The Matter Of Time...!
   
Loading...